Hatuwezi kuendelea kuilaumu Kenya na Mabeberu kwa matatizo binafsi ya Tanzania: 'We are paying the price of our own Wrongdoings!'

Excellent analysis Nantoombe! Waswahili walisema "kikulacho ki nguoni mwako".
 
Kulikuwepo na jamaa anaitwa Kalamu, halafu akapotea. Alikuwa yuko vizuri sana...Sasa ndipo akaja huyu Kalamu1, sidhani kama ndiye yule yule.
Yaah namkumbuka yule member alikuwa objective sana, huyu Kalamu1 atakuwa imposter.. Yule member Kalamu wa ukweli kwanza alikuwa sana mahiri wa kuandika
 
Nafikiri sasa ipo haja ya nchi kuwa na sera 1 yamaendeleo... Hapo kwenye katiba nakubaliana na wewe kabisa Mushi!!! Hii inchi viongozi wanaturudisha nyuma sana kwakueleana.... Naomba niulize ivi ni nchi zote duniani zinawajengea maraisi nyumba zakuishi kwakutumia pesa nyingi za walipa kodi??? Nyumba 1 milioni mia5.... Kwa katiba hii ni ngumu sana kutoboa!!! Tuna ardhi yakutosha sana serikali iwekeze uko tuwe na kilimo chenye Tija na cha kibiashara tuweze kutoka hapa tulipo... Sioni kama kina njia yakututoa zaidi ya kilimo na viwanda... Mama Samia!! Mh Raisi uwe unapita uku kusoma soma turudi kwenye viwanda na kilimo tutatoka.... Asante sana mkui Mushi kwa elimu uliyotupa ya bure
 
Mfumo wa ujamaa umefanya mtu kuwa masikini kuonekana ni sifa njema.
LOooo!
Hii umeipata wapi mkuu Naantombe Mushi. Mbona sijawahi kuisikia?
Niliahidi kurudi, sasa wakati naingia tu nikakutana na hii kabla sijaenda kule kwenye mada yenyewe.

Una maana gani na huu mstari wako mmoja.

Lakini siyo neno, ngoja niende nikakusome vizuri.
 
N. Mushi umemaliza kila kitu. Ipo sababu ya kihistoria ambayo ni kupndoka kwa mkoloni mapema Tanganyika kulileta attitude ya watu kuwa slow, unaccountable yaani kila mwanaanchi hataki kuchukua majukumu yake anabaki mtu wa lawama tuu hii ni dalili ya uvivu. Mpaka raisi naye analalamika badala ya kutake charge.

Uwazi na uwajibikaji, mfumo ulio hafifu wa elimu juzi kaonekana Secretary of state anahutubia bungeni anaongea kama anakimbizwa, hajiamini matatizo ya elimu yetu ya kupata gpa kubwa ili hali critical thinking hakuna kichwani.

Tuna kazi kubwa sana kama Taifa .
 
Mkuu Naantombe Mushi,

Kwanza nikupongeze kwa jitihada za kufanya jambo kiutaratibu; nikiwa na maana umejiandaa kuifanya kazi na kuiwasilisha.

Kazi yetu wapokeaji, ni kukusoma kwa uangalifu na kukuelewa, halafu tujadili uliyowasilisha.

Sasa nimelipitia kwa mara ya kwanza andiko lako lote; pamoja na usomaji wangu wa harakaharaka, sitajibu niliyosoma kwa sasa, ngoja niyakalie kidogo na nitasoma tena mara ya pili.
Kufanya hivyo kutanipa uhakika wa kujibu baadhi ya ambayo nimeyaona na sikukubaliana nayo.

Wakati nikiweka ahadi ya kulijadili andiko lako, naomba kama itawezekana, utoe vyanzo uli[opata hizo 'charts' zinazoambatana na andiko lenyewe.

Hongera kwa jitihada zako za kuwasilisha uchambuzi ulioufanyia kazi.
 
Ili tuweze kushindana vyema na nchi za wenzetu watanzania tuache kwanza kuwa:
(i) waoga wa wageni
(ii) wasiojiamini
(iii) wenye husuda na chuki na watu waliofanikiwa kimaisha/kibiashara
(iv) wenye ubaguzi kwa misingi ya chama cha siasa -wenye nchi a.k.a wazalendo vs wapinzani,
(v) wenye kupeana vyeo kwa misingi ya ufuasi wa chama na nasaba na viongozi wa chama walio madarakani na wastaafu.
(v) wapenda majungu na habari za udaku
(vi) wategemezi - hata ujenzi wa vyoo vya watoto wao shuleni wanasubiri serikali
(vii) ombaomba kila kitu hata kama ni haki yao ya msingi ya kikatiba wanaomba badala ya kudai
(viii) wavivu etc.
(ix) wadokozi wenye kupenda utajiri wa dili
NK.

Nadhani ile siasa yetu pendwa imechangia sana kwani wengine tuliisoma tangu primary mpaka secondary.
 
Kuwa na Dira ya maendeleo ni kitu ambacho ni cha umuhimu sana, ila pia lazima kuwe na marekebisho ya sheria ambazo mimi ndo nnaziona zinaathiri shughuli za kiuchumi.

Kwa nyongeza hata hawa viongozi ni lazima wabadilishe fikra zao kuhusu ideology haswa ya kuendesha huu uchumi

Ni kama ukisikiliza viongozi wetu bado wapo kwenye usingizi wa ujamaa
 
Kwani inatofauti gani na Magufuli akiwa anajiita mtetezi wa wanyonge.. ni mentality tu hiyo.. unafikiri ni kwanini Magufuli hakuwahi kusema yeye ni mtetezi wa matajiri ambao ndo wanaajiri hawa wanyonge???

Unauliza vitu ambavyo vipo wazi kabisa
 
Unajua Chief kuna nchi ambazo miaka 60 iliyopita tulikuwa on the same level economically. Nikimaanisha kwamba hata kama wakoloni waliondoka mapema, bado miaka 60 ni mingi sana kwa nchi kufanya turn around.

-----Kuna kitu umegusia kuhusu elimu ni sawa kabisa, huu mfumo wa elimu ni kweli hautuandai watanzania ku explore the world, ni mfumo ambao una suit zaidi nchi yenye closed economy.. yaani nchi isiyo na mahusiano na nchi nyingine.

-----Pia kuna issue ya wrong ideology ya ujamaa, hii ndo laana na majanga ya hii nchi.

--------Hizi point mbili hapo juu, ukijumlisha na ulafi wa madaraka wa chama dola CCM, ndo umekuwa ni sababu ya hii nchi kuendelea kukumbatia sera mbovu, katiba mbovu, na kukosekana kwa Democracy.
 
Ingia kwenye website ya data.worldbank utapata data zote nilizotumia. Mkuu najua hatufahamiani, ila mimi labda nisema uongo kwenye maandishi ila sio takwimu.

Takwimu zangu nachukua kwenye credible sources.

Sina motive yoyote ya kutoa takwimu hewa
 
Ni kweli kabisa, na kitu kikubwa cha kwanza cha kufanya ni kubadili mfumo wa elimu uwafanye watu wajiamini.

Tukifanikiwa hapo, Tanzania itakuwa sio hii unayoiona.

Mi siamini eti watanzania ni wajinga eti kwamba wakenya ni bora kuliko sisi.. tatizo kubwa ni kwamba watanzania tunaonekana wajinga kwasababu kuna mfumo kandamizi ambao unafanya akili za watu zinapata uvivu wa kufikiri.

Hivo yani, ukiondoa hii mifumo kandamizi, ya kielimu na sheria.. watanzania tutakuwa juu sana.. hicho naamini kabisa
 
Uzi mzuri, nimejifunza mengi, asante.
Watanzania ujamaa umetuharibu. Kweli!
Hatutaki competition, tunategemea serikali itusaidie kwa kuzuia competitors.
Ingependeza tungepambana, ili serikali ituboreshee mazingira kielimu na kisera ili tuweze kumudu ushindani.

Tuna serikali inayotumia dola kutawala, tumejaa nidhamu za uoga na unafiki.
Ndiyo maana tunapata mtu mmoja n.a. kikundi chake cha wachache. anauaminisha umma wa watz kuwa maskini ni uzalendo, na watz kama makondoo wanashabikia.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…