Hatutarajii Kuona Mabango ya Wanasiasa kwenye Simba/Yanga Day, TFF na Polisi liangaloeni hili kwa Umakini

Hatutarajii Kuona Mabango ya Wanasiasa kwenye Simba/Yanga Day, TFF na Polisi liangaloeni hili kwa Umakini

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Kwenye Michezo, ikiwemo soka ndiyo sehemu pekee wanapokutana watu wa Itikadi Tofauti, wanaweza kuwa Chama kimoja cha Siasa lakini wakakutana uwanjani wakiwa Timu tofauti, Na waweza kuwa Mahasimu kisiasa lakini wakawa wanashabikia timu moja. Hii ni kwa sababu Michezo haihusiani na Siasa wala vyama vya kisiasa.

Ili kulinda Mambo haya hatutegemei kabisa kuona Mabango ya Wanasiasa kwenye Tamasha la Simba Day wala lile la Wiki ya Mwananchi, kwa sababu, kufanya hivyo kunaweza kusababisha vurugu kutoka kwa pande tofauti za kisiasa kunakoweza kusababisha Maafa.

Kuna Maeneo mengi mno ya kubandika mabango ya Wanasiasa, zikiwemo ofisi za vyama vyao na kwenye mabango ya kulipia yaliyojaa kila mahali, ama hata kwenye nyumba binafsi ya ambaye amependa kuweka bango la Mwanasiasa amtakaye.

Natoa Wito kwa Mamlaka kuzuia Upuuzi wa Kubeba Mabango yenye picha za wanasiasa kwenye matamasha haya ili kulinda amani.

Kama unampenda mtu kwa sababu ya sura yake basi nenda kanywe naye chai- JK Nyerere
Soma pia:
SIMBA DAY 2024: Simba SC vs APR | Mkapa Stadium | 03/08/2024
 
Ni uhuru wa mtu
Acha watu wafanye wanachotaka
 
Picha linaanza kwenye yale mabango ya uwanjani Bango ni kubwa
 
Uhuru wa kisiasa ni haki yao usilete fikra za kidikteta hapa kama mbowe anavyong'ang'ania uwenyekiti wa chama
 
Simba na Yanga ni timu za serikali ya CCM,viongozi ni CCM na wawekezaji ni CCM, kama hutaki amia Burundi.
 
Back
Top Bottom