Kwa masikitiko kabisa na kwa mara ya kwanza in history chini ya uongozi wa Barba SSC imedhalilika na kupata aibu ya mwaka.
Hayo mambo yanayotokea ya kuazima makocha ni kitu ambacho kimeiondolea SSC ile standard yake na ukubwa wake, yaani imekuwa ni kama klabu ya wahuni na hii ina impact kubwa kwenye ulimwengu wa investors na sponsors. Guys hakuna kitu muhimu kama kutunza reputation yako. Barba anaua reputation ya klabu kwa kasi ya ajabu.
The worst nightmare ni kumbe hata huyo kocha Juma cheti hana, lakini kwenye public statement imeelezwa ndiyo kocha wa muda, ni aibu ni aibu, kumbe hata Juma hakuchunguzwa na kuulizwa ni kweli ana hivyo vyeti? Jamani SSC, mbona hii ni kazi rahisi sana kabla hamjaja kwa public!
Barba una shida gani ? What is wrong with you ? Kuna shida gani kwa kichwa chako?
Hii ni failure yako na niseme wazi tangu uwe Mtendaji Mkuu umeharibu reputation ya SSC , umefanya SSC ichukuliwe poa na vitimu kama Yanga vinavyoanza kuchipuka, umekuta SSC ipo ahead of time, umekuta Simba ikiwa ni klabu kubwa sana barani Africa, umekuta Simba imejengwa imara!
Chini yako tulitolewa taifa na Galaxy, chini yako tumekosa hata nusu fainali ya shirikisho na chini yako tumekosa kombe hata la mbuzi, chini yako tumeaibika na ukubwa wetu umeshuka, Chini yako tumefungwa na vitimu kama Yanga mara tatu consecutively, haijawahi kutokea in history, chini yako tumesajilI makocha wa hovyo kuwahi kutokea, chini yako tumekuwa na usajili wa hovyo kuwahi kutokea. JITAFAKARI! kama bado una fit kwenye hiyo position.
Nilisema wazi kuwa CEO wa kampuni inahitaji akili kubwa na technical skills, it was the worst decision ever made kumweka Barba kuwa CEO wa Kampuni, apart from conflict of interest na Mo na kushindwa kuwajibishana baina ya wawili hawa, hana any kind of technical skills kwenye football na ndio maana mnaona scouting za makocha na wachezaji ni NIGHTMARE!
Barba ni mzuri kwenye Marketing na public relation , angepewa hiyo position tangu mwanzo then tukawa na CEO mwenye uelewa mkubwa na mpira, hii ingesaidia sana. Mo achunguzwe kwenye hili.
Ndani ya siku moja tumekuwa na makocha watatu, hii ni faiilure na lack of corporate planning! Inaiondoa SSC kwenye ukubwa wake na ni aibu. Barba akumbuke hii ni timu ya Taifa na Viongozi wakuu wa Nchi akiwemo Samia , Spika wa Bunge, na Jaji Mkuu , hii ni mihimili mitatu ya nchi , hivyo asilete hizi mambo hii ni national klabu na inaweza kuleta machafuko mtaani na kwa vijana na taifa likaingia kwa machafuko.
Way forward ni Barba ajitafakari na ikibidi AJIUZULU HARAKA SANA! Try again AJIUZULU pia. Matola astaafu kiheshima na tuache ujinga kuwa eti matola ndio analeta ushindi viwanja vya mikoani.... hii thinking ni ya HOVYO sana na inaonesha immaturity kwenye soka. Matola apumzike kwa heshima
Barba hii sio timu ya familia, haiwezi kuendeshwa kihuni namna hii. Yaani kumbe hata Juma mlikuwa hamjui kuwa hana cheti, shame!
Barba wewe ni FAILURE!
It is the worst nightmare of all time kwa SSC.