Hatuko Salama: Vodacom kuiingilia Privacy za wateja

Hatuko Salama: Vodacom kuiingilia Privacy za wateja

Mi kila nikiingiza pesa Mpesa alaf nikawasiliana na mtu ili nifanye miamala ndo muda huo huo ndo zinaingia sms za matapeli "ile hela tuma kwenye namba hii"

Sahiv hata mama yangu mzazi akiniomba hela kwa sms nampigia simu kwanza kuhakikisha Kama Ni kweli Ni yeye ndo naituma,.
 
Mkuu hakuna uhuru binafsi kwenye ulimwengu wa mawasiliano dunia nzima' kinachotokea kwako ni bugs kwa application unayotumia au mtandao husika wa mahali ulipo' Siku ukipata dharura halisi ya tatizo la kimtandao na ukapata kibali kisheria unaweza kupata msg yako ya kwanza toka umepata kitambulisho cha kupigia kura'
 
Inasikitisha na ina hatia hasira sana. Kinachoondelea Vodacom wanasoma meseji na kusikiliza maongezi ya wateja wao ambapo ni kinyume na sheria.

Vifurushi ninunue mm tena mniuzie kwa bei ghari na mnipangie cha kutuma. Kwann? Kila siku mnapandisha vifurushi na bado mnaingilia privacy za wateja wenu. Mnatafuta nini?

Leo mke wangu alisema ananitumia picha zake. Cha kushangaza kila nikiandika meseji hii 'amezituma whatsapp au facebook?' na meseji zinazofanana na hizo haziendi ila nikituma zingine zinaenda. Hilo hizo haziendi. Kwanini? Nimezituma tena na tena zimegoma kwenda. Kwanini?

Vodacom nyinyi kazi yenu ni kupeleka ujumbe, haijalishi una maudhui gani. Hayo mengine wala hayawahusu.

Mnabahati sana tuko kwenye dunia ya 3 ambapo sheria ametungiwa masikini. Tungekuwa dunia ya kwanza, ningewapeleka mahakamani na mngenilipa kwa kuniletea usumbufu. Siokoti hela, nazitafuta kwa jasho.

Hizi ni meseji zenye alama nyekundu. Zimeshindwa kwenda. Sasa hivi natuma meseji haziendi kabisa.
Hatuko salama even kwenye face to face conversation...dunia ya wenyewe hii
 
Hapo hakuna technical evidence ya ujumbe kusomwa. Kinachoonekana ni words filtering ambayo inaweza kuwa kwao au kwenye SMS application unayotumia.

Najua mara moja utajbu wewe hujaweka filter yoyote, unaweza kuwa sawa lakini kuna app bugs, hilo ni tatizo kwenye application unayotumia ambapo mara nyingi hutokea baada ya updates

Jaribu tena kutuma msgs hizo hizo kwa kutumia ROM default SMS app uone kama bado zitagoma
Mshamba wa simu huyo, kitu kidogo anakurupuka na tuhuma za Pentagon.

Hata mm huwa inatokea hivo ila ukwel ni huo kuna maneno simu inayafungia kama mabaya (abuse) ukiliweka sms haiend, ni had uende setting ya hiyo app na kuondoa ama utumie app nyingine ya kutuma na kupokea sms
 
Duniani kote mawasiliano yanakuwa tapped ukitaka acha kutumia mawasiliano ya kisasa urudi kwenye ujima. By way kama huvunji sheria za nchi kwa nini uwe na wasiwasi?
Sio kweli. Kuna app kma Signal zinazotumia end to end encryption na zinaendeshwa na non profit organization. Hata ukienda kuiba database zao huwezi soma msg ya mtu yoyote bila keys zilizopo kwenye simu ya muhusika. Na hizo keys kwenye simu ya muhusika hazionekani kirahisi rahisi.

Watakachoweza ona ni username tu labda na contacts details. Lakini content za msg hawazioni
 
Duniani kote mawasiliano yanakuwa tapped ukitaka acha kutumia mawasiliano ya kisasa urudi kwenye ujima. By way kama huvunji sheria za nchi kwa nini uwe na wasiwasi?
Kwenye point ya kutovunja sheria hapo huwezi kuwa na uhakika kuwa hujavunja sheria yoyote kupitia simu yako na matumizi yako.
Kuna makosa madogo madogo tu ambayo unachukulia simple lakini yanaweza tumiwa zidi yako kortini hata kama ulikua na kesi tofauti. Hapo unaweza ukawa umepitia akina dj mwanga na umedownload nyimbo za wasanii bila ridhaa yao, unajua kuwa hilo ni kosa kisheria? Unajua kuwa voda wanaona website url unazopitia kwenye simu yako?


Nadhani unajua watu wanavyobakiziwa kesi huku mahakamini huko kwa mambo madogo tu. Kuwa makini
 
Ndo maana sikuizi nikiwa na inshu binafsi za kuchati na mtu, namtumia link ya game mf. 8pool table. Tunachat huko ndani ya game tukimaliza kila kitu kimeishia hapo!
 
Mitandao ya simu haitunzi privacy za wateja hiyo inajulikana na nishawahi andika Uzi huku mwaka 2016.
Nakumbuka Nlikuwa natumia Tigo, mfanyakazi mmoja wa tigo by then alikuwa ananifukuzia alikuwa anasoma text zangu bila me kujua. Kuna siku akanambia everything nlivyokuwa na chat na watu ambao nlikuwa nawasiliana nao Sana.
Since then Mimi kuchat Ni WhatsApp tu hakuna third party wa kusoma text. SMS Mara moja moja Sana
 
HEBU WEKA NAMBA YA MKEO HAPA NIJARIBU NAMI KUMTUMIA MESEJI NIONE KAMA ITAGOMA AU ITAKUBALI. TUPATE UHAKIKA. maan tusije fungua kesi kumbe sivyo. TUMA NAMBA YA MKE PLEASE.
 
Sio kweli. Kuna app kma Signal zinazotumia end to end encryption na zinaendeshwa na non profit organization. Hata ukienda kuiba database zao huwezi soma msg ya mtu yoyote bila keys zilizopo kwenye simu ya muhusika. Na hizo keys kwenye simu ya muhusika hazionekani kirahisi rahisi.

Watakachoweza ona ni username tu labda na contacts details. Lakini content za msg hawazioni
Hicho ulichokisema ni nadharia tu mkuu siyo uhalisia. Siku ukisoma zaidi mambo ya computer na applications zake utajua zaidi. Vyombo vya usalama duniani haviwezi kukubali kuwa na application ambayo hawana uwezo wakuijua in and out hata huyo mtengenezaji anajua loop hole zake.
 
Labda sijui uache kutumia mawasiliano ya simu.lakini akuna mtandao ama nchi isiyofatilia mawasiliano ya watu kwa ulimwengu wasasa ulivyo wa hovyo kwa usalama na mambo mengine.
 
Alizoea meseji za bure hujui vifurushi vimebadilika sasa hivi mwambie "mitano tena"
Punguza Ugolo mkuu, Sasa hapo Vodacom wamesoma meseji vipi ?


Kwanini usingeuliza unapotuma meseji haziendi tatizo ni Nini ili usaidiwe!?
 
Back
Top Bottom