Hatupaswi kufurahia matokeo ya Kidato cha Nne, hayana uhalisia

Hatupaswi kufurahia matokeo ya Kidato cha Nne, hayana uhalisia

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Nawasalimu kwa jina la Chama Cha Mapinduzi.

Toka mwaka jana nilianza kupata mashaka makubwa kuhusu haya matokeo yaliyosheheni division one za saba kiasi cha kutia shaka. Leo nimebahatika kupata sababu mbili za kuyapuuza haya matokeo ya kisiasa;

1. A kwa sasa inaanzia 75% badala ya 81% iliyokuwepo kwa miaka mingi. Kama tayari iko wazi kwamba mitihani imelegezwa hakukuwa na haja ya kutanua goli ili wanafunzi wapate A kirahisi. Wizara ya elimu inatakiwa itoe majibu ya kina kuhusu hili.

2. Hakuna penalty ya Hesabu. Hii sababu namba mbili ndo imefanya kuwepo na One nyingi sana zilizokosa uhalali. Hivi tunaandaa taifa gani lisilojua hesabu huko mbeleni? Hesabu ni sehemu ya maisha ya kila siku ilipaswa iachwe na penalty yake kama ilivyokuwa. Waliofanya huu uamuzi wa kuondoa penalty kwa F ya hesabu ninawalaani. Ni uamuzi wa kushoofisha kabisa taifa. Ni wahujumu.

Ni wito wangu Wizara ya elimu kujirekebisha na kuondoa huu uozo uliopo. Mwisho kabisa naomba kama kuna mtu mwenye list ya shule zote za sekondari zinazomilikiwa na CCM anitumie ili niangalie matokeo yao kwasababu naamini watakuwa wamefanya vizuri sana maana wao ndo wenye ilani ya uchaguzi.


matokeo.JPG
 
Maafisa Biashara wa Halmashauri unawauliza kuhusu kukovent service charge ya 0.3% into decimal wanakodoa macho tu.....tuna safar ndefu sana.
 
Minaona hata wakiongeza hizo asilimia haisaidii kitu mana elimu yetu haina msaada kwa watu wake kama mwalimu anapata 34000 kwa mwezi ni kupotezeana muda mitaala yetu mibovu ya hovyo haina msaada
 
Anhaa [emoji28] kumbe haya yanahesabiwa!? Kuna kitu hakipo Sawa hapa
Huelewi kitu kuhusu maswala ya taaluma na elimu kwa ujumla! Yaani unataka masomo ya ufundi technical yasihesabiwe? Shule zan ufundi hazina somo la Physics badala yake wana somo linaitwa Engeneering Science. Kuna masomo kama Additional Mathematics ambayo huwezi kuyafundisha kila mtu, Masomo kama Civil Engineering, Electrical Engineering, Electronics, Computer studies and the likes unataka yasihesabiwe?
 
Back
Top Bottom