Hatua kwa hatua uchimbaji madini ya dhahabu

Hatua kwa hatua uchimbaji madini ya dhahabu

Ng'wanapagi

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2013
Posts
9,116
Reaction score
8,652
AINA YA UCHIMBAJI
Unaweza kuchimba dhahabu kama:
1:Mtu binafisi
2:Kikundi
3:Ushirika
4:Kampuni

A: MTU BINAFISI
Hapa wewe ndiye utakuwa mkurungezi (boss). Gharama zote za uchimbaji utahusika wewe. Kununua vifaa vyote vinavyohitajika katika kazi,chakula, nyumba za wafanyakazi (mara nyingi ni nyumba temporary hususani za maturubai ama mabati) kutokana na idadi ya wafanyakazi pia huduma za hospita utahusika pindi mfanyakazi atakapokuwa mgojwa. Utawalipa mshahara endapo mkataba wenu utakuwa kulipana au utawapa posho lakini pindi uzalishaji ukianza utawapatia hisa (asilimia ambazo mtakuwa mmekubaliana)

KIKUNDI
Hapa wote mtakuwa wamiliki na mtachangia mtaji kukidhi mahitaji kama niliyoyataja hapo juu. Aidha mtatetua mwenyekiti wa kikundi,katibu wa kikundi, msimamizi wa wafanyakazi (afisa uajiri), Afisa usalama wa uchimbaji no

USHIRIKA
Kiutaratibu unalingana kama uchimbaji wa Kikundi isipokuwa katika Ushirika kutahusisha watu wenye elimu Zak

KAMPUNI
Utaratibu ni kama ule wa Ushirika na majukumu ni yaleyale isipokuwa kampuni vifaa vya uchimbaji vitakuwa bora kutokana na mtaji mkubwa au wa wastani

ENEO LA UCHIMBAJI

(i)Uchimbaji wa kienyeji

Uchimbaji huu huhusisha kuchimba eneo ambalo lina historia ya uwepo wa madini haya ama kuna uchimbaji unaendelea.
Katika uchimbaji huu wachimbaji au mchimbaji huchimba kwa "hisia" kutokana na uelekeo wa mwamba wa madini (reef) ilikoelekea pia kwa wale wazoefu huhusisha pia kuangalia aina ya mimea iliyopo eneo hilo na rangi ya udongo. Uchimbaji huu huwa ni bahati na sibu

FAIDA ZAKE
*Hauhitaji mtaji mkubwa kuanza uchimbaji
*Hauhitaji vipimo vya madini kujua kina na mwelekeo wa reef ulivyo
*Huhusisha vifaa vya kizamani
*Uchimbaji huu huhusisha kuvamia eneo la kuchimba bila kibali (leseni)

HASARA YAKE
*Kushindwa kufikia mwamba wa madini kutokana na kina au kukosea mwelekeo wake
*Kutumia muda mwingi bila malengo change
*Kufukuzwa na mwenye leseni au kugawana na mwenye leseni huku nguvu na gharama kubwa umetumia wewe
*Kujiingiza katika imani za kishirikina

UCHIMBAJI WA KILEO (NIMESHINDWA KUSEMA WA KISASA SABABU NI GHARI SANA)
Katika uchimbaji huu mara nyingi unafanywa na watu wenye mtaji wa wastani na makampuni hususani ya Kitanzania au kikundi cha wachimbaji.

Hatua ya kwanza humtafuta mtaalamu wa miamba (jiolojisti) na humlipa kwa kazi ya kuwaonyesha sehemu na mahali pa kuchimba dhahabu katika uchimbaji huu jiolojisti hutumia ramani za madini na njia za kissasa mfano GPS kubaini kama eneo hilo lina leseni ya mtu, mwamba wa madini ulipo na uelekeo wake kwa kutumia mashine special inayo scan ardhi ambapo pia jiolojisti hubaini kama ardhi hiyo ina maji au haina ili kubaini gharama ambazo utakumbana nazo wakati wa uchimbaji na ubora wa dhahabu za eneo husika.

FAIDA YA UCHIMBAJI HUU
Faida zake ni uhakika wa kazi unayoifanya kama itakuwa na matokeo chanya au hasi na katika uchimbaji huu bado kitaalamu wanakuambia ni "UTAFITI"

HASARA ZA UCHIMBAJI
*Unahitaji mtaji kwa mfano kupata leseni na kumlipa mtaalamu wa miamba
*Wachimbaji wengi hukata tamaa hususani wakiambiwa mwamba uko kina kirefu hivyo gharama za kuendesha shughuli kuwa kubwa na kuchukua muda mrefu

SHUGHULI YA UCHIMBAJI
Maandalizi ya kuchimba: Hatua ya kwanza

Mara baada ya kupitia hatua nilizozitaja hapo juu (kupata leseni na jiologisti kukuonyesha sehemu ya kuchimba ama kwa wewe ambaye huhitaji kuwa na leseni (mchimbaji wa kienyeji) ni vyema kumtafuta mmiliki wa shamba au ardhi kumuomba kufanya kazi hiyo ya uchimbaji katika shamba lake au ardhi yake. Katika maongezi yenu/makubaliano yenu mtaweka maandishi na kila mmoja wenu kubaki na nakala na nakala nyingine mtapeleka kwenye ofisi ya Serikali ya eneo husika (kijiji) na baadae mtapeleka kusajiri shampo lenu (shimo au duara kwa lugha ya usukumani) kwenye ofisi ya uchimbaji iliyoko eneo au jirani na mnakochimba madini hayo ambapo mkaguzi wa maduara (inspector) atakuja kuwatembelea mara kwa mara kukagua usalama wa shimo na kutoa ushauri. Hii itakulinda wewe mwenye duara endapo itatokea ajali katika eneo lako la kazi.

MAHITAJI
(A)Jenga kibanda cha kulala wafanyakazi mara nyingi hutumia maturubai ila ushauri hapa ni kununua mabati na kuezeka kwani maturubai yanayotengenezwa na viwanda vyetu mara nyingi sio imara na huchanika haraka sana hasa upepo ukiwa mkubwa. Tumia miti pori kama mbao ili kuepuka gharama. Weka sakafu ya kokoto au molamu kama huna uwezo wa kununua simenti. jenga kibanda chenye vyumba vitatu (chumba kimoja cha wafanyakazi wa kike hususani mpishi, cha pili wafanyakazi wa kiume cha tatu kuhifadhia vyombo,mkaa na vifaa vya kazi. Unaweza kuajiri mlinzi ukipenda

(B)Nunua vifaa kama koleo, nyundo kilo 6 au nane, moko na tindo, gunia au madumu ya kutolea kifusi madini toka shimoni, kamba ngumu na imara, turubai kwa ajili ya kukinga jua na mvua eneo la shimo kipindi chote cha uchimbaji ili kuepuka gharama za usafiri na emergency routes ni vizuri ukawa na usafiri ambao utakupeleka eneo la kazini na kukurudisha pia utatumika kufuata mahitaji pindi yanapojitokeza. Aina ya usafiri hapa nakushauri uwe na PIKIPIKI na kama una uwezo basi uwe na gari aina ya pickup.

(C)Nunua au kodi mashine ya kupeleka hewa chini hususani Blower pamoja na jenereta ambayo itasaidia kutumika na Blower kama chanzo cha umeme

(D) Ni mara chache sana kuipata dhahabu bila uwepo wa maji chini hususani ukanda wa Geita na Kahama (Shinyanga) hivyo andaa mfumo wa kutoa maji chini hii inahusisha kukodi au kununua mashine yenye uwezo wa kusukuma umeme wa 3phase kwani pampu zinazofaa kwenye uchimbaji ni zile zinazotumia umeme wa 3phase pamoja na "Mota" ya 15Amp. Hata kama eneo lako litakuwa halina maji basi utaitumia kuikodisha kwa wenye mashimo yenye maji na hapo utapata pesa au kupewa share kwenye duara zenye uzalishaji.

ITAENDELEA............
 
👏👏👏 GGM hoyeee nimepiga mzigo sana kule magema, mpomvu n.k miaka hiyo nilikuwa ni mtu niliyeona njaa kwa macho ndio maana nimekuwa mkatili 😝😝😝
 
Back
Top Bottom