ImanHB
Member
- Mar 14, 2019
- 10
- 17
Sadoth H. Balilonda
( Mjasiliamali )
sadothhenry250@gmail.com
+255756536474/+255676436474
Makala hii inatoa muamko ambao unalenga kuchochea mabadiliko katika nyanja mbalimbali za uchumi kupitia biashara, kilimo, sayansi na teknolojia, afya, maendeleo ya jamii na uajibikaji kwa ujumla. Lengo ni kujenga taswira nzuri ya maendeleo ya uchumi wa taifa
Shughuli na vyanzo vya uchumi ambavyo idara husika zikisimamia vyema
zitaleta tija katika Taifa.
Pato la taifa hutegemea zaidi kilimo, hivyo inaonyesha ni jinsi gani kilimo kina mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa. Kwakuwa zaidi ya asilimia 80 ya ardhi hapa nchini inatawaliwa na wakulima wadogowadogo wakitegemea jembe la mkono, plau na trekta kwa baadhi yao, serikali kupitia wizara ya kilimo itenge bajeti ya fedha ambazo zitamuwezesha mkulima kutatua changamoto za pembejeo, mbegu bora, mbolea na hata pia wapatiwe mafunzo ya elimu ya kilimo bora. Siyo hilo tu lakini pia ni wazi kuwa nchi hii inakumbwa na migogoro ya ardhi, hii ni kwa sababu sehemu kubwa ya ardhi haijapimwa na kuendelezwa, hivyo hupelekea watu kufanya shughuli zao tofauti na matumizi ya eneo husika kama kuchoma misitu, kuweka makazi hifadhi za wanyama na kuchunga mifugo maeneo yasiostahili.
Afya bora kwa jamii ni jambo la kupewa kipaombele, si kwa kuitegemea serikali tu kama ilivyo ada, ijenge vituo vya afya vyenye dawa za kutosha na watoa huduma wa kukidhi mahitaji ya wagonjwa. Pia ni jukumu la jamii kwa kila mtu kuchukua hatua stahiki juu ya changamoto zinazoweza kuathiri afya zetu ikiwemo kuzingatia usafi wa mazingira yanayotuzunguka na kuhakikisha vitendea kazi na vyakula tunavyotumia viko salama kwa afya zetu. Na kwa upande mwingine tunapaswa kuchukua tahadhali dhidi ya milipuko ya magonjwa yanayojitokeza, hasa kwa wakati huu mgumu tunaopitia wa janga la Corona, ni wazi tunahitajika kuchukua tahadhali zaidi kwa kutekeleza maagizo yanayotolewa na wizara za afya kujikinga na gonjwa hili.
Tume ya taifa ya sayansi na teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na taasisi zingine pamoja na vyuo vya sayansi na ufundi stadi ndani na nje ya nchi, ni wakati sahihi wa kukaa pamoja kujadili, kutatua na kutathminni ni nini kifanyike ili kukuza na kuendeleza ujuzi wetu wa ndani.
Tanzania tunaweza, wapo vijana wengi katika jamii zetu wanao ujuzi, vipaji na ndoto za kufika mbali kimaendeleo kulingana na vipawa tofautitofauti walivyojaaliwa na Mwenyezi Mungu na wengine ni wazee sasa wamezeeka navyo, nani wa kuwashika mkono? Haya ni malighafi, idara, tume na taasisi za elimu chonde tunaomba zifanye maboresho katika mitaala yake ya elimu. Kuwepo na vitengo vya elimu maaalumu ya kuinua vipaji kwa kila mtanzania mwenye ujuzi wake na hata wale angali bado wana umri mdogo.
AJIRA; Vijana ndio nguvukazi ya taifa. Tumegawanyika katika makundi tofauti kwa ngazi mbalimbali za elimu. Naweza kusema ya kwamba tumekuwa tukijijengea dhana, malengo, fikra na mitazamo hasi katika swala la ajira hasa kwa wahitimu. Kuajiriwa ni jambo la kheri katika hatua za mafanikio, lakini kulingana na sababu nyingi ikiwemo utekelezaji wa miradi ya kimikakati kuwa wa hali ya chini, uhaba wa viwanda na makampuni mengi kuzingatia sifa za ufaulu kwa waombaji, ukweli wengi wetu huishia manung'uniko. Kizazi cha sasa wasomi ni wengi nafasi za ajira ni chache ukweli hazijawahi kukidhi idadi ya wahitimu katika muhula husika.
Ukosefu wa ajira mtaani ; Chanzo IPP Media
Hivyo basi nini cha kufanya?...Tuamke, tuwajibike na kuondoa dhana ya kusubiri kuajiriwa iwe una degree au haujabahatika kupata elimu, badala yake kutumia fursa na vipawa tulivyonavyo kujenga mifumo sahihi ya kujiajiri. Angalia faida za kujiajiri link hapo chini
Faida za kujiajiri
LABDA NIKUSHUHUDIE: "Mimi mwenyewe Mungu ni muweza nilibahatika kupata elimu ya kidato cha nne mwaka 2015. Nilipomaliza nikafanikiwa kupata ufaulu wa kujiunga na chuo cha uuguzi Geita, nikatuma maombi ya kujiunga yakapokelewa. Lakini kwa bahati mbaya gharama za masomo zikawa kubwa kulingana na corse niliyochukua hivyo sikuweza kuimudu kutokana matatizo ya kifedha. Hivyo basi nilikuwa na rafiki yangu nilieishi nae kama ndugu yeye alikuwa anajishughulisha na uuzaji wa miche ya matunda, ndipo na mimi nikaona bora nijiegeshe kwake nikiwa namsaidia saidia kuchanganya udongo, mbolea na kupakia kwenye vimfuko. Baada ya miezi 3 nikawa na uzoefu, Mungu amjaalie zaidi alinipa kaeneo pembezoni na kunishauri nianze kupanda miche yangu mwenyewe. Kwa juhudi namshukuru Mungu bustan yangu ilipanuka na kupata wateja. Lakini akili yangu haikukomea hapo, nilipopata akiba ya kutosha mwaka 2017 mwezi 5 nilimuajiri mtu wa kusimamia bustan, nikajiunga na kalakana ya uchomeleaji hapohapo mtaani. Baada ya mwaka mmoja na nusu kujua ufundi, mwaka juzi 2019 mwezi wa pili wishoni kwa fedha ninazoingiza kwenye bustani nikafungua kalakana yangu mwenyewe. Na amini usiamini mpaka sasa namiliki kalakana mbili ya welding (uchomeleaji) na ya Alminium pamoja na bustani kubwa."
Mimi ni nani na wewe ni nani ushindwe. Elimu yako ulionayo kamwe haiwezi kuamua kiwango cha mafanikio yako ya baadae, bali ni juhudi zako tu ndizo zitakazoamua. THUBUTU UNAWEZA!!!
( Mjasiliamali )
sadothhenry250@gmail.com
+255756536474/+255676436474
Makala hii inatoa muamko ambao unalenga kuchochea mabadiliko katika nyanja mbalimbali za uchumi kupitia biashara, kilimo, sayansi na teknolojia, afya, maendeleo ya jamii na uajibikaji kwa ujumla. Lengo ni kujenga taswira nzuri ya maendeleo ya uchumi wa taifa
- Tunapozungunzia uchumi tunazungumzia jumla ya shughuli zile zote za kibinadamu zinazomuingizia mtu kipato kinachotosheleza mahitaji yake. Kuna shughuli kadha wa kadha ambazo kila mtu ni kipao mbele chake kujimudu kimaisha hasa katika uzalishaji. Hii ni kwa ngazi ya chini {jamii}, kwa upande wa serikali, uchumi unatafasilika kwa upana zaidi {kitaifa}. Kuna shughuli mbalimbali za uchumi nazo huegemea katika idara za serikali ambazo ndio watendaji wakuu kuhakikisha shughuli hizo zinanufaisha jamii na kuliingizia taifa kipato sahihi.
Shughuli na vyanzo vya uchumi ambavyo idara husika zikisimamia vyema
zitaleta tija katika Taifa.
- MIUNDOMBINU BORA
- KILIMO
- AFYA
- SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Tanzania tunaweza, wapo vijana wengi katika jamii zetu wanao ujuzi, vipaji na ndoto za kufika mbali kimaendeleo kulingana na vipawa tofautitofauti walivyojaaliwa na Mwenyezi Mungu na wengine ni wazee sasa wamezeeka navyo, nani wa kuwashika mkono? Haya ni malighafi, idara, tume na taasisi za elimu chonde tunaomba zifanye maboresho katika mitaala yake ya elimu. Kuwepo na vitengo vya elimu maaalumu ya kuinua vipaji kwa kila mtanzania mwenye ujuzi wake na hata wale angali bado wana umri mdogo.
- UWAJIBIKAJI NA MAENDELEO YA JAMII

Upvote
3