Hatua saba za muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Sifael Mpollo

Member
Joined
Jan 20, 2018
Posts
25
Reaction score
37
Leo tarehe 26 Aprili 2026, Tanzania inaadhimisha miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (1964 - 2026). Hata hivyo, hatukutakuwa na maadhimisho ya kitaifa kwa sababu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza fedha zilizokuwa zimepangwa kugharamia maadhimisho ya Sherehe za Muungano mwaka huu, zitumike kukarabati miundombinu ya barabara iliyoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 62 ya Muungano yatafanyika katika ngazi ya mikoa yote nchini ambapo viongozi wakuu wa kitaifa watafanya shughuli za kutembelea, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi ya maendeleo. Aidha, wakuu wa mikoa wameelekezwa kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mipya, sambamba na kushiriki shughuli za usafi wa mazingira, upandaji miti na michezo mbalimbali.

Ni vyema siku ya leo tukakumbushana hatua saba za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

1. Mazungumzo ya Siri ya Viongozi wa Tanganyika na Zanzibar.
Waasisi wa Muungano, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume, kuwa na mazungumzo ya siri wao na viongozi wengine kwa niaba ya wananchi.

Mazungumzo hayo yalikuwa yakifanyika pande zote mbili za Muungano, yakiratibiwa na kusimamiwa na wao wenyewe ili kuepusha kuvuja kwa siri kutokana na mazingira ya kisiasa yaliyokuwepo wakati ule, ambapo Zanzibar ilitokea katika kupata uhuru wake wa kweli kupitia Mapinduzi.

Ikumbukwe kuwa, Muungano ulifanyika miaka miwili na miezi minne ya Uhuru wa Tanganyika uliopatikana tarehe 9 Desemba 1961 na miezi mitatu tu baada ya kufanyika Mapinduzi ya Zanzibar ya tarehe 12 Januari 1964 na Muungano ukafanyika tarehe 26 Aprili 1964.

1. HATUA YA KWANZA..jpg

2. Utiaji saini wa hati ya makubaliano ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (22 Aprili 1964).

Tarehe 22 Aprili 1964, kwa niaba ya wananchi wote wa Tanganyika na Zanzibar Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Tanganyika Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Serikali wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume walisaini hati ya makubaliano ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Utiaji saini wa hati ya makubaliano ya Muungano ulifanyika katika Ikulu ya Zanzibar.

Wakati mkataba wa Muungano unasainiwa, Rais Nyerere aliambatana na Roland Brown (Mwanasheria Mkuu wa Serikali), P.R.N Fifoot (Mwandishi Mkuu wa Sheria), Oscar Kambona (Waziri wa Mambo ya Nje), Job Lusinde (Waziri wa Mambo ya Ndani) na Bhoke Munanka (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais).

Kwa upande wake, Rais Karume wa Zanzibar aliambatana na Abdulla Kassim Hanga (Makamu wa Rais wa Zanzibar), Abdulazizi Twala (Naibu Waziri Afisi ya Rais) na Ali Mwinyigogo (Msaidizi wa Rais Ikulu).

2. HATUA YA PILI..jpg

3. Baraza la Mapinduzi na Bunge la Tanganyika Kuridhia Hati ya Makubaliano ya Muungano (25 Aprili 1964).

Tarehe 25 Aprili 1964 Hati ya Makubaliano ya Muungano iliridhiwa na mamlaka za kutunga sheria.

Baraza la Mapinduzi ambalo lilifanya kikao chake asubuhi ya siku hiyo ya tarehe 25 Aprili 1964 Ikulu, Zanzibar na Bunge la Tanganyika lilifanya kikao chake siku hiyo jioni katika ukumbi wa Bunge wa Karimjee, Dar es Salaam.

Wakati Zanzibar ikiridhia Hati ya Makubaliano ya Muungano, Mwalimu Nyerere alimtuma Oscar Kambona (Waziri wa Mambo ya Nje) kama mjumbe wake kwenda kushuhudia tukio hilo baada ya kupewa mwaliko kutoka kwa Rais Karume.

Vilevile, Rais Karume kupitia mwaliko aliopata kutoka kwa Mwalimu Nyerere alimtuma Salim Rashid (Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi), kwenda kushuhudia tukio la kuridhia Hati ya Makubaliano ya Muungano

Kwa mujibu wa sheria ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Sheria Na. 22 ya mwaka 1964, Sheria ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika ya mwaka 1964 pamoja na Hati ya Muungano ziliweka bayana kuwa, baada ya kuridhiwa kwa Hati ya Makubaliano ya Muungano, siku inayofuata ndiyo itatambuliwa rasmi kuwa ni siku ya Muungano.

Hivyo, tarehe 26 Aprili, 1964 ikawa ndio siku rasmi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

3. HATUA YA TATU. A..jpg

4. Bunge la Jamhuri ya Muungano Kuanza Kazi (27 Aprili 1964).

Tarehe 27 Aprili 1964 ndiyo siku ambayo Bunge jipya la Jamhuri ya Muungano lilianza kazi.

Moja ya matukio makubwa katika tarehe hiyo ilikuwa ni kubadilishana Hati ya Makubaliano ya Muungano, tukio ambalo lilifanyika katika Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam wakati wa kikao cha Bunge cha jioni.

Pia, siku hiyo waliapishwa viongozi wa Jamhuri ya Muungano wakiongozwa na Sheikh Abeid Amani Karume.

4. HATUA YA NNE. A.jpg

4. HATUA YA NNE. B.jpg

3. HATUA YA NNE. D..png

5. Kuundwa kwa Baraza la Mawaziri la Muungano (28 Aprili 1964).

Tarehe 28 Aprili 1964 Baraza Jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lenye Mawaziri 23 liliapishwa katika Ukumbi wa Karimjee, watano kati yao kutoka Zanzibar.

Kuapishwa kwa Baraza hilo ilikuwa ni kielelezo cha kwamba, Serikali ya Muungano imeanza kazi rasmi.

5. HATUA YA TANO..jpg

6. Kutuma Taarifa Umoja wa Mataifa (UN).

Tarehe 30 Aprili 1964 Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ilimjulisha Katibu wa Umoja wa Mataifa, Bw. U Thant kuwa Nchi za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zimeungana na kuunda nchi moja inayoitwa "Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar".

Mwezi Oktoba, 1964 Bunge la Jamhuri ya Muungano lilabadili jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Sheria ya kubadili Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ya mwaka 1964.

Kufuatia mabadiliko hayo, tarehe 2 Novemba, 1964 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alifahamishwa kuhusu mabadiliko ya jina la nchi naye alikiri kujulishwa tarehe 18 Desemba, 1964.

6. HATUA YA SITA..jpg

7. Kuchanganya kwa Udongo wa Tanganyika na Zanzibar (26 Aprili 1965).

Tarehe 26 Aprili 1965, lilifanyika tukio la kuchanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar lilifanyika katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kama alama ya kudhihirisha Muungano wa udugu wa kudumu.

Tukio hili lilikuwa ni sehemu ya shamrashamra za sherehe za kuadhimisha mwaka mmoja wa Muungano

Sehemu ya udongo huo ilitumika kupanda mti wa mwembe katika Viwanja vya Ikulu ya Dar es Salaam ambapo upo hadi sasa.

7. HATUA YA SABA. A..jpg

7. HATUA YA SABA. B..jpg
 
Attachments

  • 2. HATUA YA PILI..jpg
    2. HATUA YA PILI..jpg
    66.2 KB · Views: 23
  • 3. HATUA YA TATU. B..png
    3. HATUA YA TATU. B..png
    550.8 KB · Views: 23
  • 2. HATUA YA PILI..jpg
    2. HATUA YA PILI..jpg
    66.2 KB · Views: 26
Kwenye huu muungano watanganyika tumepigwa na kitu kizito
 
Leo tarehe 26 Aprili 2026, Tanzania inaadhimisha miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (1964 - 2026). Hata hivyo, hatukutakuwa na maadhimisho ya kitaifa kwa sababu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza fedha zilizokuwa zimepangwa kugharamia maadhimisho ya Sherehe za Muungano mwaka huu, zitumike kukarabati miundombinu ya barabara iliyoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 62 ya Muungano yatafanyika katika ngazi ya mikoa yote nchini ambapo viongozi wakuu wa kitaifa watafanya shughuli za kutembelea, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi ya maendeleo. Aidha, wakuu wa mikoa wameelekezwa kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mipya, sambamba na kushiriki shughuli za usafi wa mazingira, upandaji miti na michezo mbalimbali.

Ni vyema siku ya leo tukakumbushana hatua saba za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

1. Mazungumzo ya Siri ya Viongozi wa Tanganyika na Zanzibar.
Waasisi wa Muungano, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume, kuwa na mazungumzo ya siri wao na viongozi wengine kwa niaba ya wananchi.

Mazungumzo hayo yalikuwa yakifanyika pande zote mbili za Muungano, yakiratibiwa na kusimamiwa na wao wenyewe ili kuepusha kuvuja kwa siri kutokana na mazingira ya kisiasa yaliyokuwepo wakati ule, ambapo Zanzibar ilitokea katika kupata uhuru wake wa kweli kupitia Mapinduzi.

Ikumbukwe kuwa, Muungano ulifanyika miaka miwili na miezi minne ya Uhuru wa Tanganyika uliopatikana tarehe 9 Desemba 1961 na miezi mitatu tu baada ya kufanyika Mapinduzi ya Zanzibar ya tarehe 12 Januari 1964 na Muungano ukafanyika tarehe 26 Aprili 1964.

View attachment 3579447

2. Utiaji saini wa hati ya makubaliano ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (22 Aprili 1964).

Tarehe 22 Aprili 1964, kwa niaba ya wananchi wote wa Tanganyika na Zanzibar Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Tanganyika Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Serikali wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume walisaini hati ya makubaliano ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Utiaji saini wa hati ya makubaliano ya Muungano ulifanyika katika Ikulu ya Zanzibar.

Wakati mkataba wa Muungano unasainiwa, Rais Nyerere aliambatana na Roland Brown (Mwanasheria Mkuu wa Serikali), P.R.N Fifoot (Mwandishi Mkuu wa Sheria), Oscar Kambona (Waziri wa Mambo ya Nje), Job Lusinde (Waziri wa Mambo ya Ndani) na Bhoke Munanka (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais).

Kwa upande wake, Rais Karume wa Zanzibar aliambatana na Abdulla Kassim Hanga (Makamu wa Rais wa Zanzibar), Abdulazizi Twala (Naibu Waziri Afisi ya Rais) na Ali Mwinyigogo (Msaidizi wa Rais Ikulu).

View attachment 3579457

3. Baraza la Mapinduzi na Bunge la Tanganyika Kuridhia Hati ya Makubaliano ya Muungano (25 Aprili 1964).

Tarehe 25 Aprili 1964 Hati ya Makubaliano ya Muungano iliridhiwa na mamlaka za kutunga sheria.

Baraza la Mapinduzi ambalo lilifanya kikao chake asubuhi ya siku hiyo ya tarehe 25 Aprili 1964 Ikulu, Zanzibar na Bunge la Tanganyika lilifanya kikao chake siku hiyo jioni katika ukumbi wa Bunge wa Karimjee, Dar es Salaam.

Wakati Zanzibar ikiridhia Hati ya Makubaliano ya Muungano, Mwalimu Nyerere alimtuma Oscar Kambona (Waziri wa Mambo ya Nje) kama mjumbe wake kwenda kushuhudia tukio hilo baada ya kupewa mwaliko kutoka kwa Rais Karume.

Vilevile, Rais Karume kupitia mwaliko aliopata kutoka kwa Mwalimu Nyerere alimtuma Salim Rashid (Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi), kwenda kushuhudia tukio la kuridhia Hati ya Makubaliano ya Muungano

Kwa mujibu wa sheria ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Sheria Na. 22 ya mwaka 1964, Sheria ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika ya mwaka 1964 pamoja na Hati ya Muungano ziliweka bayana kuwa, baada ya kuridhiwa kwa Hati ya Makubaliano ya Muungano, siku inayofuata ndiyo itatambuliwa rasmi kuwa ni siku ya Muungano.

Hivyo, tarehe 26 Aprili, 1964 ikawa ndio siku rasmi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

View attachment 3579449

4. Bunge la Jamhuri ya Muungano Kuanza Kazi (27 Aprili 1964).

Tarehe 27 Aprili 1964 ndiyo siku ambayo Bunge jipya la Jamhuri ya Muungano lilianza kazi.

Moja ya matukio makubwa katika tarehe hiyo ilikuwa ni kubadilishana Hati ya Makubaliano ya Muungano, tukio ambalo lilifanyika katika Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam wakati wa kikao cha Bunge cha jioni.

Pia, siku hiyo waliapishwa viongozi wa Jamhuri ya Muungano wakiongozwa na Sheikh Abeid Amani Karume.

View attachment 3579451

View attachment 3579458
View attachment 3579459

5. Kuundwa kwa Baraza la Mawaziri la Muungano (28 Aprili 1964).

Tarehe 28 Aprili 1964 Baraza Jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lenye Mawaziri 23 liliapishwa katika Ukumbi wa Karimjee, watano kati yao kutoka Zanzibar.

Kuapishwa kwa Baraza hilo ilikuwa ni kielelezo cha kwamba, Serikali ya Muungano imeanza kazi rasmi.

View attachment 3579460

6. Kutuma Taarifa Umoja wa Mataifa (UN).

Tarehe 30 Aprili 1964 Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ilimjulisha Katibu wa Umoja wa Mataifa, Bw. U Thant kuwa Nchi za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zimeungana na kuunda nchi moja inayoitwa "Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar".

Mwezi Oktoba, 1964 Bunge la Jamhuri ya Muungano lilabadili jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Sheria ya kubadili Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ya mwaka 1964.

Kufuatia mabadiliko hayo, tarehe 2 Novemba, 1964 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alifahamishwa kuhusu mabadiliko ya jina la nchi naye alikiri kujulishwa tarehe 18 Desemba, 1964.

View attachment 3579461

7. Kuchanganya kwa Udongo wa Tanganyika na Zanzibar (26 Aprili 1965).

Tarehe 26 Aprili 1965, lilifanyika tukio la kuchanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar lilifanyika katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kama alama ya kudhihirisha Muungano wa udugu wa kudumu.

Tukio hili lilikuwa ni sehemu ya shamrashamra za sherehe za kuadhimisha mwaka mmoja wa Muungano

Sehemu ya udongo huo ilitumika kupanda mti wa mwembe katika Viwanja vya Ikulu ya Dar es Salaam ambapo upo hadi sasa.

View attachment 3579462​

View attachment 3579463
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umeshapoteza sifa haufai kabisa .... ni bora Mamlaka kamili ya Tanganyika yetu yarudi. Huu muungano unafaidisha wanasiasa tu raia wengi wa Tanganyika hakuna kitu wananufaika nacho toka huko Visiwa vya Unguja na Pemba
 
Kila mtu atafute kazi kwao siyo sisi haturuhusiwi kufanya kazi kule wao wamejazana huku mpk Das, DC, na . ......
 
Back
Top Bottom