Hatutaki longolongo za CCM na Rais Samia

Hatutaki longolongo za CCM na Rais Samia

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
Tume huru ya uchaguzi ndio itamuinua huyu Rais aliyepatikana kwa Mujibu wa katiba iliyopo, na kama kweli waTanzania wamemkubali basi muamuzi ni Tume huru ya uchaguzi isio na doa, lakini haya yanayoendelea ni geresha kwenye mazingahombwe ya CCM.

2025 noma sana, uhakika wa Rais Samia mzanzibari mkaazi ambaae ni Rais wa jamhuri ya Muungano wa TANGANYIKA na ZANZIBAR kupitia muongozo wa katiba na vifungu vyake atakuwa Rais mchaguliwa na wananchi kupitia sanduku la kura, pale tu wananchi watakapojiridhisha upigaji kura ulikuwa tofauti miaka yote iliyopita.

Uchaguzi halali ndio uchaguzi utakaomfanya Rais atembee kifua mbele bila ya hisia ndani ya Moyo wake kuwa sikuchaguliwa kihalali

Tuseme tu na tukubali kama ni Bahati basi Mheshimiwa Samia amepata au ameipata, kwakuwa kipindi hiki ni cha kujijenga kuelekea uchaguzi wa 2025, fursa ambayo wagombea wapya huwa hawaipati.

Kuiteka mioyo ya wapiga kura kwa upande wake ni rahisi sana sana na anachotakiwa aoneshe mapenzi ya dhati kwa wananchi bila ya kuwabagua kikanda, kichama au makabila, masikini au matajiri.

Tume huru ndio itakayomsafisha kama amekubalika au la, lakini kwa kulazimishana kwamba ni yeye tu mkitaka msitake, mbona laana itamuangukia tena ya aibu kuliko waliopita.
 
ford.png
 
Si suala la kufanikiwa ,Tume huru ni lazima wakitaka wasitake au tuvunje vyama vya upinzani tukaivamie CCM mpaka wajue maana ya kikulacho.
Upinzani ungekua na sauti moja, jambo hili lingekua jepesi sana bt tatizo kubwa vyama vingine vinatumika.
 
Tinataka katiba mpya ndani yake ipo tume huru
Ukiingiza katiba mpya kwa sasa japo ni madai yaliyo huru kwa maana yapo pamoja na Tume Huru, miaka mitatu sio mingi tena, umewasikia CCM wakipigana madongo juu ya nani, akina nani wanajipanga 2025, hayo ni yao na kwao imekuwa ni kinyang'anyiro cha kufa mtu, kwa sababu anajua fika akivuka ndani ya chama basi huko mbele ni kweupe, tume polisi majeshi usalama wote wanalinda uchaguzi usiwe wa haki ila uwe wa amani.

Tunaona umuhimu wa Tume MiCCM inafukuzana mchana kweupe bila ya kuoneana haya wala vibaya kwa sababu Tume ya Uchaguzi sio huru, hivyo wanakuwa na magenge ambayo yapo tayari kumzamisha mwenzao au wenzao wanaoweka kiwingu na kutiliana miguu, inakuwa ni pata shika nguo kuchanika, umeyaona yaliyowaka kina Lowasa, Membe na wengineo, yote sababu ni Tume ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania sio huru, kwa vita ya wanaoutaka Uraisi kupitia CCM, kuupata Uraisi ni kuvuka kwenye mchakato wao CCM, baas ukivuka hapo umeshakuwa Raisi na hili lazima ipo siku litawagharimu CCM, watakuja kuuwana ndani ya mkutano wao. Ila hayo ni yao.

Tume Huru ndio kila kitu vyenginevyo bado serikali haitambuliwi na wananchi wake kama ilivyo sasa, ni basi tu wananchi nao wanaenda nayo vile inavyotaka ndio tunayaona tuyaonayo wanafukuzana bila ya kufuata sheria sababu tu Tume huru haipo.
 
CCM ni malaghai wanaotumia ujinga wa Watanzania kutapeli wananchi:

Wakati wa kampeni👇
Baada ya kuingia Ikulu👇🐒
 
Si suala la kufanikiwa ,Tume huru ni lazima wakitaka wasitake au tuvunje vyama vya upinzani tukaivamie CCM mpaka wajue maana ya kikulacho.
Nakumbuka vizuri. USSR ilibibidi wanamageuzi wampandikize Gorbachev ndani ya chama cha kikomunisti cha Urusi. Na alipofanikiwa kukawa na democracy iliyopelekea yale mataifa mengine kujitawala kidemocracy eg Lithuania, Latvia, Georgia etc .

Sasa na hapa hakuna namna ni kupandikiza mamluki ndani yake. Ili democracy iwepo.
 
upinzani ungekua na sauti moja, jambo hili lingekua jepesi sana bt tatizo kubwa vyama vingine vinatumika.
Wanaovitumia ndiyo wenye hivyo vyama.Wapinzani makini utawatambua kwa idadi ya viongozi wao wenye kesi lukuki zinazoitwa za uchochezi,kuzuiliwa kufanya mikutano na maandamano.
 
Wanaovitumia ndiyo wenye hivyo vyama.Wapinzani makini utawatambua kwa idadi ya viongozi wao wenye kesi lukuki zinazoitwa za uchochezi,kuzuiliwa kufanya mikutano na maandamano.
upo sahihi mkuu, bt haya mapandikizi ya vyama ndo yanadhoofisha juhudi za wapinzani wa kweli, mfano juzi kati imeundwa tume kazi ya tume huru, bt waliounda tume ile ni ccm na mamluki wao, haya yote yanafanyika kwa lengo la kudhoofisha madai ya katiba mpya.
 
Kwa sasa hata upinzani nao umeishiwa hoja hawajielewi nao ni wachumia matumbo. Imagine 2025 wagombea ni akina Lipumba, Rungwe, ZZK, Mbowe
 
Kweli Mkuu,ila kelele zetu hazitoenda bure.Angalia idadi ya wana CCM wanaojitambua wanaoongelea haja na umuhimu wa Katiba mpya inavyoongezeka.Pia mwenendo wa kesi ya Mwenyekiti Mbowe inavyowapiga kata funua watesi wetu-wasiojulikana sasa wapo dhahiri.
Big up Mh.Mbowe kwa ujasiri wa kuwapigania Watanzania wenzako kivitendo ukitumia mateso unayolazimika kuyapitia huko magereza.
Uhuru wetu u karibu kupitia mateso yako.
Maumivu ya kunyimwa HAKI ni mabaya kuliko ya msalaba.Tanakuombea kwa Mungu akujalie moyo wa uvumilivu na ulinzi wa Malaika wake.
Aluta continua...
 
Kwa sasa hata upinzani nao umeishiwa hoja hawajielewi nao ni wachumia matumbo. Imagine 2025 wagombea ni akina Lipumba, Rungwe, ZZK, Mbowe
Wewe ndiyo hupanga wagombea toka vyama vya upinzani?Umefahamuje ndiyo hao?Hata hivyo nakuhakikishia ikiwepo Tume Huru ya Uchaguzi hakika Mh.Hashim Rungwe anaishinda CCM.
Hivyo usiwakejeli Watanzania wenzako as if huko CCM kuna malaika na lazima mtawale.Weka fair grounds muone.
 
Kwa kifupi hao tumeishawachoka maana tokea tunaanza mfumo wa vyama vingi ndo wagombea. Kwa kifupi Upinzani hakuna Tz kwa sasa labda 2030 napo mkijipanga vizuri. Imagine Tundu Lisu, Lema walikimbia walisema serikali ya JPM inawatishia usalama haya JPM hayupo mbona hawarudi wanapigia kelele huko
 
Viongozi shupavu ni waliopo nchini wakamatwe wafungwe wahukumiwe ,na kama walikimbia kwa sababu fulani na sababu zinapoondoka inatakiwa warudi haraka iwezekanavyo.

Kukaa nje nchi na kutumia youtube kuzungumza ni uchochezi ,wananchi wanaoonja joto ya jiwe ndani ya nchi hawatakuelewa siku ukisema unarudi eti ugombee uraisi.

na hii michezo ya CCM na Raisi wao ni kutaka kuwaweka wapinzani bize, mara korona,mara ndugai ,mara mawaziri mara spika mpya na wapinzani wote nao wanaungana katika yupi mzuri yupi anafaa huyu ana kasoro zile ,alimuradi wapinzani wanatekwa na kuwa sehemu ya mawazo ya kiccm, huo sio upinzani.

madai ni Tume huru ya Uchaguzi kusiwe na kiunganisho cha mawazo na mambo yanayofanyika CCM hayo ni yao.
 
Kwa sasa hata upinzani nao umeishiwa hoja hawajielewi nao ni wachumia matumbo. Imagine 2025 wagombea ni akina Lipumba, Rungwe, ZZK, Mbowe
Kwani kwenye CCM ukimuondoa Samia nani mwingine anaweza kuwa Rais?Kwani wote waliomo kwenye mfumo tunawajua.
 
Back
Top Bottom