SoC02 Hatua za kufuata ili kupunguza au kumaliza matatizo ya Ndoa katika jamii zetu

SoC02 Hatua za kufuata ili kupunguza au kumaliza matatizo ya Ndoa katika jamii zetu

Stories of Change - 2022 Competition

DANIEL NOAH

New Member
Joined
Aug 12, 2022
Posts
2
Reaction score
0
Ndoa ni muunganiko wa mtu jinsia ya kiume na mtu mwingine jinsia ya kike na kwa muunganiko wao husababisha pia familia zao kuungana na kuwa na mahusiano baina yao.Kwa miaka ya hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la ukatili katika ndoa nyingi kwenye jamii zetu za kitanzania ambao husababishwa na misingi mibovu ya ndoa tangu kuanza kwake.Kila jambo hutegemea msingi wake ulikuwaje na umeanzaje tangu hapo kwanza,vile vile nayo ndoa inahitaji mwanzo wake uwe sahihi na imara ili kuondosha au kupunguza ukatili katika jamii zetu.

Migogoro ya ndoa hutokea pale wanandoa wanaposhindwa kuelewana kwa kiasi cha upendo kati yao kutoweka kabisa na kupelekea kuachana au hata kufikia mahali mmoja kati yao kuondosha uhai wa mwenzake,uhai wake mwenyewe au wote kwa pamoja.

Kwa wale wanao amini katika dini ya kikristo kuna mahali katika kitabu cha waebrania inasisitiza heshima iwepo katika ndoa,naomba kunukuu “Waebrania 13:4 Ndoa na iheshimiwe na watu wote“.Kuheshimu ndoa ni jukumu la wana ndoa wenyewe lakini pia na watu wote ni lazima waheshimu ndoa ya mtu na kuwaacha wahusika kujenga nyumba yao wenyewe bila kuingiza maneno yatakayo wagombanisha wahusika.
HATUA ZINAZOPASWA KUFUATA ILI KUMALIZA MIGOGORO YA NDOA KWENYE JAMII ZETU.
Katika kuwa na misingi bora ya ndoa kuna hatua nne au pengine Zaidi ambazo kijana wa kike au wa kiume kabla hajaamua kuingia katika ndoa azifuate kwa umakini akijua kwamba akikosea kufanya maamuzi ya kweli katika hatua mojawapo itamplekea kuwa na majuto katika ndoa yake ya baadae.
  1. URAFIKI
Kijana anapotaka kuingia katika ndoa ni lazima kwanza kabla ya yote awe na urafiki na huyo anayemtazamia hapo baadae,endapo kijana wa kike au wa kiume akifanikiwa kumfanya huyo mwenzake kuwa rafiki yake kabisa itamsaidia kwa asilimia mia moja kufahamu kwa undani kuhusu mwenzake.

Baada ya kumfahamu mhusika itakua rahisi sana kwa kijana kufanya maamuzi sahihi akiwa katika hatua hii ya mwanzo.Urafiki unaweza ukavunjika au ukaendelea mbele katika hatua inayofuata kutegemeana na alichokiona au alichojifunza kwa mwenzake kama ataweza kuendana nayo na kubebana nayo katika maisha yake yote ya hapa duniani.

Endapo kijana wa kike au wa kiume akiona tabia au hali yeyote kwa mwenzake ambayo anahisi itakuwa vigumu kwake kuvumilia ikiwa mhusika atashindwa kubadilika ni vuziri wakaishia katika hatua hii ya urafiki na asikubali kuingia na mtu huyo katika mahusiano.
Mfano kuna mtu ana roho ya ubinafsi na wala haonekani kama kuna uwezekano wa kubadilika ni vyema ukabaki naye katika urafiki.

2. UHUSIANO/MAHUSIANO.
Baada ya kuwa marafiki ni wazi kwamba kijana wa kike au wa kiume amekwisha pata uwezo wa kufanya maamuzi sahihi baada ya kufahamu tabia,mwenendo na maisha ya mhusika hata kama ni kwa kiasi kidogo lakini itampa nafasi ya kufanya maamuzi ambayo ina asilimia kubwa ya kuwa na matokeo chanya.

Ikiwa kijana wa kike au wa kiume ameamua kwa moyo wake wote bila vishawishi kutoka kwa mtu yeyote yule na akamkubali mwenzake jinsi alivyo basi wanaweza kuingia katika hatua hii ya mahusiano.

Katika hatua hii kila mmoja anaweza kuwa wazi kwa asilimia kidogo juu ya malengo yake ili kumpa kila mmoja nafasi ya kuona kama wanaweza kusaidiana katika kutimiza malengo ya kila mmoja wao na malengo yao ya jumla kama wataweza kuwa pamoja.
Nimesema watakuwa wazi kwa kiasi kidogo kwa sababu bado katika hatua hii wanaweza kushindwana na wakaachana na mara nyingi mtu akiwa wazi sana katika hatua hii ikitokea wameachana katika hali ya ugomvi kwa walio wengi hujutia sana na wakati mwingine hulazimika tu kwenda hivyo hivyo hata kama ameona mhusika siyo sahihi ili tu kuficha yale maumivu lakini pia na ile hofu kwamba huyu mtu ananijua sana.

Mfano:
kijana wa kiume malengo yake ni kuwa mfanyabiashara mkubwa baadae lakini kabla hajafika huko kazi yake kwa sasa ni machinga akitegemea kufika kule anakotaka,lakini kijana wa kike aliyekutana naye yeye anataka mtu ambaye tayari amekwisha fanikiwa hataki mtu mwenye maono anataka kuona sasa.

Kwa kifupi mtu mwenye tamaa asiyetaka kuvumilia na kufanya kazi kwa bidi ni ngumu kuwa naye.

Hata kama ikitokea wakawa pamoja unaweza kabisa kutabiri mwisho wao.Ni vyema kijana wa kike na wa kiume kujuana kwa undani katika hatua hii kabla ya kwenda katika hatua nyingine.

3. UCHUMBA
Katika hatua hii kijana wa kike au wa kiume anaweza sasa kufanya maamuzi ya kumtambulisha mwenzake kwa wazazi,ndugu au hata rafiki kwani kuna asilimia kubwa ya watu hao kufikia hatua ya mwisho ya kuishi pamoja.Kama kweli kijana husika alikuwa makini katika hatua mbili za mwanzo basi katika hatua hii tunampa asilimia tisini (90%) za kufikia mwisho mzuri.

Katika hatua hii kila mmoja kati ya kijana wa kike na kijana wa kiume wanapaswa kuwa na mtazamo wa pamoja kwani hatua hii inawapelekea wao kuhusisha familia za pande zote mbili na kwa kawaida siyo sifa njema kuhusisha familia katika vitu ambavyo hata nyie wenyewe kama vijana husika hamuelewi mnachokifanya.

4. MAISHA YA NDOA
Baada ya kijana wa kike au wa kiume kupitia hatua zote tatu na mwenzake mtarajiwa kama mume au mke na wakafanikiwa kufika hatua hii ya mwisho,watakuwa na nafasi kubwa ya kuishi pamoja kwa furaha na amani katika ndoa yao.
Hii haimanishi kwamba hakuna vikwazo katika ndoa moja kwa moja baada ya hatua hizo bali itasaidia sana kuondosha ukatili wa mtu kuondoa uhai wa mwingine kwani katika hatua zote ni wazi kwamba kila mmoja amekwisha kujua madhaifu ya mwenzake kwa asilimia zote na bado akaamua kwenda nae kwa tafsri hiyo,mhusika anaweza kubebana na mwenzake katika hali aliyokuwa nayo katika maisha yake yote ya hapa duniani.Katika hatua hii kila mmoja atatakiwa kwa ulazima kukubaliana na mwenzake na kuvumilia jumla ya mambo yote bila ya kuchoka,hii itapunguza kasi ya ukatili katika familia zetu.

HITIMISHO
Pamoja na hatua zote hizo pia kijana wa kike au wa kiume anapaswa kumtanguliza Mungu wake kwa kadiri ya imani yake ili pia hatua hizo ziweze kumpatia matokeo chanya katika maisha yake ya ndoa kama ambavyo hata katika vitabu vya kiimani inaelezwa kwamba mume au mke bora na mwema hutoka kwa mwenyenzi Mungu.Nina amini katika hayo ukatili katika ndoa utapungua kwa kiasi kikubwa kama siyo kuisha kabisa.
 
Upvote 1
nikweli @ Mai Muna,lakini wakati mwingine unaweza kupita njia yako mwenyewe na ukafika salama kuliko upite njia ya wengi alafu ukapata tabu,ahsante!
 
Back
Top Bottom