Hatuna Serikali Mbili Tu, Tuna Nchi Mbili Pia

Hatuna Serikali Mbili Tu, Tuna Nchi Mbili Pia

Mautino

Member
Joined
Feb 20, 2014
Posts
42
Reaction score
22
Tatizo la akina Mrema na Shibuda wanaojidai kupigia debe serikali mbili ni kwamba wako ndotoni. Katiba ya Zanzibar, ambayo inaitambulisha Zanzibar kama nchi, imeshaondoa uhalali wa Muungano (Mimi siyo separatist, lakini sielewi kwa nini Wanzazibari wanashiriki katika mchakato wa Katiba sasa hivi wakati wana Katiba yao na nchi yao kamili)

Ndani ya Tanzania kwa sasa hivi hatuna serikali mbili katika nchi moja - tuna nchi mbili na serikali mbili! Kuufumbia macho ukweli huo ni kujiliwaza wakati kisheria/Kikatiba, Zanzibar ni nchi kamili!

Sasa huo Muungano tunaouzungumzia ni Muungano kwa msingi upi? Kwa hiyo hati feki ya Muungano ambayo mnaona hata aibu kuiweka hadharani?
 
Usiogope nchi moja kubwa imeimeza ndogo, hiyo katiba huru ya zanzibar ni kama ki samaki kidogo kinachoogelea kwa uhuru ndani ya tumbo la nyangumi
 
Yaani Zanzibar ni nchi ndani ya kwenye makaratasi ya hiyo katiba tu. Tafuta publications,journals na vitabu hautakuta kuwa kuna nchi ya Zanzibar. Wametaka nchi isiyo na mamlaka. Unabaki na jina la nchi huku huna hadhi ya kimadaraka ya ki-nchi.
 
Bunge la katiba lina lazi moja tu kukataa Tanganyika kurudi na kuhakikisha katiba ya Zanzibar inaondoka.
 
Back
Top Bottom