UNCLE THREE
Member
- Jul 20, 2021
- 25
- 88
MBINU ZA KUPAMBANA NA MABADILIKO YA HALI YA HEWA NA TABIA YA NCHI.
Mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya nchi ni tatizo linalokumba maendeleo ya katika nyanja zote kama inavyolipotiwa na vyombo mbalimbali vya habari ulimwenguni kote ambapo majanga ya vifo, ukame, njaa yamelipotiwa kutokana na ongezeko la joto duniani ambalo chanzo chake asilia ni shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi kama vile;- ukataji miti, ongezeko la viwanda pamoja na ongezeko la watu duniani.
Lakini, kama watu binafsi, katika ngazi ya familia na vijiji tunaweza kupunguza kwa kiasi ongezeko la joto duniani kwa kutekeleza hatua ndogondogo endelevu ndani ya jumuiya zetu pasipo kusubilia maagizo na utekelezaji wa jambo hili kutoka ngazi za juu za mamlaka ya kiutawala ambapo maagizo yamkini utekelezaji wake huweza kuchelewa
MBINU RAHISI ZINAZOWEZA KUTUMIWA ILI KUPAMBANA NA MABADILIKO YA HALI YA HEWA NA TABIA YA NCHI
1. Kupunguza idadi ya magari au vyombo vya usafiri vinavyotumia mafuta. Ikumbukwe kwamba kila lita moja ya mafuta huzalisha kiasi cha kilo 2.5 za hewa ya Cabondioxide. Inapowezekana vyombo vya usafiri vitumie nishati ya gesi asilia hata viwandani ili kupunguza ongezeko hewa ya Cabondioxide ambayo ndiyo chanzo kikuu cha kuongezeka kwa joto duniani pamona na uhalibifu wa Ozone layer.
2. Kupunguza matumizi ya nishati ya kuni na mkaa. Katika jamii nyingi za kitanzania na kiafrika kwa ujumla kuna kiwango kikubwa sana cha matumizi ya nishati ya kuni na mkaa ambayo hupelekea ukataji wa miti. Licha ya kuwa nchi yetu inazalisha gesi asilia na kuwa na unafuu wa upatikanaji wa majiko ya kutumia gesi asilia bado mwamko wa jamii zetu juu ya matumizi ya gesi asilia badala ya kuni na mkaa bado upo chini sana hasa maeneo ya vijijini.
3. Sela ya mtu na mti. Katika baadhi ya jamii hapa nchini kumekuwa na sela mbalimbali za kusaidia uhifadhi wa miti kama vile sela ya 'kata mti panda mti' lakini pia kuna sela ya 'Mtu na mti' ambayo inaweza kuwezesha ongezeko la upandaji miti hali itakayosaidia kupunguza ongezeko la hewa ya Cabondioxide katika anga. Sela hii ni mbinu nzuri ya kuigwa na jamii zote nchini na duniani kwa ujumla ili kupunguza tatizo la mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya nchi.
4. Kuchukua hatua dhidi ya upotevu wa misitu na kutenga maeneo ya kupanda miti walau hekali 10 za mraba kila kata. Serikali na mamlaka husika vinatakiwa kuchukia hatua stahiki juu ya suala ya upotevu wa misitu kama inavyorekodiwa duniani kote kwamba kuna tatizo la upotevu wa misitu unaosababishwa na hitaji kubwa la miti katika kuzalisha vitu mbalimbali hasa vifaa vya ujenzi kama vile mbao, miti na Sling bord. Hivyo serikali na mamlaka husika vinapaswa kuchukua hatua juu ya hili pamoja na kutenga eneo la hifadhi ya misitu walau kwa kila kata nchi nzima.
5. Kupunguza kasi ya kuzaliana. Idadi kubwa ya watu na ongezeko la watu duniani imeonekana kuwa changamoto na sababu mojawapo inayopelekea kuongezeka kwa joto duniani kutokana na kuongezeka kwa mahitaji makubwa na vifaa vya ujenzi pamoja na kukua na kupanuka kwa miji kunakopeleka misitu kuingiliwa na kutoweshwa ili kupisha maendeleo na miundombinu mingine kama vile makazi na shunguli za kilimo.
6. Kutunza na kuhifadhi misitu asilia. Nchini Tanzania kuna mapori na misitu asilia ambayo ndiyo mapafu ya nchi yanayosaidia upatikanaji wa hewa safi ya oxygen na inayofyonza na kupunguza hewa ya Cabondioxide katika anga. Serikali, mamlaka husika, vingozi wa ngazi ya juu hadi ngazi ya chini, familia na mtu binafsi wanalo jukumu la kutunza, kuhifahi na kuilinda misiti na mapori visivamiwe na wafugaji, wakulima na majangili wa misitu ili kuendeleza nchi yenye hali ya hewa rafiki kwa shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi.
Hitimisho.
Mifugo ni moja ya vichafuzi vikubwa vya anga na tunashauriwa kuongeza ulaji wa matunda na mboga kwa kiasi kikubwa na kupunguza ulaji wa nyama ili kupunguza Cabondioxide. Kula chakula ambacho ni cha ndani na cha msimu, epuka uagizaji wa bidhaa kutoka nje ambazo mbadala wake unapatikana ndani ya nchi maana kwa kufanya hivyo utapunguza uzalishaji zaidi wa hewa ya Cabondioxide kwa sababu ya usafirishaji na pia utakuwa mzalendo kwa kupenda bidhaa za nchi yako.

Upvote
6