Katakata kabichi yako iwe nyembamba.....
Osha chuja maji maana inajua kukaa na maji
Katakata karrot (ukizigrate itakuwa bomba)
Hoho na kitunguu maji
Kaanga mafuta kidogo, weka kitunguu maji, koroga kama una tumajani twa rosemary unaweza tia kiduchu kuweka harufu.....( kama una nyama ya kusaga unaweza tia kiduuuuuchu kuongeza utamu)
Weka kabiji geuza
Weka karoti (ukitanguliza karoti itanyonya mafuta unaweza jikuta unaongeza mafuta kumbe unaharibu)
Ikikaribia kuiva weka hoho
Then ikiiva weka pembeni tia chumvi kiasi upendacho (hii ni ili kuepuka kutoa maji, mboga ya majani ukiitia chumvi wakati ipo kwenye moto inatoa maji sana) pakua tayari kwa kuliwa....
Unaweza kutia nyanya kama utapenda... ukishakaanga vitunguu kaanga karoti (hapa usizigrate? Ongeza nyanya, halafu chumvi then hoho kabichi (ingawa ukiweza hoho tia mwishoni maana sizipoiviana sana hutoa harufu nzuri zaidi) ila ukitia nyanya kuwa makini itatoa maji sana