Hatua za kikanuni za Bunge zitakazochukuliwa dhidi ya Luhaga Mpina ziambatane na hatua muafaka za kikatiba za CCM kumng'atua

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388

Ni wakati muafaka sasa kwa CCM kufanya wajibu wake muhimu sana, dhidi ya wenye kiburi, waongo, wabishi na wenye tamaa waliobakiza mioyo yao ccm, lakini akili zao zikiwa kwa walio watuma.

Wakati kamati ya maadili ya bunge ikiendelea na majadiliano, kufanya uchambuzi wa kina na kujiridhisha mbivu na mbichi juu ya nyaraka na vielelezo alivyo wasilisha Mh. Luhaga Mpina kwa spika, dhidi ya tuhuma anazomtuhumu waziri wa kilimo, mwenye bidii sana, mchapakazi hodari waziri Mh. Hussein Bashe.

CCM ijiandae kumchukilia Mh. Luhaga Mpina hatua stahiki za kinidhamu dhidi ya kumdharau spika, kulidharau bunge, kumzushia Mh. waziri waziri Bashe kinachofanyiwa kazi na kamati ya bunge, na kuituhumu bila hakika serikali yote sikivu ya CCM kwa ujumla.

Hii si sawa kwa taasisi imara na makini kama CCM, kuendelea kuwavumilia wanachama wake wasio zingatia misingi ya nidhamu, kanuni na katiba ya chama na kukengeuka kwa chuki isiyo na sababu.

Na baada ya kumchukilia hatua za kawaida za kinidhamu kwa mujibu wa katiba ya CCM, iwe pia ni wakati muafaka chama kiende mbali zaidi, kwa kumvua uanachama wa CCM Mh. Luhaga Mpina kwa kukiuka na kwenda kinyume na kanuni, taratibu, mila, desturi na utamaduni wa CCM, wa kufanya kazi kwa kuheshimiana na kwa umoja ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Mh Luhaga Mpina abanduliwe CCM haraka iwezekanavyo kwa kutatiza mara kwa mara kupinga, na kijaribu kidhoofisha na kwa kupotosha kwa makusudi nia, mipango mikakati na malengo ya chama na serikali sikivu ya ccm katika kuwaletea wananchi maendeleo, na kuchochea mageuzi ya kisiasa, kijamii na kiuchumi kwenye maisha ya waTanzania wote.

Mh. Luhaga Mpina apokonywe uanachama wa CCM, ili akapate fursa na wasaa mzuri zaidi wa kuendeleza tuhuma zake na gubu binafsi alizonazo, dhidi ya baadhi ya waandamizi serikalini, ambao anahisi ndio waliosababisha na kuchochea, yeye Mh. Luhaga Mpina kutoswa kwanye baraza la mawaziri alilokua akihuduma kama waziri wa uvuvi, hapo awali.

Mh. Luhaga Mpina avuliwe uanachama ili kwa uhuru zaidi, akaungane na wenzie wa upande wa pili, wanaomtetea na waliopoteza uelekeo, walio kosa hoja, sera na wasiojua hata wana dai nini wala wanatetea nini, yaani wapo wapo tu.

Ni matumaini yangu, mpaka sasa kwa hali ilipofikia, pasina shaka yoyote, kupitia vyombo maalumu vya chama, CCM itakua imejiridhisha pasina shaka yoyote kwamba Mh. Luhaga Mpina kwa kiburi, jeuri na utovu wa nidhamu hana sifa wala vigezo tena vya kua mwananchama, mkereketwa wala shabiki wa CCM na anastahili kufubgashiwa virago vyake CCM.

- Spika Tulia amburuza Luhanga Mpina Kamati ya maadili
 
Kwani ccm huwa inafuata kanuni!? Ushahidi wa ripoti ya cag kama chama kimechukua hatua gani!?
FBora mpina kuliko spika!
jukumu na wajibu wao kuona ni kipi muafaka cha kufanya na hatua gani za kuchukua dhidi ya anae onyesha kiburi, jeuri na utovu wa kimaadili kulingana na sheria, kanuni, taratibu, mila desturi, utamaduni na ustaarabu miongni mwa viongozi na wanachama cha Mapinduzi πŸ’

ni rahisi na iko wazi..
lakini pia ni jambo zuri zaidi kwa Mh.Mpina, baada ya kubanduliwa CCM, aende kuungana na wenzie anao imba nao verses na choruses zenye tone na midundo inayofanana kwa uhuru zaidi....πŸ’

au comrade,
unajisahaulisha kwamba "Birds of the same feather flock together "🐦
 
Tangu lini CCM imesimama na wananchi dhidi ya mafisadi na majizi yanayoiangamiza nchi yetu

Ile ripoti ya CAG iliyosubiri bunge la mwezi wa tisa mwaka jana, nani aliwajibishwa na serikali ya ccm licha kwamba CAG alibainisha wizi mkubwa katika ripoti yake?

Hivi nyinyi maccm ni lini mmeanza kuwakubali wakweli na kuwapa kipaombele katika kulijenga taifa?

Hivi juzi tu tunaambiwa Warabu wa bandari zetu wametoa gawio kubwa zaidi kuwahi kutokea ilihali tumekuwa na gawio la zaidi bilion 600 dhidi ya hizo bilioni 2.5?

Akili zenu huwa zinawaza kuiba tu
 
Mpina kwenda chadema ni biashara ya CCM kupeleka mapandikizi! biashara za Mbowe hizi.
binafs sifahamu,
but nadhani kwa aina ya siasa anazofanya, ni dhahiri tayari ameshajihakikishia destination ya platform miongni mwa vyama vya siasa nchini,

na anafahamu fika kwamba, hawezi kuachwa kuendeleza jeuri na kiburi yake ndani ya CCM, na hawezi tena kuishi ndani ya CCM kwa style ya siasa anazofanya...

anaelekea wapi ni suala la muda tu,

but politically speaking,
sioni akikimaliza kipindi cha bunge kilichosalia, kakiwa mbunge wa CCM na haitawezekana tena kua mbunge wa Upinzani πŸ’
 
Ni sahihi kwa watu wote wema kukikimbia hicho chama chenu cha mauwaji na majizi
 
Wachunguze kifo cha Hayati Rais John Pombe Magufuli-kwa hiyo hiyo katiba/ kanuni za Kichama za CCM. ama?

Mpaka kieleweke. 2025

Chagua kwa Umakini 2025

Magulification must go on.
nadhani lilio halisi, bayana na dhahiri mchana kwepeee mbele ya CCM na umma waTanzania kwa sasa ni muafaka zaidi kufanyiwa kazi na kuchukuliwa hatua kuliko jambo jingine lolote ndani ya CCM πŸ’
 
Ni sahihi kwa watu wote wema kukikimbia hicho chama chenu cha mauwaji na majizi
kwamba ukitoswa kwenye baraza la mawaziri, unakasirika na kuanza kuhisi ati fulani ndie amekuchomea ukatoswa, na sasa unajenga chuki binafsi na gubu dhidi yake kwa kubuni tuhuma za uzushi na uongo eti nae aachishwe kazi, kama yeye mchoma nyavu za wavivu wadogo wanyonge, na mpima ukubwa wa samaki tena waliorostiwa kwa rula 🀣

eti huyu ndie mtu mwema anaekimbia CMC, right?
mtu mwema aliangamiza mamilioni ya vifaranga vya kuku aise dah 🀣
 
Kutetea waovu inahitajika kuwa mjinga kupita hali ya ujinga

Kwamba utetezi wa Mpina ni uwongo kwa mjibu wenu wajinga?

Yaani kampuni yenye mtaji wa m50 ipewe tenda ya kuleta sukari yenye thamani ya b 600?

Maccm mmelogwa na nani?
 
Bunge la CCM
na hata lijalo baada ya uchaguzi mkuu 2025 litasheheni wabunge makini, hodari na madhubuti sana wa CCM ili kuishauri serikali, kujisimamia serikali, kutunga sheria, sera na mipango mbalimbali ya maendeleo, kujadili na kupitisha bajeti za mawizara na bajeti kuu ya serikali...

kwani wanainchi wakiamua, kuna nini iko mbaya hapo gentleman πŸ’
 
Wenye akili wakifanya mkutano, wewe hutahudhuria..!!
 
Pumbavu sana wewe dog
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…