Hatua za dhati zichukuliwe kudhibiti ebola isiingie nchini

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363



Serikali imesema itaongeza udhibiti dhidi ya watu wanye virusi vya ugonjwa hatari wa ebola, ili wasiweze kupenya na kuingia nchini.

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid, baada ya kuulizwa na gazeti hili juzi kuhusu hatua zinazochukuliwa na serikali katika kuzuia ugonjwa huo usipenye nchini kufuatia Shirika la Afya Duniani (WHO) kutoa tahadhari kwa nchi za Afrika juu ya kusambaa kwake.

Waziri huyo alisema kuwa serikali inaendelea kuweka uangalizi kwenye maeneo ya mipakani kwa lengo la kuwabaini watu wenye ugonjwa huo wasiweze kuruhusiwa kuingia nchini.

Alisema mbali na kuweka uangalizi kwenye mipaka, pale watakapogundua mgonjwa watachukua taarifa zake alikotokea zikiwa ni njia za kuongeza udhibiti.

Alisisitiza kuwa jitihada za serikali zipo palepale ndiyo maana hata ugonjwa huo ulipoibukia nchini Uganda miaka iliyopita, uliweza kudhibitiwa usiingie nchini.

Kwa mujibu wa Dk. Rashid, ugonjwa huo unaotokana na maambukizi ya virusi utaweza kudhibitiwa kama ilivyokuwa kwa ule wa dengue ambao uliingia takribani miezi mitatu iliyopita na kusababisha vifo vya watu wanne.

Ugonjwa wa ebola ambao unaweza kuambukizwa kutoka kwa mgonjwa kwenda kwa mwingine kwa kugusana, hadi sasa umeshaua zaidi ya watu 400 katika baadhi ya nchi za Afrika Magharibi ikiwamo Guinea Bissau.

Kutokana na hali hiyo, WHO, limetoa tahadhari kwa nchi za Afrika hasa zilizojirani na nchi hiyo dhidi ya ugonjwa huo hasa baada ya wagonjwa wa ebola kukimbilia Siera Leone.

Ebola ni ugonjwa hatari kutokana na kutokuwa na tiba wala kinga na ni ugonjwa unaoua haraka.Hilo linatosha kuwa fundisho kwetu kwamba serikali na wananchi wenyewe wanatakiwa kuchukua hatua za tahadhari ili homa hiyo isiingie nchini.

Kama alivyosema Waziri Rashid, tahadhari inayotakiwa kuchukuliwa na mamlaka mbalimbali ni kudhibiti wageni wanaoingia nchini katika maeneo ya mipaka kwa kuwachunguza kuhakikisha kwamba hakuna aliyeambukizwa ebola.

Pamoja na hatua hizo, upo umuhimu kwa mamlaka mbalimbali kutoa elimu kwa wananchi kuhusu dalili za ugonjwa huo lengo likiwa ni kwenda hospitali na katika vituo vya afya ikiwa wataona dalili hizo.

Wataalam wanasema kwamba pamoja na kutokuwapo na tiba wala kinga dhidi ya ebola, kuna uwezekano wa muathirika kupona ikiwa atapata uangalizi na huduma bora kutoka kwa madaktari, wauguzi na watoa huduma wengine wa sekta ya afya.

Ebola huhesabiwa moja kati ya magonjwa ya mlipuko na wagonjwa wake hutengenishwa na wagonjwa wengine ili wasipate kuambukizwa. Wataalamu wa afya wanasema kuwa huambukizwa kwa kugusa damu ya mtu aliyeembukizwa ugonjwa huo.

Pale mtu anapopata ebola, dalili zake za kwanza ni kuonekana kama magonjwa mengine. Watu wanapata homa, kujisikia kuchoka, maumivu ya kichwa, maumivu ndani ya tumbo, maumivu katika viungo na maumivu ya kooni. Kwa dalili hizo, watu hufikiria kwamba wana magonjwa mengine kama vile malaria au homa ya matumbo.

Baada ya dalili hizo, mgonjwa huanza kutokwa damu kwa kiasi kikubwa sambamba na kupata mshituko huku shinikizo la damu likiwa chini. Pia mapigo ya moyo kwenda kwa kasi, na mzunguko wa damu kuwa hafifu mwilini.

Wataalamu wa afya wanasema hali hiyo husababisha viungo vya mwili kuuma sana na baadaye viungo vya mwili hunaacha kufanyakazi. Ugonjwa huo pia husababisha ukakamavu mwilini na humuacha muathirika kitandani na hata kama atafanikiwa kufika hospitalini, lakini wengi wao hupoteza maisha.

Huu ni ugonjwa hatari sana na usiotaka masihala. Hii ni changamoto kubwa kwa jamii nzima ya Tanzania kuchukua hatua zinazostahili ili kuudhibiti kuepusha uwezekano wa kutokea vifo.

Hatua ya kwanza ni serikali kupeleka wataalamu wa kutosha wa afya katika maeneo ya mipakani wakiwa na vifaa kwa ajili ya kuwafanyia uchunguzi wageni wanaoingia nchini.

Hatunabudi kukumbuka kwamba ugonjwa unapoingia katika nchi jirani, kuna uwezekano mkubwa kuingia nchini kwa urahisi ikiwa hatua madhubuti hazitachukuliwa.

Ni matarajio yetu kwamba serikali imekusudia kuchukua hatua madhubuti za kudhibiti ebola isiingie nchini kutokana na kauli hii ya Waziri Dk. Rashid.

CHANZO: NIPASHE


 

Attachments

  • Ebola virus.jpg
    31.9 KB · Views: 156
  • ebola-outbreak-africa-2.jpg
    13.2 KB · Views: 156
Fahamu ugonjwa hatari wa Ebola:



Mgonjwa wa Ebola akipata huduma

Dk. Leopard Mwinuka

Ebola ni ugonjwa wa hatari unaosababishwa na virusi vijulikanavyo kwa lugha ya kitaalamu Ebola Virus .
Ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa yajulikanayo kitaalamu kama ‘homa za virusi’ na husambazwa na damu kutoka kwa mtu mwenye virusi hivyo kwenda kwa ambaye hana ugonjwa baada ya kutokwa na damu yule aliyeathirika.
Kwa kitaalamu hali hiyo ya maambuziki huitwa Viral Haemorrhagic Fevers na chanzo kamili cha virusi vya ugonjwa huu hakijulikani kama ilivyo hali inayosababisha mlipuko wake pia haijulikani. Maradhi haya hayana tiba tiba wala chanjo.

DALILI
Dalili za ugonjwa huu zipo nyingi lakini muhimu ni hizi, kwamba mgonjwa anakuwa na homa kali, inayoambatana na kutokwa damu katika matundu yote ya mwili kama vile puani, njia ya haja kubwa na ndogo, masikioni, mdomoni, machoni au anaweza kupasuka ngozi n.k.
Dalili nyingine ni kutapika damu, kuharisha damu, fizi kuvuja damu, kutokwa na damu na kuvia chini ya ngozi au kutokwa na damu sehemu za haja kubwa na ndogo, choo na mkojo pia vitaonekana kuwa na damu. Ugonjwa huu huweza kuenea kwa jamii kirahisi na haraka sana kutoka mtu mmoja hadi mtu mwingine kupitia njia mbalimbali kama vile kugusana, kwa njia ya mate, damu, mkojo, machozi, kamasi au kwa njia ya majimaji mengine ya mwili,ikiwa ni pamoja na jasho. Mtu anaweza kupatwa maambukizi kwa kumgusa mtu aliyekufa kwa ugojnwa wa Ebola au kuchomwa sindano ambayo mwenye maradhi haya amechomwa nayo na vile vile huambukiza kwa njia ya kujamiiana.
Lakini vifaa ambavyo ametumia mtu mwenye maradhi haya vikitumiwa , mtumiaji anaweza kupatwa na ugonjwa huu.

KINGA
Ugonjwa wa Ebola unaweza kuzuilika kwa kuepuka kugusa au kuingiwa na mate, damu, mkojo, jasho, machozi na majimaji mengine yanayotoka katika mwili wa aliyeathirika au mtu mwenye dalili za ugonjwa huu wa Ebola.
Ili kujikinga ni vema wananchi wakatoa taarifa mapema kwa viongozi hasa wa afya mara tu waonapo mtu mwenye dalili za ugonjwa huu. Wakati huo huo ni vyema kumuwahisha hospitali mgonjwa mwenye dalili tulizozitaja hapo juu.
Wananchi waepuke kuishughulikia maiti ya mtu aliyefariki kwa ugonjwa au dalili za ugonjwa wa Ebola na badala yake waiarifu serikali ambayo itatoa wataalamu wenye vifaa maalum wa kuzika na kuipima maiti ili kujua kama aliambukizwa maradhi hayo au la.
 

Attachments

  • ebolavirusreuters670.jpg
    28.5 KB · Views: 115
Muuguzi akimuhudumia mgonjwa mwenye virusi vya Ebola. WHO/Chris Black

Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema kuwa kufikia Juni 30, idadi ya vifo vilivyotokana na mkurupuko wa ugonjwa wa Ebola imepanda na kufikia watu 467, huku visa vya maambukizi ya virusi hivyo hatari katika nchi tatu zilizoathiriwa za Guinea, Liberia na Sierra Leone vikiwa sasa vimetimu 759.

Idadi kubwa zaidi ya vifo hivyo imetokea nchini Guinea, ambako watu 303 wamefariki dunia, huku Liberia ikishuhudia vifo 65 na vifo 99 kutokea Sierra Leone.

Kwa mujibu wa WHO, sababu tatu kubwa zinazochangia kuongezeka maambukizi katika ukanda huo utamaduni na imani za kijadi vijijini, idadi ya watu wengi katika maeneo yaliyo nje ya miji ya

Conakry na Monrovia, pamoja na shughuli za kibiashara na kijamii zinazoendelea kwenye mipaka ya nchi hizo na watu kuvuka mipaka.

WHO imesema kudhibiti mkurupuko huo kunahitaji hatua thabiti katika nchi hizo, hususan kwenye maeneo ya mipaka. Kama njia moja ya kuitikia tatizo hilo, WHO inaandaa mkutano wa ngazi ya juu

kwa ukanda huo kuanzia Julai 2-3 mjini Accra, Ghana, ili kutathmini hali, kutambua upungufu, kuunda mpango wa kuudhibiti ugonjwa huo, pamoja na kuongeza utashi wa kisiasa na ushirikiano mipakani baina ya serikali za ukanda huo. chanzo.Vifo kutokana na Ebola vyaongezeka hadi 467 | Idhaa ya Redio ya UM

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…