Hatua za haraka zichukuliwe kuinusuru nchi na mfumuko mkubwa wa bei kwa vifaa vya ujenzi

Hatua za haraka zichukuliwe kuinusuru nchi na mfumuko mkubwa wa bei kwa vifaa vya ujenzi

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
25,937
Reaction score
41,161
Salaam!

Baada tu ya sintofahamu ya Oct 29, pametokea mfumuko mkubwa wa bei za bidhaa mbalimbali Katika sekta mbalimbali, Leo nitaongelea sekta ya ujenzi.

Bei ya kigae Cha size (40"*40") January 2025 ilikuwa tshs 23,000 kwa boksi moja lenye 12 PCs,

January 2026, kigae hicho hicho Cha size (40"*40") kinauzwa madukani kwa bei ya tshs 43,000.

Ongezeko hili la bei kutoka 23,000 Hadi 43,000 ni shilling 20,000, sawa na 86%.
Hili halikubaliki.

USHAURI

Kwa kuwa October 29 hapakufanyika uchaguzi, bali mauaji ya halaiki, nashauri tufanye uchaguzi wa haki Kisha tupate viongozi halali kwa ngazi zote, na inflation hii kubwa itakoma ghafla.

Mungu ibariki nchi YANGU nzuri niipendayo Tanzania 🇹🇿

Nawasilisha 🙏
 
Mwananchi huko kijijini kama alitunza sh 230,000 tangu January 2025 akitegemea atapata box kumi za vigae vya size ya 40*40, kwa bei ya 23,000 kwa box moja lenye 12pcs,

Akienda saizi dukani, ataambulia box Tano pekee.

Maana bei ya sasa Ina ongezeko la TSH 20, OOO kwa box, yaani 43,000 kwa box moja.

Hii ni hatari kubwa.
 
Au ndo tuseme wachangiaji wa mabilioni ya uchaguzi fake wanajilipa KUPITIA kupandisha bei hizi?
 
Nataka vita itokee
SI vyema kuchoma nyumba watoto wakiwa ndani eti kwa sababu. umemwona nyoka akiingia ndani ukiwa nje,

Busara hapa ni kutoa vitu na watu ndani,

Nyoka mkamate, muue,

Habari itaishia hapo,

Ila clkuchoma nyumba SI sahihi, maana nyoka aweza chimba shimo akazamia humo asiungue moto,wwe ukapata hasara kubwa.

Tutumie akili kubwa sana.

Umeelewa?
 
Ongezeko hili la bei kutoka 23,000 Hadi 43,000 ni shilling 20,000, sawa na 86%.
Hili halikubaliki.
Vitu vingi sana vimeongezeka bei ila kuna maeneo bei ipo vilevile tembea tembea utafika sehemu wanauza 23,000 sema ni mbali na hapo unaponunua 43,000... sasa hivi kila mfanyabiashara anajipangia tu bei anavyojisikia
 
Vitu vingi sana vimeongezeka bei ila kuna maeneo bei ipo vilevile tembea tembea utafika sehemu wanauza 23,000... sasa hivi kila mfanyabiashara anajipangia tu bei anavyojisikia
Wapi huko ndugu?

Mimi naongelea bei ya mwisho wa nchi.

Yaani bei ya dar to sirari au Musoma .

Inflation ni kubwa mno.
 
Acha unyumbu
Tuelezee kinagaubaga mahusiano kati ya kurudiwa uchaguzi na mfumuko wa bei?
 
Jeshi letu Lina wajibu wa kulinda usalama wa raia na mali zao,

Lisinyamazie hatari hii.
 
Acha unyumbu
Tuelezee kinagaubaga mahusiano kati ya kurudiwa uchaguzi na mfumuko wa bei?
Ni rahisi sana.

1. Uchaguzi haurudiwi, sababu Uliyeyuka,haukufanyika, yalifanyika mauaji ya raia. Sasa unatakkiwa ufanyike.

2. Waliochagia kukusanya pesa za uchaguzi fake Uliyeyuka ni wafanyabiashara, ndio walioruhusiwa kupandisha vitu bei Ili kurudisha pesa walizohonga watawala fake.

HITIMISHO.

Nadhani umeona sasa mhusiano ya inflation na viongozi haramu waliopo.
 
Back
Top Bottom