Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
HATUTAKI AKOPE! WALA HATUTAKI TOZO!
Anaandika, Robert Heriel
Nikiwashauri tuvamie mataifa mengine mnaniona Popoma! Mnaona siwezi kufikiri vizuri! Sawa bhana! Ipo siku mtanielewa hata Kwa kuchelewa. Jueni kuwa Taikon hafikirii akiwa ananjaa au akiwa ameshiba. Ninafikiria nikiwa nimetuliza kichwa changu. Sinaga ushabiki Mimi! Wala sina muda wa kupendelea.
Hii nchi hata aje aichukue Malaika kuendelea itahitajika itumie Sera za Uvamizi kivyovyote vile. Iwe Uvamizi wa kiteknolojia, kibiashara, kimichezo, kiburudani, kivita, na mizengwe ya hapa na pale.
Oooh! Anakopa!
Oooh! Nchi itapigwa Mnada!
Oooh! Kazi kuzurura kutembeza Bakuli!
Ndio tunakataa mikopo, tunauweza muziki wa kujitegemea?
Hakuna asiyejua muziki wa kujitegemea hapa.
Kijana aliyemaliza tuu Chuo kikuu licha ya kuwa na maarifa na elimu kubwa lakini mpaka ajitegemee yahitaji kazi ya ziada. Sembuse Nchi.
Kujitegemea inahitaji kukamuana, kupasuana, kuminyana,
Tozo kila mahali!
Tozo kwenye Mdomo, tozo kwenye masikio, tozo puani, tozo machoni tozo kila mahali hayo ndio mambo ya kujitegemea.
Kama nilivyowahi kusema hapo nyuma, Kama tunataka Kupunguza makali ya maisha basi hatuna budi kuvamia Maeneo mengine kivyovyote bila huruma.
Vinginevyo tutaumizana wenyewe Ka wenyewe bila huruma.
Tusipovamia tutavamiwa
Kwani bado Sisi nivipofu? Hatuoni Raia WA kigeni wakija kutamba katika Ardhi yetu wenyewe? Hatuoni!
Hatuoni makampuni Makubwa mengi yanashikiliwa na wageni, Hilo hatuoni?
Hizi tozo na Kodi zitazidi maradufu Kama tusipokaa macho kusuka mipango ya kusaidia wananchi wetu.
Wazungu wanaijua vyema kanuni hii. Wameivamia dunia. Wanatunga sheria Kali zinazowasaidia wao kuvamia mataifa mengine alafu ngumu Kwa wao kuvamiwa.
Uvamizi uwe wimbo wetu!
Uvamizi uwe ndio maono ya viongozi wetu wajao.
Ni rahisi kumkuta Mkenya akiwa hapa TANZANIA akifanya kazi zake Kama Mwalimu, au Daktari, n.k. lakini ni ngumu Kwa Mtanzania kuwa Mwalimu wa Kenya.
Unajua Kwa nini?
Sababu ni mtazamo, falsafa, fikra zetu na wenzetu zipo tofauti.
Tuangalie Wanaijeria, Wahindi, Wachina n.k.
Kama hatutaki Kukopa iweje tukatae Kodi nyingi na tozo hata kama hazina kichwa wala miguu?
Nipumzike sasa mpaka siku Kiongozi mwenye fikra Kama zangu atakapowasili.
Majeshi mbele, wanaume mbele! Popote palipo na fursa tunapiga.
Haramu kwetu hatutumii halali kwao tunawauzia.
Uzia mataifa mengine Bangi ikiwa yanatumia. Kama kwetu ni haramu kwao sio haramu. Hiyo ni fursa. Nini kinazuia.
Mnataka Nani Aamue mambo madogo Kama hayo? Au mpaka Wazungu waseme?
Au labda ni biashara ya watu Fulani wakubwa?
SABATO NJEMA!
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam