Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Baada ya kufungana aggregate ya 2-2, Algeria imepewa kombe kwa vile walitufunga hapa kwetu bao moja zaidi. Ni sheria za CAF ambazo zimepitwa na wakati kwa vile kama wote tulivyoona mazingira ya Mkapa Stadium yalikuwa ya kistaarabu ila mazingira ya July 5 Stadium ulikuwa ya kishenzi sana kiasi kuwa ilibidi refarii asimamishe mchezo ili kupisha moshi uliokuwa unajaa uwanjani kiasi cha kuwafanya wachezaji wasione mpira.
Hata hivyo tulimaliza mashindano kwa kufungana 2-2; ukweli huo hauwezi kufutika ingawa ukweli mwingine ni kuwa 2-2 yetu haikutosha kutupatia kombe kutokana na utaratibu mbovu wa CAF uliopitwa na wakati. UEFA, AFC, CONCACAF, CONMEBOL na OFC hawana upuuzi huo tena.