Zakaria Maseke
Member
- Apr 26, 2022
- 90
- 150
Elimu ya sheria: Kuhusu
namna ya kufanya biashara yako iwe rasmi na inayoaminika kwa kufuata taratibu za kisheria.
Kama unataka biashara yako iwe rasmi na ilindwe kisheria nchini Tanzania, fuata hatua hizi:
1: Chagua wazo la biashara. Tambua unataka kuuza nini au kutoa huduma gani.
2: Chagua aina au muundo au mfumo wa biashara unaotaka, mfano kampuni (company), ubia (partnership) au biashara ya mtu mmoja (sole proprietor).
3: Chagua jina la biashara au kampuni. (Hakikisha jina halijatumika na mtu mwingine).
Kujua kama jina la biashara halijatumika Tanzania, unafanya kitu kinachoitwa name search / name clearance kupitia mfumo wa BRELA.
4. Sajili biashara yako BRELA ili biashara yako itambulike kisheria.
5: Pata TIN, leseni na vibali maalum
-TIN (namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN) kutoka TRA.
-Leseni ya biashara kutoka manispaa au BRELA kulingana na aina ya biashara na eneo unalofanyia biashara.
-Vibali maalum kulingana na sekta husika. Baadhi ya biashara zinahitaji vibali vya ziada kutoka taasisi kama TMDA, TBS, OSHA, NEMC, LATRA, n.k., kutegemeana na sekta husika.
6: Zingatia sheria za kodi. Wasilisha marejesho ya kodi kwa wakati na ulipie kodi zinazostahili kwa mujibu wa sheria.
7: Linda biashara yako. Andaa mikataba mizuri na wateja, wasambazaji na wafanyakazi. Sajili alama ya biashara (trademark) ili kulinda jina na chapa yako.
Kwa nini ni muhimu kufanya biashara yako iwe rasmi?
• Huongeza uaminifu kwa wateja na taasisi za fedha.
• Hukuwezesha kupata zabuni, mikopo na wawekezaji.
• Hukuruhusu kuingia mikataba rasmi na mikubwa.
• Huiwezesha biashara yako kukua bila vikwazo vya kisheria.
------Mwisho-----
Mwandishi: Zechariah Wakili Msomi
(0612275246 📞 ).
(0754575246)