Hatua ya Pili ya Mchakato wa Ajira ni Kuandaa Tangazo la Kazi

Joined
Nov 15, 2022
Posts
25
Reaction score
142
- Tangazo la kazi huandaliwa kwa kuzingatia sifa kwa mujibu wa Muundo wa kada husika uliowasilishwa na Mamlaka ya ajira husika.

- Tangazo pia huzingatia masharti ya jumla yanayotolewa na Sekretarieti ya Ajira ambayo yanatafsiri Sera, Sheria Kanuni na Miongozi mbalimbali inayohusu michakato ya ajira.

- Tangazo hutolewa katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira,tovuti ya taasisi husika inayotangaziwa nafasi, radio, runinga, magazeti na/ au mitandao ya kijamii.

- Tangazo husika hutangazwa kwa muda wa siku 14 ili kutoa nafasi ya wadau wengi zaidi kuweza kuliona na kuomba Ajira.
 
Hongera zenu mupo vizuri simamieni kazi zote kuketa usawa
 
Matangazo ya nafasi za kazi za serikali za mitaa nnaweka wapi sijawai kuona kwenye website yenu wala za halmashauri.
 
Nyie nao hamjielewi
Key questions tukiwauliza mnakwepa kujibu.
 
- Tangazo la kazi huandaliwa kwa kuzingatia sifa kwa mujibu wa Muundo wa kada husika uliowasilishwa na Mamlaka ya ajira husika.

- Tangazo pia huzingatia masharti ya jumla yanayotolewa na Sekretarieti ya Ajira ambayo yanatafsiri Sera, Sheria Kanuni na Miongozi mbalimbali inayohusu michakato ya ajira.

- Tangazo hutolewa katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira,tovuti ya taasisi husika inayotangaziwa nafasi, radio, runinga, magazeti na/ au mitandao ya kijamii.

- Tangazo husika hutangazwa kwa muda wa siku 14 ili kutoa nafasi ya wadau wengi zaidi kuweza kuliona na kuomba Ajira.
PSRS mjitahidi kutenda haki kwa vijana wa kitanganyika...mnawazibiaga fursa vijana wa kitanganyika kwa kuruhusu wazanzibari kuomba ajira katika ofisi ambazo si za kimuungano...mfano ofisi ya NAOT si ya kimuungano ila mliruhusu wazanzibari kuomba na mkaendesha usaili

Na pia mkumbuke mambo ya muungano yamepunguzwa sana sio tena yale 22....mfano bandari, mafuta & gesi
 
50/50 Yakhee awamu yetu
 
Sekretarieti ya Ajira

Habari za muda huu. Poleni kwa majukumu mazito muliyonayo. Niliona mumetangaza kuhusu nafasi ya kutoa maoni na mukaweka muda wa mwisho wa kupokea maoni, tarehe 15 Feb 2023.

2023-02-04 17.21.34.jpg

01.) JamiiForums hamkuitaja kama platform mojawapo ya kutolea maoni kuhusu kanuni za uendeshaji wa shughuli za Sekretarieti ya Ajira katika utumishi wa uma. Ni vyema mukaizingatia na kui-recognise JamiiForums kama sehemu sahihi ya kupata maoni ya wadau.

02.) Kuwa na interval elekezi kama ya kila baada ya miezi 2 au 3 kukusanya maoni na kuyafanyia kazi. Hili ni suala muhimu na linahitaji quick response kwa kuwa linagusa hali ya ajira ambayo ina direct impact katika sustainability ya uchumi wa nchi yetu.

03.) Musichoke kujibu hoja na mada za wadau mbalimbali japo wapo ambao wana comments vitu ambavyo havipendezi kwakuwa vinaharibu taswira ya taasisi yenu. Naomba muelewe kuwa watu tupo na tabia tofauti na wengine wapo desperate kutokana na kuumizwa sana na hali ya kukaa bila ajira na kuzingatia ya maisha wanayoishi. Hivyo tuboreshe professionalism kwani taasisi hii tunaitarajia mbali na kusimamia ajira bali iwe pia ni mwalimu wa professionalism and accountability hususani kwa waajiriwa wapya.

04.) Kuhusu suala la kuchelewa kuitwa watu kwa ajili ya written interview. Tunaomba muweke angalau ratiba maalumu ya kuwa waomba ajira wa expect baada ya miezi kadhaa basi watapewa taarifa ya lini wataanza kuitwa kwa ajili ya written interview. Hata kama itachukua muda, madhara si makubwa sana kwa kuwa muombaji wa ajira ana angalau hint ya lini ataitwa kufanya usaili. Kuna faida hapa: Msailiwa atakuwa na uwezo wa kujiandaa kifedha pamoja na maandalizi ya mtihani kwani mara nyingi muda hua ni mdogo sana (aghalabu usahili hua ni wiki moja toka siku ya tangazo la kuitwa interview).

05.) Kuhusu matokeo ya written interview. Hapa nawapongeza kwa kuwa muko fast sana kusahisha na kutoa matokeo. Japo kuna sintofahamu ya kuchelewa kwa matokeo ya MDAs na LGAs, lakini si kawaida yenu, hivyo hilo halinifanyi mimi kutotambua utendaji wenu unaopendeza katika uharaka wa usahihishaji na utoaji matokeo. Vile vile, nimefanya saili zenu makadirio ya marks zangu nilizojiekea kwenye written kutokana na kufanya mtihani hazikupishana sana na marks nilizokutana nazo kwenye PDF ya results, iwe nimefaulu ama nimefeli. Hivyo tunawaomba muendelee kutenda haki na kutimiza wajibu wenu. Hongereni kwenye hili.

06.) Kuhusu practical interview. Ningependa kutoa maoni kuhusu muda. Kuna practical interview moja ilijawa na lawama za kutozingatia muda. Yaani watu wanafika kwenye usahili ndani ya muda lakini maandalizi yenu yanachukua muda kiasi kwamba huenda ikawa sababu ya kufeli kwa wasahiliwa (Njaa, anxiety kuongezeka, kusahau au kuchanganya madesa, nk). Ila hilo halinifanyi kutowapongeza kwa kuwa na uwazi mkubwa kwenye practical interview.

07.) Kuhusu oral interview. Jitahidini kuendana na muda. Kama interview ni saa 1 asubuhi basi hakikisheni mahojiano yanaanza hata saa 3. Kuna wakati interview ni saa 1 lakini mpka saa 6 au 7 bado usahili haujaanza. Jua la Dodoma ni kali, wasahiliwa wanahamishwa hamishwa, wengine njaa zinawauma wanahofu wakila wataitwa hawajamaliza, yani inakua ni kama organisation ya utaratibu imevurugika kiasi. Kwenye hili naomba kuwe na utaratibu mzuri, au la waiteni watu saa 3 asubuhi kama munajua kuna mambo ya kuyaweka sawa ili hata ikifika saa 6 au 7 basi kusiwe na kukaa sanaa kusubiri mahojiano. Liekeni sawa na hili.

08.) Kuhusu placement. Naimani haki hutendeka huko. Naimani uwajibikaji upo huko. Naimani uzalendo nao haukosekani kwenu. Japo yakini na uhakika wa hilo anajua Mola alietuumba.
Ningependa kutoa maoni ya kwamba, kama ambavyo hua mnaanza kutoa majibu ya written na practical kwenye accounts za wasahiliwa basi na majibu ya oral pia yatoeni huko kwanza ndani ya muda mfupi. Hali hii imepelekea mpaka kuwe na mjadala ambao wa juu ya "Status" kubadilika badilika baada ya "Oral" kama ina-implication yoyote kwenye "placement" ama la.
Hivyo, napendekeza muweke matokeo ya placement ya kazi kwenye accounts za waliofanya oral interview ndani ya muda mfupi kama ilivyo written na oral (Ndani ya wiki moja, mbili, tatu au mwezi mmoja). Baada ya hapo mutatoa PDF kuujulisha uma kuwa haya ndiyo majina ya waliofaulu kupata kazi. Lakini ndani ya wiki 2 au 3 baada ya kufanya interview wasailiwa wajue kama walipata au waliokosa.
Hii kuna faida:
(a) Afya ya akili ya wasailiwa ni muhimu kwa kuwa ni binaadamu na wana hisia. Kuna wakati wasahiliwa wanakuwa na expectations kubwa, wanasubiri placement kwa miezi miwili au mitatu, matokeo yake hawajapita kupata kazi. Mara nyingi hua kuna maumivu makali sana na hata mtu kukata tamaa. Kuna hoja mdau mmoja aliibua kuhusu watu kujiua kama wapo au hawapo. Si hoja ndogo, mpka mdau alisema basi tufahamu kuwa hiyo hali hupitia baadhi ya watu. Na counseling juu ya hili ni muhimu sana kwa wasahiliwa; (b) Itapunguza idadi ya watu kuomba na kuhudhuria usahili. Hii itasaidia nyomi la washiliwa kupungua kama mtu ana uhakika baada ya kuona kwenye account yake kuwa yupo kwenye placement na hapo anasubiri PDF tu ili kuthibitisha na ili ajue ni lini haswa barua yake itakua tayari akachukue; (c) Itasaidia kuwapa nafasi wengine wapate nafasi ya kazi. Hii inamaana ya kwamba aliepata akaona kwenye account yake baada ya wiki au wiki mbili kuwa amepata ajira basi hatohudhuria nyengine hivyo atasave muda na pesa. Bali kama asipokua na taarifa ataenda sahili nyengine na nyengine pengine mpka kufika tena oral huku asiwe na ufahamu kuwa yumo kwene PDF ya placement na hapo alipo amefanya wengine wasipate nafasi ya kuitwa na yeye anaitwa mara ya pili au ya tatu ilhali ameshafaulu oral na taarifa hana; (d) Kuweka placement kwenye account ya msahiliwa ndani ya muda mfupi baada ya kufanya oral interview pia ni kusaidia watu wawe na ufanisi wa mambo mengine. Sometimes kuna kuwa na wenge na mawazo baada ya oral kama mtu kapita au la kufika hatua ufanisi hupungua kibinaadamu. Hivyo taasisi hii ifanye ubinaadamu kuzingatia na wengine kwani kusubiri sana PDF ya placement hua ni mfano wa adhabu kwa baadhi ya watu hususani wale ambao ni jobless ambao hawana hata pa kujishikiza; (e) Pia itasaidi wale ambao wameshapata notification ya kuwa wamefaulu oral interview kujiandaa vizuri kwa ajili ya kazi. Na pia itasaidi hata kama PDF itachelewa mtu yeye binafsi atakua ameshajua kuwa amefaulu oral na muda wowote atawekwa kwenye PDF hivyo atakuwa yupo on time pale PDF itakapo toka rasmi.

Summary ya maoni yangu hapo juu.

-Kwa kuwa hii Sekretarieti ya Ajira ni account yenu rasmi hapa JamiiForums , basi ni vyema mukaitambua na JamiiForums kwenye press release za taasisi kama sehemu ya kupokelea maoni ya wadau wa maendeleo na ajira nchini.

-Kuwe na interval elekezi ambayo ni rasmi juu ya ukusanyaji wa maoni. Isiwe tu mwaka hadi mwaka au randomly. Hapana, kuwe na muda maalumu wa makusanyo ramsi ya marekebisho ya kanuni za uendeshaji.

-Msichoke kujibu hoja na mada zinazoibuliwa na wadau hata kama nyengine ni negatives. Kila kazi na changamoto zake.

-kuwe na angalau ratiba maalumu kuwa, waomba ajira wa-expect baada ya miezi kadhaa basi watapewa taarifa ya lini wataanza kuitwa kwa ajili ya written interview. Huenda ikawa hivi: kutokana na mchakato wa ajira za nafasi hizi, baada ya miezi 2 tunatarajia kuwaita kwenye written interview waombaji wote waliofuzu kuitwa kwenye usahili wa kuandika.

-Pongezi juu ya utendaji wenu na uharaka wa usahihishaji wa mitihani.

-Pendekezo juu ya kuzingatia muda wa practical interview kuanza. Pia hongereni kwa uwazi katika hatua hii ya practical.

-Jitahidini kuendana na muda. Kama interview ni saa 1 asubuhi basi hakikisheni mahojiano yanaanza hata saa 3.

-Kuhusu placement. Matokeo yatolewe mapema kwenye accounts za wasahiliwa baada ya wiki, wiki mbili, tatu, au maximum mwezi mmoja.
Baada ya oral interview, matokeo yatolewe kwenye accounts za wasahiliwa ndani ya muda mfupi. PDF ya placement ifuate baadae kwa ajili ya kuuthibitishia uma juu ya mchakato wa ajira na uwazi wake, na kwa ajili ya kuwajulisha waliofaulu oral interviews zao ni lini waende kuchukua barua. Yaani PDF isiwe ndio taarifa ya kumjulisha msahiliwa kwa mara ya kwanza ya kwamba alifaulu oral interview aliyofanya. Hii ni kwasababu, huwa inachkua muda mrefu sana kwa PDF ya placement kutoka baada ya oral interview. Mapendekezo yapo hivi, matokeo ya placements yawekwe kwenye accounts za aliefaulu na aliwekwa kwenye data base, na yule aliefeli baada ya wiki moja au mbili, then PDF iwe released kwenye website yenu baada ya kukamilika kwa taratibu za kiserikali.

Kama kuna sehemu nimekosea basi ni ubinaadamu na naomba radhi. Na kama kuna sehemu nimepatia, basi shukrani zote anastahiki Mola, muumba mbingu na ardhi.

Naimani maoni haya yatazingatiwa, ahsanteni sana.
Sekretarieti ya Ajira JamiiForums Jamii Opportunities
 
Sekretarieti ya Ajira

Habari za muda huu. Poleni kwa majukumu mazito muliyonayo. Niliona mumetangaza kuhusu nafasi ya kutoa maoni na mukaweka muda wa mwisho wa kupokea maoni, tarehe 15 Feb 2023.

View attachment 2506153

Maoni mazuri sana Hakika,umegusa kila nyanja.Naimani
Sekretarieti ya Ajira watayapokea.
Umegusia suala placement hakika kusubiri placements muda mrefu kunaumiza sana.Akili inakuwa haijatulia kabisa.
 
- Tangazo la kazi huandaliwa kwa kuzingatia sifa kwa mujibu wa Muundo wa kada husika uliowasilishwa na Mamlaka ya ajira husika.

- Tangazo pia huzingatia masharti ya jumla yanayotolewa na Sekretarieti ya Ajira ambayo yanatafsiri Sera, Sheria Kanuni na Miongozi mbalimbali inayohusu michakato ya ajira.

- Tangazo hutolewa katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira,tovuti ya taasisi husika inayotangaziwa nafasi, radio, runinga, magazeti na/ au mitandao ya kijamii.

- Tangazo husika hutangazwa kwa muda wa siku 14 ili kutoa nafasi ya wadau wengi zaidi kuweza kuliona na kuomba Ajira.
Sekretarieti ya ajira ni Bora mungesema matokeo ya MDA na LGA yanatoka tarehe gani au mwezi gani kuliko kusubirisha hivi. Wengine bado tunatoka mbali kufata hzo sahili n Hadi Sasa hatujui hatima yetu
 
Back
Top Bottom