Hatua za Kufuata katika Utekelezaji wa Mradi (Project Life Cycle)

Hatua za Kufuata katika Utekelezaji wa Mradi (Project Life Cycle)

The Consult

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2017
Posts
220
Reaction score
252
happy-workspace-2.jpg

Mradi ni shughuli (endeavor) yenye malengo maalum inayopaswa kufanyika ndani ya wakati maalumu na kwa kutumia kiasi maalumu cha gharama. Ili mradi uweze kukamilika, rasilimali mbalimbali huhitajika; miongoni mwazo ni; watu, vifaa, fedha, malighafi n.k. Mradi wowote ni lazima uwe na muda maalum wa kuanza (specific starting date) na muda maalum wa kuisha (specific ending date), na hapa ndipo tunapata tofauti kati ya Mradi (Project) na shughuli za kila siku za kampuni (Operation Activities)

Mradi hutekelezwa kwa lengo la kutimiza matakwa ya mteja (Customer's need/expectation). Mteja wa mradi ni taasisi au mtu anaetoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi husika, hivyo utekelezaji wa mradi lazima ukidhi vigezo na viwango vinavyotarajiwa na mteja (Meeting Customer's Expectations). Mfano wa Miradi ni; Kuimarisha/kutanua kiwanda, Utengenezaji wa bidhaa mpya, Uandaaji wa mkutano, Kujenga mji baada ya janga la kiasili, Ujenzi wa shule, Ujenzi wa nyumba n.k

Mafanikio ya mradi kwa kiasi kikubwa hutegemea udhibiti wa gharama (cost), muda (schedule), shughuli zinazopaswa kufanyika (Project Scope) na kuridhika kwa mteja (Customer's Satisfaction). Hivyo Meneja wa Mradi katika kipindi chote cha usimamizi wa mradi jicho lake hupaswa kuangalia vitu hivi.

Katika utelekelezaji wa mradi, hatua zifuatazo hupaswa kufuata ili kuleta matokeo tarajiwa, hatua hizo ni;
  • Utambuzi wa tatizo, fursa au hitaji (Problem/Need/Opportunity Identification), hii hatua ya kwanza, katika hatua hii mteja hufanya utambuzi wa tatizo/hitaji/fursa, aidha katika mfomo wa uzalishaji, mfumo wa usambazaji bidhaa sokoni, n.k. Baada ya kutambua hilo mteja atapaswa kuandaa 'document' maalum ijulikanayo kama " Request for Proposal". Kupitia 'document' hii, mtu mmoja mmoja (Individuals), taasisi au wakandarasi watawasilisha michanganuo "Proposals" wakionyesha ni kwa namna gani watatatua tatizo linalomkabili mteja.
  • Ufumbuzi wa tatizo husika (Development of a proposed solution), hii ni hatua ya pili ambayo hujumuisha uwasilishaji wa mchanganuo (Proposal) kwa mteja unaonyesha jinsi tatizo litakavyotatuliwa. Katika hatua hii, juhudi za mkandarasi (Muwasilisha Mchanganuo) huzingatiwa sana. Muwasilisha Mchanganuo atapaswa kuonyesha 'approaches', rasilimali na muda atakaotumia katika kutatua tatizo la mteja. Kutokana na wingi wa maombi, mteja atafanya tathmini ya maandiko yaliyowasilishwa ili kutafuta andiko bora zaidi, baada ya andiko bora kupatikana, MKATABA huandaliwa kwa ajili ya kazi. Wakati mwingine mchakato unaweza kufanyika ndani ya kampuni pasina kuhusisha watu wa nje, kwa mfano; Uongozi wa kampuni unaibua hitaji, au unaona fursa kisha idara husika hupaswa kuwasilisha mchanganuo (Proposal) ukionyesha namna watakavyotatuta tatizo, uongozi wa juu ukiridhika na andiko, hutoa fedha kwa idara husika kwa ajili ya kutekeleza mradi.
  • Utekelezaji wa mradi (Implementation of Proposed Solution), hii ni hatua ya tatu ambayo hufuata baada ya mteja kuwa amekwishapata 'Proposal' nzuri na makini itakayoweza kutatua tatizo lake. Katika hatua hii rasilimali mbalimbali kama vile rasilimali watu, fedha, malighafi, vifaa n.k hutumika.
  • Kuhitimisha mradi (Project termination),hii ni hatua ya mwisho ambapo shughuli zote za mradi hufika kikomo, katika hatua hii, malipo yote huhakikisha yamelipwa. Jambo la msingi linalopaswa kufanywa katika hatua hii, ni tathmini ya kiutendaji (Evaluating Performance) ya mradi ili kujua wapi kumefanywa vizuri na wapi kumefanywa vibaya kwa ajili ya maboresho ya mradi ujao, pia katika hatua hii, mrejesho (feedback) kutoka kwa mteja hupokewa ili kujua ni kwa kiasi gani matarajio yake (mteja) yamefikiwa.
N:B
Makampuni mengi makubwa duniani kwa sasa yanachukulia PROJECT MANAGEMENT kama ni faida ya kiushindani (Competitive Advantage) ambapo kampuni inapaswa kuwa nayo ili iweze kukabiliana na ushindani sokoni. Mf; Blaine Peters alipoingia RobustArm Global Industries (RGI) kwenye miaka ya 90 kama CEO alijipa cheo cha Meneja wa Mradi (Assumed himself a title of Project Manager) na kuunda 'Project Team' ndani ya kampuni, kisha akatafuta mtaalamu wa Project Management kwa ajili ya kutoa INTENSIVE PROJECT MANAGEMENT TRAINING kwa wafanyakazi wa idara mbalimbali ndani ya kampuni, ikiwemo idara ya uhandisi, lengo lilikuwa ni kuhakikisha shughuli za kampuni zinafanyka katika utaratibu wa projects ili kufikia viwango vya ubora kwa gharama ndogo ndani ya muda mchache.

Ahsante
The Consult +255 719 518 367
Dar es Salaam
Tanzania
 
Attachments

  • English Ad.jpg
    English Ad.jpg
    203 KB · Views: 142
Asante sana kwa uzi mzuri, nimependa jinsi umefafanua kwa undani ila bado sijaelewa sana kuhusu PROJECT/MRADI!!

ni lazima kuwa na PROJECT TERMINATION?

Kwanini Project haiwezi kuwa endelevu au ndio kusema project sio biashara?

Naomba link ya website yenu tafadhali.
 
Chief
Project yoyote huanzishwa kwa malengo. Kuna aina mbili za malengo; Malengo Makubwa (Project Goals/Overall Objectives) na Malengo Mahsusi/Madogo (Project Specific Objectives). Utekelezaji wa malengo haya hususani Malengo Mahsusi (Specific Objectives) hutegemea kiasi cha bajeti kilichopangwa na muda pia uliopangwa wa utekelezaji wa mradi.

KWANINI KUWE NA HITIMISHO LA MRADI? (WHY PROJECT TERMINATION), hitimisho la mradi hutokana na sababu kuu mbili;
  • Kwanza, pindi mradi unapokuwa umetimiza malengo yake (Attained Its Objectives), kama nlivyosema hapo juu, utekelezaji wa malengo haya hutegemea rasimali fedha na muda uliopangwa. Kwa mfano; Unafanya mradi wa kuongeza uzalishaji katika kilimo kwa kaya 50 kwenye Kata X. Miongoni mwa malengo mahsusi ya mradi yatakuwa ni i) Kuzijengea uwezo kaya 50 katika uzalishaji wa mazao ya kilimo kwa matumizi ya chakula na biashara ifikapo Disemba 2019 ii) Kuongeza uzalishaji kwa asilimia.... kwa wakulima wadogo wadogo ifikapo Disemba 2019, n.k. Katika kufikia malengo haya, kiasi cha Shilingi milioni 200 zimetengwa kama bajeti ya mradi. Hivyo tunatarajia ifikapo Disemba 2019 malengo haya yatakuwa yamekamilika, na kiasi chote cha pesa kitakuwa kimeisha/kimetumika. Hivyo kwa mantiki hii, mradi utapaswa kuhitimishwa. Kama utataka kuendelea itakubidi utafute pesa zingine, na malengo u-set upya, na huo utakuwa ni mradi mwingine tena.
  • Pili , kipindi ambacho mradi unaonekana hautofikia malengo. Hii hutokea kama mchakato wa "Project Planning" umefanyika pasina umakini, matokeo yake kuwa na malengo ambayo si mahsusi (Vague) ambayo pia ni vigumu kuyapima, kuyatekeleza, kuwa na bajeti ambayo si ya kina (Undetailed budget) n.k. Katika hali hii, suluhisho ni kuhitimisha mradi na kufanya "Project Designing" upya.
Karibu Chief
 
Safi sana
Je unaweza Fanya mradi kama individual ukaandika proposal na ukapata mkopo bank?? Au kwenye taasisi zozote zinazowezesha?
 
Asante sana chief kwa maelezo,
ila bado sijaelewa vizuri...kwamfano mm nna wazo la mradi fulani na huo mradi nataka uwe endelevu kama biashara je siwezi kuuita mradi?

Na mradi kwa makadilio unaweza kusema ni kuanzia kiwango cha tsh ngapi ili tuuite mradi?
 
Mradi lazma uwe na specific timeline (muda mahususi) ktk kutimiza malengo mahususi (specific objectives)

Ukishatimiza hayo malengo, project inaishia hapo

Vinginevyo, kinachofuata ni operations za hicho kilichozalishwa
 
Back
Top Bottom