MAKULILO
Member
- May 30, 2010
- 84
- 95
NA: ERNEST BONIFACE MAKULILO (MAKULILO, JR.)
CALIFORNIA, USA
View attachment 46332
Ufuatao ni muendelezo wa hatua za kufuata ili mtu uweze kupata udhamini wa elimu ya juu ughaibuni. Na katika wiki iliyopita tuliona vitu vikubwa viwili navyo ni Barua ya Motisha (Statement of Purpose) na Insha ya Udahili (Admission Essay). Leo hii tutaangalia hatua nyingine ambayo ni Barua ya Mapendekezo (Recommendation Letter).
Barua ya Mapendekezo (Recommendation Letter) ni nini? Ni nani anatakiwa kuandika? Nini kinatakiwa kuandikwa? Ni barua ngapi zinahitajika? Njia zipi za kufanikisha kutuma barua hizi? Haya ni maswali muhimu ambayo mtu ukiyajua na kuyafanyia kazi itakuwezesha kuwa mwamboji mshindani na si msindikizaji.
Barua ya mapendekezo ni barua ambayo ni muhimu sana ambayo wanaodahili huitumia kama kigezo kikubwa cha nani achukuliwe na kupewa udhamini na nani aachwe. Mtu unaweza kuwa na matokeo mazuri sana, ila ukawa na barua ya mapendekezo mbovu inayoonesha kuwa huna uwezo nk hivyo utashindwa kudahiliwa na kupata udhamini sababu ya barua hiyo.
Kila chuo utakachoomba unatakiwa utume barua za mapendekezo. Barua hizi zinatakiwa ziandikwe na aidha mwalimu wako aliyekufundisha au mwajiri/mkuu wako katika fani unayofanyia kazi. Kama ni mwalimu wako anayeandika barua hii ni lazima aoneshe uwezo wako wa kuandika insha makini zenye utafiti ulioshiba, uwezo wako darasani kwa ujumla, matarajio yake kama wewe ukipata nafasi hiyo utafanya nini nk. Na kama ni mwajiri au msimamizi wako kazini akiandika barua hii ni vyema aoneshe uwezo wako kikazi upo vipi, mchango wako kazini na ni nini matarajio yao endapo wewe utapata nafasi ya kusoma chuo uombacho ni mabadiliko gani unaweza kuyaleta katika ofisi hiyo na/au jamii yako husika.
Mara nyingi unapoombwa kupeleka barua za mapendekezo hupendelea barua tatu kutumwa. Ushauri wangu ni vyema upeleke barua si chini ya nne, yaani barua mbili toka kwa mwajiri au msamizi wako kazini, na barua mbili toka kwa mwalimu wako aliyekufundisha. Hii itaonesha kuwa una watu wanaoamini uwezo wako.
Si kila mtu kwakua alikua mwalimu wako basi ana sifa za kukuandikia barua za mapendekezo au kwakua mtu ni mwajiri wako au msimamizi wako kazini basi ndio akuandikie barua hizi. Kuna waajiri wengine hawapendi wafanyakazi wao waende kujiendeleza kielimu, au kuna wasimamizi wengine wanakuwa na chuki binafsi au kutopenda maendeleo ya mwingine, sasa ukimpa nafasi ya kukuandikia barua ya mapendekezo anaweza kutumia fursa hiyo kukuangamiza kwa kuandika kuwa una uwezo mdogo, hufai na huwezi kuleta mafanikio yoyote kwa jamii yako. Barua ya namna hiyo itakufanya uondolewe kwenye kinyanganyiro cha watu wanaweza kupata udhamini. Hivyo uchaguzi wa mwalimu gani au msimamizi gani kazini akuandikie barua ni muhimu sana.
Kuna njia kuu mbili ambazo hutumiwa mwandikaji wa barua za mapendekezo kuwasilisha barua hizo. Njia hizo ni njia ya kwenye mtandao (online recommendation) na njia ya barua kwa njia ya posta (snail mail). Itategemea chuo na chuo, kuna vyuo ambavyo wao wanampa mwandikaji barua chaguo yeye angependa atumie njia gani kati ya hizo, ila kuna vyuo wanakuchagulia utumie njia gani kuwasilisha barua hiyo kama ni kwa njia ya mtandao au barua kwa njia ya posta.
Endapo barua itakuwa inaandikwa na kutumwa kwa njia ya posta, ni lazima barua hiyo iwe kwenye bahasha ya kiofisi yenye nembo ya ofisi au chuo husika. Na pia barua iandikwe kwenye karatasi la kiofisi lenye nembo ya chuo au ofisi husika (official letter head). Pia muhuri wa ofisi au chuo husika ni vyema uwepo ili kuthibisha. Na endapo barua itawasilishwa kwa njia ya mtandao ni vyema anuani ya barua pepe ya mwandishi wa barua hiyo iwe ya kiofisi na si anuani binafsi. Mfano wa barua pepe binafsi ni zile kama za yahoo.com, gmail, hotmail nk, na zile za kiofisi huwa zinakuwa na tovuti ya kiofisi mwishoni mwake, mfano Makulilo@makulilofoundation.org. Endapo hutofuata masharti hayo kuna walakini wanaodahili kuanza kuhisi kuwa barua iliyowasilishwa ni ya kugushi na si halali, kupewa walakini. Inabidi uondoe huo walakini kwa kuwa makini katika kila hatua. Na kama pia barua hiyo itaandikwa kwa kutumwa kwa njia ya posta ni vyema barua hiyo iandikwe mapema na kutumwa mapema ili iwasili kabla ya tarehe ya mwisho ya kupokea maombi.
Napenda kukupa anuani hizi mbili za tovuti ambazo zitakusaidia kujua zaidi kuhusu barua za mapendekezo na utaweza pia kupata sampuli baadhi. Anuani hizi ni www.recommendationletters.org na www.lettersofrecommendation.net
Pia nimeandaa video ambayo inatoa maelezo mazuri kuhusu barua hizi na ninaamini itakuwa ya msaada sana kwako. Tovuti yangu ya www.makulilofoundation.org ina video hiyo. Na kwa video nyinginezo za msaada wa kupata udhamini ughaibuni zinapatikana katika Makulilo Scholarship Show inayoongozwa nami www.youtube.com/makulilofoundation
Kwa wenye maswali au maoni, niandikie hapa Makulilo@makulilofoundation.org. Fuatalia mfululizo wa hatua za kupata udhamini ughaibuni katika makala inayofuata.

MAKULILO, Jr.
CALIFORNIA, USA
CALIFORNIA, USA