Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] mkuu umeweza kukaza 6month Chaka .. Leo unataka urudishe Mpira kwa kipa ..acha hzo mkuu komaa mpaka kielewekeMada imenikuta nimeweka mgongo kwny godoro macho kwa dari, natafakari nawaza mbali.. npo mji wa watu takribani 6 months najitegemea kwa heka ya TAESA, kijana niliemaliza chuo mwaka jana na mtaa hausomi.. 26 ndio age yangu lakn natafakar sijui nirudishe mpira kwa kipa[emoji28]
I gree with you big bro...Napingana na wewe. Mimi nimekaa home mpaka naoa nikiwa na umri wa miaka 30+ Baada ya kuoa nikahama nyumbani nikahamia kwenye nyumba niliyojenga na ninayoishi mpaka leo. Sikuona kwa nini nitoe pesa kulipa kodi badala ya kuipeleka kwenye ujenzi wa nyumba yangu mwenyewe.
Tatizo la vijana wengi ni kuwa na mienendo ambayo inakua vigumu kuishi na wazazi (ulevi, umalaya, u-popo, n.k). Kama unaishi kistaarabu, unachangia pesa ya matumizi nyumbani, utapewa heshima zote na hakuna atakayetamani uondoke.
Kama nyumba ni ndogo nakubali, ni muhimu kuhama. Nachokataa ni kuhama simply because eti una 25 yearsI gree with you big bro...
Ila majority tunatokea familia za chini ambazo hata idadi ya vyumba n vyakubanana so age ikifika 25 tayari wanaanza kukufukuza mdogo mdogo ukajitegemee ...
Sahihi kabisaWell said, kujitenga na wazaz ni mbinu ya kuelekea mafanikio. Waswahili husema shida ni chanzo cha maarifa. Sasa akina sie tunaosubir ajira ndio tujitegemee tunachelewa saaana.
Nakubaliana na hili kwa 100% mifano iko mingi, mfano ukiangalia wachaga ukitembea kwenye hii karibu kila wilaya ya mkoa ni vigumu kukosa mchagaHi wana Jf,
Nimejaribu kuchunguza hasa hizo nchi zetu za Africa hususani (East Africa) limekuwa ni jambo la kawaida kukuta kijana ana miaka takribani 30 na bado anaishi kwa wazazi wake bila aibu anasubiri ugali wa shikamoo.
Hili jambo ukiliangalia kwa mapana utagundua linasababishwa na vitu Vingi..
Mfano mfumo wetu wa elimu nao unachangia kwa sababu elimu mtu anayopata mpaka chuo kikuu haimjengi muhusika katika kuwa na mawazo ya kujiajiri . Tatizo linakuja pale mtu kamaliza chuo alafu kakosa kazi ..utashangaa mtu anakaa nyumbani mpaka anaoa/kuolewa akiwa nyumbani.
Lakini upande wa pili hata kama mtu hajasoma pia bado utakuta anaishi nyumbani kwa wazazi akiwa na umri mkubwa..mi nadhani pia sisi wa Africa uvivu unatupeleka pabaya.
Tumezoea kukaa vijiweni muda mwingi tukijadili mambo yasiyo na msingi na tumekuwa watu wa kutojali muda kabisa... Wala hatuna ratiba ..
Yangu ni hayo tuu kama kuna mwingine mwenye mawazo tofauti na mimi anaweza akaongeza au kunipinga kwa hoja lakini...
Nawasilisha
Usiondoke wizo hujawaomba wakuzae bien starehe zao hizo sawa? 😹
Eeeeh kabisaaa 😂😂😂 haondoki mtu hapa, wao ndio waondoke waniachie mji 😋😋😋Usiondoke wizo hujawaomba wakuzae bien starehe zao hizo sawa? 😹