Hatua ya msingi

TZ-1

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
4,321
Reaction score
7,501
Habari wajenz /mafundi na wajenz wenzangu , naomba ushurik wenu hapa

Nipo katika kujiandaa kuanza ujenzi na nataka nijenge kwanza hatua ya msingi kwanza kutokan na kipato changu naomba makadirio ya karibu kbsa katika kuanza msingi na kuumalza hasa katika vifaa kama:-

-MATOFALI
  • CEMENT
  • KOKOTO
-MCHANGA
- NONDO
-MALIPO YA FUNDI

KIWANJA KIPO ENEO TAMBARALE KWA 93% UDONGO NI KICHANGA ILA NATAKA NIFUNGE MKANDA KUTA ZA NJE ZA JENGO Na kuta/msingi zote ambazo hutoka Nje kuingia ndani ,

BEI ZA TOFAULI ZA MSINGI TSHS 1100/- @1 INCH 6
CEMENT 15000/-

KWA MSISITIZO Ushimen na Njuka II

Peace of floor plane [emoji116][emoji116] moderate jitahd pcha ionekane.





JE KWENYE MKANDA NILAZIMA KUSUKA NONDO 3 VIPI NIKILAZA NONDO 2[emoji4][emoji19]
 
1. Kuanzia msingi hadi lenta Tofali - 2,000
2. Kuanzia msingi hadi lenta Cement - 25
3. Mkanda wa msingi, jamvi na lenta kokoto fuso - 2
4. Kenye mkanda na lenta hakuna haja ya kusuka nondo, lakini unaweza ukaacha nafasi ya inch 1 na nusu hadi 2 kwa kulaza nondo pembeni na pembeni zitakazo shikiliwa na ringi ndogo za 5/6 milimita.
5. Mchanga wa ujenzi kutoka msingi hadi lenta fuso tripu - 3
6. Mengineyo weka - 300,000
7. Makadirio ya nondo ni 38 hadi kusimamisha nguzo (kenopi) au pillar.
8. Ufundi kwa ujumla wa mchakato huo "ingekua mimi nafikiri ningekadiria sio zaidi ya - 1,800,000.
 
Kwann mkuu unapatkn maeneo ya pwani au...?
 
Kwann mkuu unapatkn maeneo ya pwani au...?
Hapana chief, mimi nipo huku Kerende, Mugumu Serengeti ndani ndani......
Hayo makadirio nimefanya ili upate wepesi, kama kupigwa usinyooshwe sana mkuu...
 
Hapana chief, mimi nipo huku Kerende, Mugumu Serengeti ndani ndani......
Hayo makadirio nimefanya ili upate wepesi, kama kupigwa usinyooshwe sana mkuu...
Aksnt sana kwa overview yako
 
Haya ndio makadirio ya fundi wa awali aliyonipa


Asee huyu jamaa amenigopesha hadi nilitak kuach kuanz ujenz

Ushimen
 
Ebu jifanye kichaa kwanza, agiza tofali 1,000 ambazo kwa makadirio zinajengwa kwa mifuko walau 15 ya cement.
Agiza mchanga tripu 2 za fuso, kisha nunua kamba ya manila rola moja ya mita 300 na misumari ya inchi 4 kilo 5.
Kisha baada ya hapo mwambie msingi afanye setting kwa kutumia matofali ili kubapa skwea mita na nyuzi 90 za mjengo wako.
Jitahidi kukubakiana nae kwenye ufundi aweke takataka zake zoooote ili wewe ujue tu kwamba unapaswa kumlipa kiasi gani, hii itakuepusha kila wakati kupigiwa sim kwamba kimepungua hiki na kile.
Pia hakikisha unakuepo siku ya kuchimba msingi na wanapo anza kuset nyumba.
Pia jitahidi kuwepo wakati wa ujenzi wa msingi kabla hawaja gukia (matofali ya msingi) na kusawazisha muonekano wa ndani, maana huku juu unauwezo wa kuhesabu tofali zilizo jengewa.
Jiepushe na gharama za vifaa kama mbao, pleti za kukodi, kumwagilia jengo, kukodisha ngazi, kununua ndoo ili aweke yeye kwenye ufundi wake.
 
Saw mkuu
 
App ya JF ina shida mahala, picha hazifunguki
 
Hizo 3 zenyewe zimepunguzwa kutoka 4 ambayo ni standard katika ujenzi
 
Tofali 1000 sawa na 1.1mil
Mchanga 4.5qm 60000/-
Cement 15bags 300000/-
Nondo 10 200000/-
R6 6 50000/-
Binding wire 3kg 15000/-
Misumari 5k 15000/-
Mbao nenda kakodi ila makadirio sio chini ya 100000/-
Ufundi 400000/-
Toto 2.7mil
 
Tofali 1000 sawa na 1.1mil
Mchanga 4.5qm 60000/-
Cement 15bags 300000/-
Nondo 10 200000/-
R6 6 50000/-
Binding wire 3kg 15000/-
Misumari 5k 15000/-
Mbao nenda kakodi ila makadirio sio chini ya 100000/-
Ufundi 400000/-
Toto 2.7mil
Aksnt sana
 
Hivi kama eneo ni kichanga kuna ulazima wa chini kuanza na zege? Siwezi anza kwa kupanga tofali?
Na pia kwenye kufunga mkanda wa msingi wenye kozi 7 ambazo tatu ardhini 4 zimetokeza nje. Kuna umuhimu gani wa kuzungushia na nondo nikiamua piga mkanda wa bila nondo..kuna hatari gani naitengeneza?
 
Ni vyema kama utafung mkanda uweke nondo 3 ukuta wa nje ndan unawez wek mbili au moja ata usipg mkand ndan sio issue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…