Hatua zilizopo sasa za kukabiliana na UKIMWI, tiba na huduma

Hatua zilizopo sasa za kukabiliana na UKIMWI, tiba na huduma

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Acquired Immune Deficiency Syndrome (AIDS) ilijulikana kama ugonjwa mpya mwaka 1981. Kadiri miaka ilivyokwenda virusi vya UKIMWI viligundulika 1985. Kipindi hiki ukisikia ugonjwa huu hofu na uoga vilitawala duniani. Kunachosikitisha ni kuwa kuna wengi wanye maambukizi lakini hawajijui.

Binadamu tuna DNA (deoxyribonucleic) ambayo ni genetic material kwenye chembe hai za mwili, HIV virus wana RNA (ribonucleic acid) kama genetic material. Baada ya maambukizi HIV virus wana reverse transcriptase na kubadilisha RNA kuwa DNA. Retrovirus wanaingia kwenye cell halisieya mwili DNA na kuiamrisha izalishe virus zaidi vya Ukimwi. HIV RNA huingia kwa mlangi wa CD4 cells. CD4 ni sehemu muhimu ya kinga ta mwili na kazi yake kubwa ni kukinda wavamizi kama fungus, Kandinsky, parisites, bacteria na hata cells zinazoanza dalili za cancer.

Uharibifu huu wa kinga ya mwili baada ya muda humsababishia mtu aliye na maambukizi kushambuliwa na magonjwa mbali mbali.

Tiba iliyopo ya kukabiliana na UKIMWI ni Highly Active Antirectroviral Therapy (HAART) ambayo ni mchanganyiko wa dawa mbili au tatu unaozuia HIV replication kwenye cell. HAART imefanya UKIMWI kuwa gonjwa sugu sasa hivi kutoka kwenye hatari ya kifo.

Katika kujilinda na UKIMWI waganda walikuja na ABC
A- abstinence
B- be faithful
C- use condoms

Canada walikuja na ‘on me not in me’.

Siku za karibuni mbinu mpya za kuzuia maambukizi zimekuja baada ya maendeleo ya tiba kuleta matumaini.


1. Kukumbusha matumizi ya condom.

2. Kufikia UNAIDS 90 tatu.

3. Kuhimiza watu wapimwe na kuanza dawa mapema.

4. Kuelimisha watu kuhusu matumizi ya PrEP.

90 tatu za UNAIDS ni
1. 90% ya wenye maambukizi wawe wamepimwa .
2. 90% ya wanaogundulika na maambukizi waanze kunywa HAART
3. 90% ya watumiaji wa HAART wafikie undecteble status. Kutoka na utafiti uliofanywa, wenye undecteble status hawaenezi maambukizi mapya. Hii si Christmas kwao ila wajijue kuwa kinga zao za mwili bado ni dhaifu hivyo kubadilisha wapenzi ni hatari kwao.

90% ya waathirika waliupata ugonjwa huu kwa njia ya ngono, na wengi bado wanashiriki ngono. Kuelimisha jamii kuhusu ngono salama bado ni muhimu.

Makundi mawili yaliyo hatari zaidi ni 50+ na vijana. Hawa wa 50+ wengi walikuwa kwenye ndoa muda mrefu na sasa wengine wameachika au kufiwa. Wamesahau kabisa habari ya ngono salama.

Vijana wanapenda kujaribu na wanaanmbiana kavu ni tamu. Kumbukeni ngono salama vijana.
 
Hivi kumbe bado kuna kitu kinaitwa UKIMWI hapa nchini?
 
Back
Top Bottom