Hatua ya kwanza ya makubaliano kati ya UN, UKRAINE na URUSI inaiwezesha URUSI kuuza nafaka na mbolea bila vikwazo

Hatua ya kwanza ya makubaliano kati ya UN, UKRAINE na URUSI inaiwezesha URUSI kuuza nafaka na mbolea bila vikwazo

ryan riz

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
423
Reaction score
683
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema hatua muhimu ya kwanza imefikiwa katika juhudi za kuwezesha nafaka kusafirishwa kutoka Ukraine.

Guterres ameeleza kwamba hatua hiyo imefikiwa kwenye mazungumzo ya mjini Istanbul kati ya wajumbe wa Urusi na Ukraine. Wajumbe wa Umoja wa Mataifa na Uturuki pia walishiriki kwenye mazungumzo hayo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameelezea matumaini ya kupatikana makubaliano rasmi wiki ijayo.

Amesema kwa jumla pana makubaliano juu ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa kusafirisha mamilioni ya tani za nafaka kutoka Ukraine na kufikisha kwenye masoko ya kimataifa na pia kuiwezesha Urusi kuuza nje nafaka na mbolea. Vikwazo vya kimataifa dhidi ya Urusi vimeongeza bei ya mbolea, ambayo inasababisha kupanda kwa bei ya chakula.

USA UNO-Generalsekretär Antonio Guterres Ukraine

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres​

Naye waziri wa ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar aliyeshiriki kwenye mazungumzo hayo amefahamisha kuwa pande zote zimekubaliana juu ya udhibiti wa pamoja kwenye bandari na kwenye njia nyingine ili kuhakikisha usafirishaji salama.

Mpango huo uliopendekezwa na Umoja wa Mataifa utawezesha kusafirishwa shehena hizo za nafaka kupitia njia maalum, zitakazoepuka maeneo ya hatari.
 
Back
Top Bottom