Hatua ya kwanza ya kusimamia uchumi wako na mafanikio

Hatua ya kwanza ya kusimamia uchumi wako na mafanikio

Elisha Chuma

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
282
Reaction score
275
Watu wengi wanaishi bila kuwa na mipango,mambo yao wanapeleka mambo kwa kufuata mkumbo na bora liende hiyo ni hatari kubwa,mafanikio hayaji kama ajali yanatengenezwa na jitihada,umakini,ustahimilivu na imani,vivyo hivyo kwa upande wa mafanikio ya kiuchumi.

Sheria na kanuni zake ni zile zile lazima uwe na mpango wa vitu vyako binafsi na vitu vya nje kwa ajili ya kukuongoza na kutengeneza dira madhubuti,wengi huogopa kusimamia mipango yao hivyo huishia kutokuwa na mipango na kuiishia leo bila kuipanga kesho lakini wakiwa na matarajio ya kufanikiwa zaidi kesho yao.

Badili mtindo wako wa mawazo na matendo,tatizo kubwa la uchumi wako haliko kwenye matendo liko kwenye ufahamu,ukianza kubadilika huko hata uchumi wako pia utabadilika.

Leo tuko mwezi disemba haupangi chochote ila ikifika mwezi Januari malalamiko ni mengi kama vile ni mwezi wa kushtukiza kwenye mwaka,hii yote ni kwa sababu vitu vinafanyika pasina mipango vinajiendea vyenyewe tu.

Uchumi wako unasimamiwa na mipango na vingine vingi lakini ukiweza kusimamia mpango wako unakuwa umeanza safari ya kusimamia uchumi wako.nidhamu ya fedha,matumizi,utunzaji vyote hivi viko kwenye usimamizi wa mpango.ANZA LEO KUIJENGA KESHO YAKO.

Elisha Chuma
Mwalimu na Mshauri
 
asante sana . Ila siku hizi sikusikii redioni kulikoni mkuu?
Ni kweli mwaka huu nilipunguza kusikika redioni na semina,ili kutafuta kwa undani zaidi tatizo letu liko wapi na kwanini tunafeli sana kuliko kufanikiwa.

Panapo majaaliwa mwezi ujao,mwaka 2020 nitaanza tena kusikika tena.
 
Mambo kama haya yangeanza kufundishwa shule ya msingi huko..tungekuja kuwa na kizaz bora sana!
Bahati mbaya bado hatujaamka kiasi hicho ila naona tusiitegemee sana elimu ya darasani,tujifunze sisi tutengeneze jamii yetu mtaani zaidi hata hivyo baada ya shule ni mtaa na watu wengi wanafeli zaidi mtaani.
 
Bahati mbaya bado hatujaamka kiasi hicho ila naona tusiitegemee sana elimu ya darasani,tujifunze sisi tutengeneze jamii yetu mtaani zaidi hata hivyo baada ya shule ni mtaa na watu wengi wanafeli zaidi mtaani.

Sure...tuanze na ngazi ya familia .mwe i wish tuwe km wahindi jamani
 
Back
Top Bottom