Hatua muhimu utafutapo mwenza.

Hatua muhimu utafutapo mwenza.

Daby

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2014
Posts
33,894
Reaction score
76,810
Kila mtu huwa na taswira ya mke/mme amtakaye. Ni kweli kabisa, maisha hayana kanuni lakini nakuhakikishia kanuni zipo, haipo moja zipo nyingi.

Ili maisha yaende kama ulivyopanga lazima uwe na mipango "hii mipango ndiyo kanuni". Moja ya mipango mikubwa ni kuchagua mwenza wa maisha. Nisiandike saana. Unapoamua kutafuta mwenza wa maisha jaribu kumpitisha kwenye hizi hatua anuai.

1. Mahali ulipo.

Hili lipo wazi tunapenda na kuchagua wenza sahihi kwa mahalu tulipo na wakati tunaokuwa nao. Huwezi kumpenda mtu wa Msumbiji ilihali upo Vingunguti otherwise ulishafika Msumbiji. Kwenye hii hatua ya kwanza, mosi uwe na nia ya kutafuta mwenza. Kisha angalia waliopo ulipo na uwaainishe. Wapeleke hatua ya pili.

2. Jamii ya mwenza mtarajiwa.
Kwenye jamii tunazoishi kuna mila na taratibu za mfumo wa kuoana. Bila shaka nawe jamii yako inazo hizo taratibu. Hivyo baada ya kuangalia wanawake/wanaume waliopo katika mazingira uliyopo wachuje kwa taratibu za jamii yako. Je, wanaoendana na taratibu za jamii yako? Hao watakaoendana nazo nenda nao hatua inayofuata.

3. Mvuto hasa wa nje.

Wale uliotoka nao hatua ya pili vipi unavutiwa nao? Kwa mara ya kwanza ulipowaona walikuvutia! Wale ambao hujavutiwa nao waache kwenye hii hatua beba wale uliovutiwa nao. Nenda nao hatua inayofuatia.

4. Utangamano.

Kwa kimombo compatibility. Maana yake je mnaweza kwenda sawia???

Hapa utakao vutiwa nao angalia wanavyopendelea, tabia zao na mipango yao ya maisha. Je, inaendana na yako? Mtaweza kuendana? Yes. If no achana naye chukua waliobaki nenda nao hatua inayofuatia.

5. Nakosa neno sahihi la kuweka hapa. Hii hatua tuiite Returns/ compesation/faida atakayo kuongeza.

Hii hatua imekaa kibiashara zaidi ila ni ya muhimu saana. Sasa wale mlioendana hatua ya 4 walete hapa napo wachuje.

Je, atakuongezea nini kama mwenzi wa maisha? Atakuwa kupe au nyuki? Anao msaada wowote kwako? If exchange is reasonable, then choose her/him.
Kama hana returns zozote tupilia mbali.

NB : kwenye kila ulifanyalo usisahau imani yako.

Mengi yametoka kwa afande google.
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106] mkuu tunafanyaje maana ukigusa tu unakuta mtu ana character za kupe. Kwahiyo tusiwowe????

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa mujibu wa hizi hatua "kuntu" sikushauri mkuu.

Unawezaje kuishi na binadamu asiye na faida kwako?
 
Yani umeshuka vizur,
But hapo kwenye NB ndo ukaja kutaga,
Kwasababu iman bila Mungu imekufa, haiwez kufanya kitu.

So unatakiwa ujue
Unatumia nguvu gani,
Upo kwa Mungu au kwa shetani.
Wew peke ako huwez toa muujza wowote utaangukia pua tu.

NB: Mungu wetu aliye juu, hakuna anae weza kumshinda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani umeshushuka vizur,
But hapo kwenye NB ndonukaja kutaga,
Kwasababu iman bila Mungu imekufa, haiwez kufanya kitu.

So unatakiwa ujue
Unatumia nguvu gani,
Upo kwa Mungu qu kwa shetani.
Wew peke ako huwez toa muujza wowote utaangukia pua tu.

NB: Mungu wetu aliye juu, hakuna anae weza kumshinda.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwenye hiyo NB umesema ukweli mtupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani umeshuka vizur,
But hapo kwenye NB ndo ukaja kutaga,
Kwasababu iman bila Mungu imekufa, haiwez kufanya kitu.

So unatakiwa ujue
Unatumia nguvu gani,
Upo kwa Mungu au kwa shetani.
Wew peke ako huwez toa muujza wowote utaangukia pua tu.

NB: Mungu wetu aliye juu, hakuna anae weza kumshinda.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe unayo haki ya kushutumu imani ya mtu mwingine kuwa ni mbaya mzee baba?
 
Back
Top Bottom