PreGE2025 Hatutakubali Tena Kuishi kwa Hofu – Kukosoa Siyo Uasi, Ni Uzalendo wa Kweli!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

UHURUWANGU

Member
Joined
Mar 11, 2025
Posts
54
Reaction score
85
Tunaomba Nini? Si Miujiza – Ni Mambo ya Msingi:

1. Katiba Mpya – Ili tuwe na msingi wa haki kwa wote, si kwa wachache.

2. Tume Huru ya Uchaguzi – Ili kura iwe na maana, na si maigizo ya ushindi wa lazima.

3. Uhuru wa Kujieleza na Kushiriki Kisiasa – Ili kila sauti ihesabiwe, si kuzimwa.

4. Haki kwa Waliodhulumiwa – Waliopoteza ndugu, kazi, au uhuru wao kwa kudai haki, waachiwe na kufidiwa.

---

NO REFORM, NO ELECTION – Sio Kauli ya Hofu, Ni Sauti ya Ukombozi!

NO REFORM, NO ELECTION – Haki Haiombwi, Inadaiwa!
 
Sijasikia sera yoyote ile mbadala na za CCM kutokea CHADEMA.

Itoshe, sitakubali Mtu au Watu na makundi mengine ya Siasa kuingilia haki yangu ya kikatiba kupiga kura. Yani nitafanya kila niliwezalo kuhakikisha napiga kura.

Na kwa msing huo, ikifika Octoba 2025 naenda kukipigia kura chama chechote kilicho na sera mbadala na za CCM, tambua CHADEMA haina sera, haijawahi kuwa na sera dhamira ama nia ya kuwa nazo, na hivyo basi haitokuwa CHADEMA.

...yaani ikishindikana kabisa kupatikana chama chenye sera mbadala na za CCM, itanibidi tu kuwapigia kura CCM-Bora mara 100 badala ya kupiga kura za huruma na hasira kwenda kwenye chama cha waasi magaidi na wahaini.
 
Wengine hiyo haki mtaikuta kaburini
 
Una akili sn
 
🔥🔥🔥👉💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐💐🌻🌻🌻🌻💐🌻💐🌻🌻💐💐💐💐💐💐🌻🌻🌻
 
Mhubiri 3:1
Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.

Maana rahisi - KIla jambo na wakati wake. => Huu ni wakati wa No Reforms No Election

Tukimaliza na kufanikisha hili utajua Chadema ni mabingwa namna gani kuandaa sera za kulikomboa Taifa

Huwezi kuangaika na sera wakati msingi ambao ni uchaguzi umeharibiwa.

Chadema imeamua kujenga msingi. Msingi ukiwa sahihi vingine vyote vinaleta maana
 
HAKI AIOMBWI, INADAIWA.

Hapo ktk kudai hiyo haki, ni kwa namna ipi na nan wa kudai
 
Mhubiri 3:1
Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.

Maana rahisi - KIla jambo na wakati wake. => Huu ni wakati wa No Reforms No Election

Tukimaliza na kufanikisha hili utajua Chadema ni mabingwa namna gani kuandaa sera za kulikomboa Taifa

Huwezi kuangaika na sera wakati msingi ambao ni uchaguzi umeharibiwa.

Chadema imeamua kujenga msingi. Msingi ukiwa sahihi vingine vyote vinaleta maana
Majibu mazuri, walakin

CHADEMA imeamua kujenga msingi au kubomoa msingi?

...yani kama ninaweza kuweka tafsiri ya majibu yako, unakubali CHADEMA haina sera, kwamba inataka kushika madaraka tu tena kwa nguvu sasa na madaraka hayo ni Uraisi tu ndio ije iandike sera?

Mhubiri haukukosewa mkuu. NRNE ndio imekosewa na sasa sio wakati wake;

Kama mwananchi katiba imeshanipa nguvu na haki yangu ya kupiga kura.

Na mwaka huu, ndio wakati muafaka kulingana na Mhubiri 3:1

Sintokubali CHADEMA ije inipokonye haki hio kwa sababu ya kuwafurahisha watu wachache, namely watendaji wakuu wa CHADEMA eti kwasababu ya No Reforms No Elections.
Kama wao hawatashiriki sawa, ila wasinizuie mie kwenda kupiga kura.
 
Wakati fulani changamoto ya kukubalika au kukataliwa kwa hoja inabaki katika uungwana.

Naweza kukubaliana nawewe kwamba sera za chadema kwa wakati huu inawezekana bado hazijawa wazi naomba nitoe sababu

1. Chadema sio chama kichanga kimeshiriki, kimeshinda na kimeshindwa mara nyingi. Huenda kwa mtazamo wao kuwa na sera nzuri au mbaya sio sababu ya kushinda kwani kura ya mwananchi haithaminiwi.

2. Kuwa na sera nzuri bila utaratibu wa haki wa kuchagua ni upumbavu kwani box la kura halieshimiwi.

3. Wamechagua kutoweka sera wazi ili nguvu kubwa iwekwe kwenye kudai madaliko ya usimamizi wa uchaguzi.

Mwisho kama pakiwa na mazingira huru na haki ya kuendesha uchaguzi basi mwananchi atapima yupo mwenye sera bora na yupi hafai ivyo sioni kwanini unakuwa na mashaka na kura yako.

Ukiangalia mnufaika mkubwa wa mapambano ya chadema ni mwananchi ili maamuzi yaheshimiwe.

Zipige rungu hizi hoja kama unazipinga
 
Sijasikia sera yoyote ile mbadala na za CCM kutokea CHADEMA.

Itoshe, sitakubali Mtu au Watu na makundi mengine ya Siasa kuingilia haki yangu ya kikatiba kupiga kura. Yani nitafanya kila niliwezalo kuhakikisha napiga kura.

Na kwa msing huo, ikifika Octoba 2025 naenda kukipigia kura chama chechote kilicho na sera mbadala na za CCM, tambua CHADEMA haina sera, haijawahi kuwa na sera dhamira ama nia ya kuwa nazo, na hivyo basi haitokuwa CHADEMA.

...yaani ikishindikana kabisa kupatikana chama chenye sera mbadala na za CCM, itanibidi tu kuwapigia kura CCM-Bora mara 100 badala ya kupiga kura za huruma na hasira kwenda kwenye chama cha waasi magaidi na wahaini.

Asante kwa maoni yako, lakini naomba tuweke mambo sawa kwa misingi ya hoja na si mihemko.

Kwanza, kusema CHADEMA haina sera ni upotoshaji wa wazi. CHADEMA ina ilani rasmi ya uchaguzi, yenye sera nyingi zilizochapishwa na kujadiliwa kwenye majukwaa mbalimbali—kuanzia elimu bure yenye ubora, huduma bora za afya kwa wote, uwezeshaji wa vijana na wanawake kiuchumi, mabadiliko ya mfumo wa kodi, haki kwa wakulima na wafanyakazi, hadi kwenye mageuzi ya mfumo wa utawala wa nchi kwa kupitia Katiba Mpya. Kama hujaziona, basi ni jambo la kutafuta taarifa zaidi, siyo kukana kilicho wazi.

Pili, hoja ya kudai kuwa una haki ya kupiga kura ni ya kweli kabisa—na CHADEMA wala NO REFORM, NO ELECTION haipingi haki yako ya kupiga kura. Inachosema ni tusifanye uchaguzi wa maigizo tena, ambao hatma yake inajulikana hata kabla ya kupiga kura. Haki ya kupiga kura haimaanishi kitu kama mazingira ya uchaguzi ni ya dhuluma, ya hila, na tume siyo huru.

NO REFORM, NO ELECTION siyo wito wa kuchochea vurugu—bali ni wito wa kufanya marekebisho ya msingi kwenye mfumo mzima wa uchaguzi ili kura yako, yangu na ya kila Mtanzania iwe na maana halisi. Bila tume huru, bila sheria ya uchaguzi ya haki, bila katiba mpya, ni sawa na kushiriki michezo ya kupoteza muda kwa jina la demokrasia.

Na kuhusu kudai CHADEMA ni chama cha “waasi” au “magaidi”, hiyo ni lugha inayotumiwa kufunika hoja kwa kejeli—lakini haina msingi wowote wa kisheria wala kihistoria. CHADEMA imepigania haki kwa njia ya amani tangu ilipoanzishwa. Kama ingetumia njia za kihalifu, isingekuwepo hata leo—wala viongozi wake wangekuwa uraiani. Kuipinga serikali si uhaini. Ni haki ya kikatiba.

Kwa hiyo ndugu, kama kweli unathamini haki yako ya kupiga kura, basi unapaswa pia kuunga mkono marekebisho ya mfumo ili kura hiyo ihesabiwe kwa haki. Ndivyo demokrasia inavyolindwa—si kwa kushiriki kila uchaguzi hata kama ni wa kitapeli, bali kwa kupigania mazingira huru na ya haki.

Tusifanye maamuzi kwa jazba au chuki—tufanye kwa tafakuri, uchambuzi na kwa fikra huru.
 
Tunaomba Nini? Si Miujiza – Ni Mambo ya Msingi:

1. Katiba Mpya – Ili tuwe na msingi wa haki kwa wote, si kwa wachache.

2. Tume Huru ya Uchaguzi – Ili kura iwe na maana, na si maigizo ya ushindi wa lazima.

3. Uhuru wa Kujieleza na Kushiriki Kisiasa – Ili kila sauti ihesabiwe, si kuzimwa.

4. Haki kwa Waliodhulumiwa – Waliopoteza ndugu, kazi, au uhuru wao kwa kudai haki, waachiwe na kufidiwa.

---

NO REFORM, NO ELECTION – Sio Kauli ya Hofu, Ni Sauti ya Ukombozi!

NO REFORM, NO ELECTION – Haki Haiombwi, Inadaiwa!
Tatizo kujiamin kwenu kupo huku kwenye mitandao hapo ndipo huwa nashindwa kuelewa kwanini tulinyimwa ujasiri ?
 
Tunaomba Nini? Si Miujiza – Ni Mambo ya Msingi:

1. Katiba Mpya – Ili tuwe na msingi wa haki kwa wote, si kwa wachache.

2. Tume Huru ya Uchaguzi – Ili kura iwe na maana, na si maigizo ya ushindi wa lazima.

3. Uhuru wa Kujieleza na Kushiriki Kisiasa – Ili kila sauti ihesabiwe, si kuzimwa.

4. Haki kwa Waliodhulumiwa – Waliopoteza ndugu, kazi, au uhuru wao kwa kudai haki, waachiwe na kufidiwa.

---

NO REFORM, NO ELECTION – Sio Kauli ya Hofu, Ni Sauti ya Ukombozi!

NO REFORM, NO ELECTION – Haki Haiombwi, Inadaiwa!

Maneno mazuri na murua kabisa.

Chapisheni vipeperushi muwasambazie watu na kuvigawa kwenye mikutano ya Chadema cc. Erythrocyte.
 
Sijasikia sera yoyote ile mbadala na za CCM kutokea CHADEMA.

Itoshe, sitakubali Mtu au Watu na makundi mengine ya Siasa kuingilia haki yangu ya kikatiba kupiga kura. Yani nitafanya kila niliwezalo kuhakikisha napiga kura.

Na kwa msing huo, ikifika Octoba 2025 naenda kukipigia kura chama chechote kilicho na sera mbadala na za CCM, tambua CHADEMA haina sera, haijawahi kuwa na sera dhamira ama nia ya kuwa nazo, na hivyo basi haitokuwa CHADEMA.

...yaani ikishindikana kabisa kupatikana chama chenye sera mbadala na za CCM, itanibidi tu kuwapigia kura CCM-Bora mara 100 badala ya kupiga kura za huruma na hasira kwenda kwenye chama cha waasi magaidi na wahaini.
Umeelewa kilicho andikwa hapo juu na ulichojibu ndugu? Kuna mahali popote pameandikwa SERA HAPO JUU?
SERA AU KUŔA YAKO INA MAANA GANI KAMA CCM WANAIBA KURA NA KUSOKOMEZA KURA ZILIZOKWISHA PIGWA TAYARI KWENYE MABOX YA KURA?
 
Sijasikia sera yoyote ile mbadala na za CCM kutokea CHADEMA.

Itoshe, sitakubali Mtu au Watu na makundi mengine ya Siasa kuingilia haki yangu ya kikatiba kupiga kura. Yani nitafanya kila niliwezalo kuhakikisha napiga kura.

Na kwa msing huo, ikifika Octoba 2025 naenda kukipigia kura chama chechote kilicho na sera mbadala na za CCM, tambua CHADEMA haina sera, haijawahi kuwa na sera dhamira ama nia ya kuwa nazo, na hivyo basi haitokuwa CHADEMA.

...yaani ikishindikana kabisa kupatikana chama chenye sera mbadala na za CCM, itanibidi tu kuwapigia kura CCM-Bora mara 100 badala ya kupiga kura za huruma na hasira kwenda kwenye chama cha waasi magaidi na wahaini.
Watu wenye akili kubwa kama wewe wanazidi kupungua JF. Badala yake watu wanaoshabikia uasi kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano, ambao hufikri kinyumbu nyumbu wanazidi kuongezeka. Bahati nzuri mambo ya hovyo yanayofanywa na chadomo yanawazindua wengi wao.
 
Back
Top Bottom