Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Kuna dadangu mdogo mmoja anataka kuja kusomea mambo hayo ya forensics (nadhani amekuwa kiangalia CSI na NCSI too much) na sasa anataka kujifunza mambo hayo ili kusaidia katika mambo ya kupambana na uhalifu. Nimemuuliza kwanini asitafute Chuo TZ ambacho kinafundisha kozi hizo na nitamsaidia kugharimia.
Anarudi na kuniambia kuwa hajaona kozi yoyote ya mambo ya forensics kwa kiwango cha shahada. Sasa sijui hii ni kweli?
Nilipoangalia lile tukio la ujambazi Temeke na matukio mengine ya uhalifu ninajiuliza hivi tunatumia teknolojia gani au mbinu gani za kisasa katika sayansi ya mambo ya uhalifu (criminology)?
Je, ipo haja ya kuwa na watu waliosomea katika forensics ndani ya nchi au tutaendelea kuwapeleka nje ya nchi mmoja mmoja? Je, kwa yawezekena kwa UDSM kuanzisha kozi ya namna hiyo ambayo itavutia labda wanafunzi kutoka sehemu kubwa ya Afrika ya Mashariki na Kati hasa kutokana na uwepo wa uhalifu wa kila aina na vita badala ya kuendelea kutegemewa wakwe zetu kututumia forensics experts kila tunapopatwa na majanga makubwa?
Oh we are too poor to afford such a modern necessity in law enforcement?