Hatua za kufungua shampein(champagne)

Numbisa

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2016
Posts
301,221
Reaction score
1,172,274
1.Kabla Ya Kuanza Kufungua, Hakikisha Chupa Yenye Shampeni Imehifadhiwa Kwenye Ubaridi Kwa Muda Fulani Kwani Kinywaji Hiki Ni Bora Zaidi Kikinywewa Kikiwa Baridi. Unaweza Usiweke Kwenye Baridi Kama Tu Unataka Shampeni Iruke Sana Na Kusambaa Kila Mahali.
2.Itoe Shampeni Kwenye Jokofu Au Mahali Popote Ulipoihifadhi, Futa Chupa Na Kitambaa Lain (Kisafi) Kuzuia Kuteleza Mikononi Mwako.
3. Ondoa Karatati Inayozunguka Shingo Na Mdomo Wa Chupa Ya Shampeni. Ili Kuondoa Karatasi Hiyo, Zungusha Chupa Yako Na Kutazama Kiungio Cha Karatasi Hiyo Na Kuivuta Taratibu.2.Itoe Shampeni Kwenye Jokofu Au Mahali Popote Ulipoihifadhi, Futa Chupa Na Kitambaa Lain (Kisafi) Kuzuia Kuteleza Mikononi Mwako.
4.Utaona Waya Uliosukwa Kuzunguka Kizibo Cha Chupa Ya Shampeni. Waya Huo Unazuia Kizibo Hicho Kisitoke Kunapokuwa Na Presha Kubwa, Joto, Au Mtikisiko.

5.Weka Kidole Gumba Cha Mkono Uliotumia Kushika Shingo Ya Chupa Ya Shampeni, Tumia Mkono Wako Mwingine Kuondoa Waya Unaozunguka Kifuniko Cha Chupa.
Kumbuka Waya Huo Huondolewa Kwa Kuzungusha Ukianzia Sehemu Ya Pembeni Iliyofungwa Kama Kitanzi.

6.Ondoa Waya Na Kuuweka Pembeni. Bila Kuachia Kizibo, Unaweza Kutikisa Chupa Mara Kadhaa Kama Unataka Shampeni Iruke. Kama Hutaki Iruke Basi Usitikise Chupa Hiyo.

7. Weka Kitako Cha Chupa Tumboni Kwako Ili Kuipa Balance Huku Mdomo Wa Chupa Ukiangalia Juu Kwa Nyuzi 45 (45 Degrees). Hii Itazuia Kizibo Au Shampeni Kumrukia Mtu Aliyeko Karibu Wala Wewe.8.Achia Kidole Kilicho Juu Ya Kizibo, Huku Mkono Wako Mmoja Ukiwa Umeshika Shingo Ya Chupa (Usiielekeze Chupa Kwa Mtu) Na Mwingine Ukiwa Huru.
9. Anza Kuzungusha Kizibo Cha Chupa Taratibu Kulia Na Kushoto Huku Ukikivuta Taratibu Sana Mpaka Kitoke. Kumbuka Unaweza Kukiachia Kiruke Au Kukishikilia Kama Ni Tafrija Inayohitaji Utulivu Sana.
10.Hongera, Umeshajua Kufungua Shampeni. Nyanyua Chupa Juu, Na Kuanza Kugawa Kwa Watu.
.

Chanzo: HATUA KUMI ZA KUFUATA (Pamoja na Picha) UNAPOFUNGUA CHUPA YA SHAMPENI (Champagne)
 
Hongera kwa somo zuri, huu uzi ungekuwa wa mapenzi nazani ungekuwa ushafikisha wajumbe hata 300 hadi sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…