Hatua ya kwanza ya mafanikio ni kuondoka nyumbani

Hatua ya kwanza ya mafanikio ni kuondoka nyumbani

kibongo bongo ni heri kutoka home ukaenda kujitafutia maisha hasa pale unapoona hali ya home hairuhusu na wewe ni mkubwa.
kwa wasio wabongo wakiona home mambo safi hakuna kuondoka ni kubanana hapohapo kurithi utajiri na mtoto akitaka kusepa wazazi wanamkataza wanamtengenezea mazingira ya kuwa mrithi wao...
shida ya huku kwetu unakuta familia ina watoto 8 au zaidi, mtoto wa kwanza kamaliza chuo kikuu mdogo wake wa mwisho hata chekechea hajaanza, so kuendelea kukaa home ni kubana tu nafasi kwanza unajishtukia mwenyewe.
Kabisa mkuu .thank u
 
Sasa wewe kama familia yenu mnakaa kwenye nyumba ya kupanga mpaka leo utakaeje hapo?acha kuwaonea wivu watoto wa wenzio Wazazi wao waliojipanga na kujenga nyumba ili kuwasitiri watoto wao mpaka pale watakapofanikiwa kimaisha,wewe mlaumu Baba yako wakati wenzie wanasoma yeye alijifanya mjanja kuwa chimbo na kuvuta bangi na kunywa mataputapu.
 
mtoa hoja upo sahihi kabisa familia nyingi wa kina mama ndio hawaamini kwa mtoto kutoka na kwenda jitafutia wanahisi kama anakwenda teseka.
wenzetu wazungu ukifikisha miaka 18 hata kama unaishi kwa wazazi unatakiwa kuchangia chakula nyumbani au kulipa kodi hapo kwa wazazi maana yake uanze kutafuta kazi.
vijana wa kiafrika anakaa kwa mzazi anakataa kufanya kazi za kusafisha barabara kufanya usafi maofisini kulea wazee amemaliza form 4 anakataa kuosha magari au hata kujitolea sehemu yoyote.

cha ajabu tukienda ulaya tunagombea kazi hizi hizi ambazo huku tunazikataa mwenye masters anaenda soma phd ulaya anasafisha vyoo vya public, analea wazee na walemavu, anasafisha mifugo ili apate pesa ya kujikimu na bado tulio africa tunamwomba omba wakati kazi afanyazo kule huku zipo ila tunadharau
 
Hi wana Jf,
Nimejaribu kuchunguza hasa hizo nchi zetu za Africa hususani (East Africa) limekuwa ni jambo la kawaida kukuta kijana ana miaka takribani 30 na bado anaishi kwa wazazi wake bila aibu anasubiri ugali wa shikamoo.
Hili jambo ukiliangalia kwa mapana utagundua linasababishwa na vitu Vingi..

Mfano mfumo wetu wa elimu nao unachangia kwa sababu elimu mtu anayopata mpaka chuo kikuu haimjengi muhusika katika kuwa na mawazo ya kujiajiri . Tatizo linakuja pale mtu kamaliza chuo alafu kakosa kazi ..utashangaa mtu anakaa nyumbani mpaka anaoa/kuolewa akiwa nyumbani.

Lakini upande wa pili hata kama mtu hajasoma pia bado utakuta anaishi nyumbani kwa wazazi akiwa na umri mkubwa..mi nadhani pia sisi wa Africa uvivu unatupeleka pabaya.

Tumezoea kukaa vijiweni muda mwingi tukijadili mambo yasiyo na msingi na tumekuwa watu wa kutojali muda kabisa... Wala hatuna ratiba ..

Yangu ni hayo tuu kama kuna mwingine mwenye mawazo tofauti na mimi anaweza akaongeza au kunipinga kwa hoja lakini...
Nawasilisha
[emoji121]
MKUU
WEKA PICHA YA UTHIBITISHO KWANZA!

VINGINEVYO HUU UZI NI WA KICHOCHEZI KABISA HUU!
 
Back
Top Bottom