mwanazuoni mgeni
JF-Expert Member
- Sep 11, 2016
- 1,944
- 1,726
Hi wana Jf,
Nimejaribu kuchunguza hasa hizo nchi zetu za Africa hususani (East Africa) limekuwa ni jambo la kawaida kukuta kijana ana miaka takribani 30 na bado anaishi kwa wazazi wake bila aibu anasubiri ugali wa shikamoo.
Hili jambo ukiliangalia kwa mapana utagundua linasababishwa na vitu Vingi..
Mfano mfumo wetu wa elimu nao unachangia kwa sababu elimu mtu anayopata mpaka chuo kikuu haimjengi muhusika katika kuwa na mawazo ya kujiajiri . Tatizo linakuja pale mtu kamaliza chuo alafu kakosa kazi ..utashangaa mtu anakaa nyumbani mpaka anaoa/kuolewa akiwa nyumbani.
Lakini upande wa pili hata kama mtu hajasoma pia bado utakuta anaishi nyumbani kwa wazazi akiwa na umri mkubwa..mi nadhani pia sisi wa Africa uvivu unatupeleka pabaya.
Tumezoea kukaa vijiweni muda mwingi tukijadili mambo yasiyo na msingi na tumekuwa watu wa kutojali muda kabisa... Wala hatuna ratiba ..
Yangu ni hayo tuu kama kuna mwingine mwenye mawazo tofauti na mimi anaweza akaongeza au kunipinga kwa hoja lakini...
Nawasilisha