Tatizo la akina Mrema na Shibuda wanaojidai kupigia debe serikali mbili ni kwamba wako ndotoni. Katiba ya Zanzibar, ambayo inaitambulisha Zanzibar kama nchi, imeshaondoa uhalali wa Muungano (Mimi siyo separatist, lakini sielewi kwa nini Wanzazibari wanashiriki katika mchakato wa Katiba sasa hivi wakati wana Katiba yao na nchi yao kamili)
Ndani ya Tanzania kwa sasa hivi hatuna serikali mbili katika nchi moja - tuna nchi mbili na serikali mbili! Kuufumbia macho ukweli huo ni kujiliwaza wakati kisheria/Kikatiba, Zanzibar ni nchi kamili!
Sasa huo Muungano tunaouzungumzia ni Muungano kwa msingi upi? Kwa hiyo hati feki ya Muungano ambayo mnaona hata aibu kuiweka hadharani?