Green Beret
JF-Expert Member
- Apr 22, 2022
- 631
- 991
Wakuu naulizia hatua za kufuata kununua kiwanja kwa mtu.
Naomba ushauri nisije kuingizwa mjini
Nawasilisha wakuu
Naomba ushauri nisije kuingizwa mjini
Nawasilisha wakuu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante sana mkuu1. Uliza umiliki wake, imekuwaje mpaka akamiliki hichi kiwanja. Baada ya hapo ndiyo utaamua hatua za kufuata.
2. Kama kina hati ya wizara, mtafute mwanasheria asimamie ununuzi na ikiwezekana uhamishaji wa jina kutoka kwa muuzaji Kuja kwako.
3. Kama kina hati ya kimila, mtafute surveyor kutoka Manispaa aende kupima kwa kuitumia handheld receiver.
Akipata coordinates, ataenda kuangalia kama Kuna ramani ya mipangomiji katika kiwanja chako. Kama ipo, atakueleza hichi kiwanja/eneo limepangwa Kwa matumizi gani eg. Makaburi, hospital, makazi au open space.
Pia utaambiwa kama ramani ya mipangomiji itatakiwa kubadilishwa (amendment) kimchoro au kimatumizi au vyote.
Ukiridhika na gharama ya amendment utaendelea na manunuzi.
Kama hakuna ramani ya mipangomiji utaendelea na hatua ya manunuzi au kama unataka kujenga Shule, zahanati au taasisi utaanza mchakato wa Kujua gharama za planning na surveying. Ukiridhika utaendelea na hatua ya manunuzi.
4. Kabla ya manunuzi, andaa sales agreement. Mkataba wa makubaliano ya manunuzi. Hakikisha mkataba huo unataja jina kamili la muuzaji, eneo kiwanja kilipo i.e mtaa/Kijiji/kitongoji. Pia ukubwa wa eneo, jinsi ya kulipana na kiasi.
Hakikisha mkataba huo unaainisha kuwa malipo kamili ni baada ya Baraza la Kijiji/mtaa kukaa kikao na kupitisha mauziano hayo. Kikao hichi kiwe na quorum na uwiano wa wanaume na wanawake na sahihi zao wote na wewe uwepo. Ikiwezekana mwanasheria akusumamie.
5. Baadae umalizie malipo na msaini hati ya mauziano. Hakikisha wote mnasaini, ukubwa wa eneo umeelezwa, majirani wa pande zote wameelezwa (mipaka) na wamesaini, pia location ya kiwanja imeelezwa.
Mwanasheria, mwenyekiti wa mtaa wasaini na muhuri na mashahidi watie Saini.