SoC03 Hatutaki mbovu hizo

SoC03 Hatutaki mbovu hizo

Stories of Change - 2023 Competition

Neykapoor

New Member
Joined
Mar 24, 2023
Posts
2
Reaction score
2
Yapata miaka mingi tangu Mzee MBUGI kuwaaidi wananchi wake kuwa atawajengea barabara, madarasa kwa wanafunzi, vituo vya afya na kuzuia vifoo vya mama na mtoto pia Mzee MBUGI alienda mbali zaidi nakusema endapo akipata nafasi ya kuwa mwenyekiti wakijiji atahakikisha serikali inawapa kipaumbele zaidi vijana katika swala Zima la ajira na kujiajiri.

Lakini ahadi zile zilikuwa ni maneno matupu Mara baada ya kupata nafasi ya uenyekiti hakuweza kutimiza hata theruthi ya maneno yake zaidi alionekana kuwa mtu wa kubadili nguo, gari na watoto wake kusoma shule za masafa ya mbali na zenye umaridadi katika lugha za kigeni, ingawaje wananchi wake hawapati huduma staiki katika nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kijamii vilevile vijana wamebaki kuwa wazululaji na mabinti kupata mimba za utotoni mala baada ya kumaliza elimu zao za awali kutokana na kukosa fedha za kuendelea.

Miaka ikaenda na awamu ya pili ya uchaguzi iliwadia na kwawakati huu Mzee MBUGI alikuwa akiwania kiti Cha udiwani na katika nafasi yake alikuwa pamoja na kijana mwenye umri wa miaka 35 ambaye alionekana kuaminiwa zaidi na wananchi wake kwa KIASI kikubwa Sana hali hiyo ilimtisha zaidi Mzee MBUGI kwa kuhofia kukosa nafasi ya udiwani ivyo aliitaji kuwashawishi zaidi wananchi wake.

KAMPENI YA MZEE MBUGI
Manzoshe juu! Manzoshe juu zaidi,
Siitaji kuongea sana maana maneno matupu hayavunji mfupa ndugu Wana manzoshe najua mnaitaji kiongozi bora anayejua Nini maana yauongozi pia mtu mzima maana kichwani mwake ndipo nidhamu na busara ilipo ndugu zangu endapo mtanichagua nakunipa nafasi kwamala ya pili nitahakikisha balabala zinazokwamisha watu kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine hasa nyakati za mvua kuziboresha pia nitahakikisha kwa wale vijanaa wote wanao haribu maisha ya mabinti zetu kuwa kamata na kuwaweka ndani pia nitaandaa mradi utakao shirikisha vijana wote ambao hawana ajira pia kugawa dawa ya maralia kwamama na mtoto pia kuhakikisha zahanati zetu zina vitendea kazi vya kutosha.

Unaweza kujiuliza kwanini naitaji udiwani kwamala ya pili jibu ni ninauzohefu na uongozi takribani miaka mitano pia ninajuana na watu qakubwa serikarini ivyoo ndugu zangu itoshe kusema ninaomba kura Yako kwaajili ya mabadiriko ya Kijiji chetu. ( Sauti ilisikika kutoka sehemu isiyojurikana na kusema)

" HATUTAKI MBOVU HIZO"
Walinzi wa Mzee MBUGI walijitaidi kumtafta mtu mwenye sauti hiyo lakini hawakumpata, hofu kwa Mzee MBUGI ikatanda ivyoo ikambidi achukue hatua mbadara kwa kuwapa rushwa wanakijiji wao akaaanza na walevu akalipia fedha katika kilabu ilikila mlevi apate kunywa pombe ijurikanayo kama dadii kwamdai asuze nafsi yake ,kwa wale vijanaa wanaopenda kucheza mpira akawanunulia jezi pamoja na mpira na kwa mabinti akahakikisha Kila Binti aliyevunja ungo anapata Pedi itakayomsitiri mwezini pia Kila mwanaume wafamilia alipewa zawadi ya shilingi elfu kumi kwaajili ya kuhakikisha upatikanaji wachakula, kitu hicho kikawafanya wanakijiji kufurahi na kusahau machafuko yote na uovu wote alioufanya nyuma Mzee MBUGI na wakamuaidi kura za ndio katika kiti Cha udiwani.

KAMPENI ZA MASHAKA KIJANA WA MIAKA 35
Sina maneno mengi lakini ninajua nyote mnaitaji mabadiriko sitosema Wala sinachakuwapa ilimnichague lakini kumbukeni mbovu za awali tulizo zipata ivyo kwasasa kama mnataka mabadiriko ya kijamii kwamaana uboreshwaji wa zahanati, kuongeza madarasa kwaajili ya wanafunzi, kuruhusu dini zote ziabudu kwa uhuru pia kutengeneza Bomba la kijiji Ilikuepusha ubakwaji wa dada zetu, katika nyanja ya kiuchumi nitahakikisha Kila kijana anajua nini maana ya ubunifu Ili azindue kitu chake kitakacho mpa kipato pia nitahakikisha kwa wale ambao wamesoma kupata usahili wa haki juu yanafasi za ajira katika Kijiji chetu pia nitaanzisha mfumo utakao saidia mabinti zetu namna ya kujitambua na kujithamini wao kama vijana, katika nyanja ya kisiasa ninaaidi kuwa kiongozi bora nitake fata katiba, haki na usawa na kufuata kanuni zote zilizopo katika kiti changu Cha udiwani.

Sina maneno mengi ya kusema ilaitoshe kusema kama unaitaji mabadiriko na unasema "HATUTAKI MBOVU HIZO" chagua mashaka lakini kama mnataka kuendelea kuwa na mbovu msinichague.

Basi muda wa kampeni ulipita na wananchi wakaanza kujadili kati ya mashaka na Mzee MBUGI ni nani kiongozi bora lakini wananchi wapendao mabadiriko waliendelea kisisitiza na kusema kama Mzee MBUGI nafasi ya uenyekiti wa Kijiji ulimshinda jee nafasi ya udiwani ataweza kweli lakini vibaraka wa Mzee MBUGI waliendela kushawishi na kusema ilikuwa ni uenyekiti tujaribu udiwani tuone atafanya Nini.

Mzee MBUGI aliendelea kutoa rushwa lakini siku ya uchaguzi asilimia aabini na Tano ya wanakijiji Cha manzoshe waliungana na kusema " HATUTAKI MBOVU HIZO" na kumchagua mashaka lakini asilimia ishirini na Tano walimuitaji Mzee MBUGI, hivyo kutokana na watu wengi walimchagua Mashaka, na Mashaka akawa diwani wa Kijiji Cha manzoshe kama alivyoahidi ndivyo akatekeleza na akasaidia katika kuzuia vifoo vya mama na mtoto pia watoto wote walienda shule kwasababu aliongeza Madarasa na akataifisha mali zote za Mzee MBUGI ambazo alikuwa akitumia fedha za wanakijiji kwa pamoja na umoja wanakijiji wakasema ilitulate mabadiriko nilazima mtu mpya apatikane hatutokubali mbovu hata siku moja.
 
Upvote 3
Tusubirie majaji mkuu naona awamu hii watu hawapigi kura kabisa sijui kwa nini
 
Back
Top Bottom