Hatuwezi kuendelea kuilaumu Kenya na Mabeberu kwa matatizo binafsi ya Tanzania: 'We are paying the price of our own Wrongdoings!'

Unapozungumzia uchumi na kukuza uchumi hautakaa ukwepe namna fulani ya kukuza uchumi. Ndo mana kwenye theories za development, unaona mifano mingi inatoka Asian Tigers, na hata kuna nchi za sasa huwa wana borrow strategies zilizofanywa na Asian Tigers.

So nikukosoe kwanza, kwenye uchumi ni lazima uangalie mwenzako anafanya nini na wewe unafanya nini, na wewe amefanikiwa vip.. Ndo maana kuna kitu tunaita economic intelligence. Huwez ukasema eti hatutakiwi kufananisha.. utakuwa unakosea sana.. unless wewe utakuwa haufahamu haswa kuhusu masuala ya kiuchumi.
 
Ume mention Ethiopia na Somalia kwamba wengi wanaishi nje ya nchi, lakini umesahau kueleza ni kwanini wengi wapo nje ya nchi zao..

Kuna issue ya political instability kwa Somalia na hata Ethiopia, halafu kuna issue za baa la njaa, kwa hiyo hata ukichunguza wengi wa wa ethiopia na wa somalia walio nje ya nchi zao, hawa walikuwa granted hati ya ukimbizi.

Kwahiyo mpaka hapa, hakuna relevance ya unachotaka kukicommunicate.

Halafu naona una downplay role ya remittances flow.. itakuwa huelewi vema umuhimu wa remittances. Na kama huelewi hautakiwi uendelee kubishana kwa kitu ambacho hukifahamu. Nenda kakisome ndo uje tueleweshane vema
 
Umeandika sana sana na umeonesha namna Kenya imefanya tena kwa kiwango na mifano na hapa tuna safari ndefu sana kwetu,

Kizazi cha Mkapa Na JK kilipaswa kuandaliwa kama wenzetu Kenya wana vizazi vinavotaka Urais vyenye maono ya Kiuchumi wa sasa duniani.
 
Kwanini Aliko Dangote alishindwa kuwekeza kenya?

Kwanini Rostam Aziz alishindwa kuwekeza kenya upande wa gesi?

Bakhresa aliomba awekeze kenya na hawakumpa nafasi

CRDB waliomba kuwekeza na walinyimwa fursa

Sasa wakenya kwenye maendeleo yao wanavuna $ ngapi kwa makampuni 500 yaliyopo Tanzania?

Kenya wanajua hili wakiweka mazingingira rafiki kwa Tanzania kuingia kuwekeza kenya, nchi yetu itavuna $ za kutosha

Ni kweli wapo juu kiuchumi kwanini hakuna double standard kwenye uwekezaji ingali ni nchi majirani?

Inaumiza Sana Rudi kaangalie YouTube ya Rostam Aziz alivyoongea kwa niaba ya wafanyabiashra kutoka Tanzania

Bado wanaitaka gesi yetu iende kwao kenya ili nao waruhusu mahindi ya Tanzanian yauzwe kenya[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]

Faida watakayoipata kenya wakiuza gesi iliyotoka Tanzania utakuja kutuambia kenya wako vizuri kuliko Tanzania kiuchumi
 

..Rostam amechuma hapa Tanzania halafu anataka kwenda kuwekeza Kenya.

..Mimi nimefurahi Rostam alivyonyimwa kuwekeza Kenya.

..badala ya kutengeneza ajira hapa Tanzania, Rostam anataka kwenda kutengeza ajira Kenya?!

..Hayo mabilioni angeyawekeza hapahapa Tanzania ambapo ndipo palipompa utajiri.

..Rostam Aziz anapaswa kuwa mza-RENDO.
 

..kuna waraka unaitwa " tanzania vision 2025 " ambao uliandaliwa wakati wa Mzee Mkapa.

..sina uhakika kwa kiasi gani Kikwete na Magufuli walisimamia utekelezaji wa waraka huo.
 
Kukuza uchumi wa nchi hakuhitaji rocket science aisee...nikuongeza production period...sasa Tanzania tuna produce nini yarabi..ni hayo mahindi tunayoombea soko Kenya..

Tunatafuta watu nje waje kuwekeza which is fine...terms za mikataba ni siri...watanzania wapole sana hatuna shida tunaimani na viongozi wetu...ninaamini hakuna mfanyabiashara anaetaka kuwekeza asietaka apate faida zaidi...akija kiongozi akituambia jamani tunaibiwa mikataba mibovu..km uwekezaji hauna tija kwa nchi yangu sepeni mnasema ditekta anafukuza wawekezaji...mikataba mibovu maana yake nini muwekezaji anazalisha anachukua noti sisi tunabaki na coin..na unakuja kuambiwa hizo coin asilimia kubwa inaishia kwa wachache...

Haya sasa tunafungua nchi watu waje kuwekeza kwa terms zipi...na tunavyoomba kwa kupiga magoti nina shaka km tutaweza kuchallenge terms zao...msione watu wanalalamika, viongozi wenyewe ndio wanatuchanganya...Upinzani ajenda yao kubwa bungeni ilikuwa mikataba mibovu...sasa hv kiko wapi...

Tumlaumu nani
 

Mkuu,this is a thread of the year!!! Nimesoma hoja zako zote pamoja na jinsi unavyojibu kina "walee" nikagundua,WEWE NI NGULI na unautashi wa kutosha kwenye uandishi,uwasilishaji na ujenzi wa hoja. KONGOLE YAKHE.

Pili,labda nitupie wazo langu hapa. Binafsi nadhani elimu mbovu ndio imetufikisha hapa. Hadi Karne hii yupo mbunge bungeni ambaye ni darasa la Saba! SAMAHANI,darasa la nne!!! Cha kushangaza,kamati ya chama eti iliwapitisha kisa ni hodari wa kubwabwaja matusi na upyoro wa lugha chafu pindi wanapojibu hoja za wapinzani😂😂😂😂

Papa,we can never compete with a country whose lawmakers in the assembly a chosen by the people on the ground of credibility, intelligence and academics. For instance,for anybody to become a senator in Kenya,must have at least masters from a recognized public institution and not those fetched from the streets of Delhi, India!!! While a member of parliament should at least be a degree holder...!!! Tunaanzaje sasa ushindani???

Tatu,tunaanzaje ushindani na watu ambao si waoga kudai haki yao? Mkuu,kumbuka nchi ile kiongozi wa upinzani anazunguka na rais kuzindua miradi ilhali huku mpinzani anatakiwa atolewe kafara ili viuongo vyake na damu vitumike kuisokota hirizi ya Muungano ili isipoteze uhalali???

Tunaanzaje kushindana na taifa ambazo ili uchaguliwe kuwa CEO,CHIEF JUSTICE,POLICE COMMISSIONER etc lazima ufanyiwe public vetting tofauti na huku kwetu ambapo kamishna wa polisi sharti awe mbabe mwenye alama nyingi usoni zinazoashiria makovu yaliyomkuta katika medani ya mapambano au uwe na sura ngumu inayoweza kutisha maandamano ya wapinzani!!!

Tunaanzaje ushindani na nchi amabayo inaamini katika ushindani wa kielimu ilhali sisi tumewekeza katika kushawishi waganga wa jadi kwamba tuko pamoja nao na tunaendelea kutetea haki zao!!! Kenya mabango ya kuonyesha taasisi zinazotoa elimu ya juu ni mengi sawa na yale yanayoonyesha wasafisha nyota,warefusha uume,warudisha wapenzi,wauza Pete za bahati Tanzania!!! Dadeki!!!

Tunaanzaje ushindani na nchi ambayo ili uwe askari angalau uwe na elimu ya form four ilhali huku kwetu Bongo kigezo ni uwe mwana green brigade au la,wazazi wako wawe wastaafu wa jeshi au walau wanafahamiana na washika dau.!!! Tunaanzaje Mushi huu ushindani kakaangu?

Tunaanzaje ushindani na wakenya ambao ili uonekane smart ni kichwani uwe vizuri ilhali huku kwetu kijana smart ni anae miliki I.S.T au Kama ni mwanamke,awe na makalio makubwa ambayo akipita karibu na wewe unaitika "naam"hususan Kama unaitwa Paul maana yanapiga kelele "poo,poo,poo"apitapo. Kenya mdada anahangaika na mafaili ya vyetu ilhali huku kwetu wadada ni kubusti maziwa na kuhangaika kuyarudisha kwenye brezia kila Mara gari linapogonga bampsi!!!

Viongozi wakenya huwa wanajadili masuala ya kitaifa hususan wawapo bungeni,sisi wakwetu huwa wanajadili vyama kila Leo na kutaka wananchi wamseme na kumsoma kwenye magazeti. Uhuru Kenyatta anasifika kila kina ilhali Magufuli anasifika kwenye zilizokiki za Milad Ayo!!! What a stoke!!!

Wakenya wamewekeza sana kwenye ujasusi wa kiuchumi,kisera na hata kisisasa. Maraisi wao huwandalia mapema sana kiasi kwamba unaweza kupredict huku kwetu raisi anadeveop political pressure kwa kupitishwa kuiongoza nchi bila kutegemea au kuota! Afu anasema hadharani,"Mimi SI mwanasiasa" ila bado Wana wa ujamaa wanamshangilia na kumpamba kwa nyodo na mikogo afu tuanze kushindana na wakenya!!!

Kaka Nina mengi ila tayari hasira zimenipanda naomba nisiendelee. Nikichokozwa na "wale" nitarejea......ila tukitaka kubadili upepo na kuwa kimbiza wakenya,TUWEKEZE KWENYE ELIMU YENYE TIJA. SI HII YA "WANYONGE"
 

Pitia post yangu tena, ili uelewe ni kwa nini nilikubishia kwamba sababu ya wakenya kwa kiasi fulani kutoka nje ni nini!!? Wewe ulikazia sana kiingereza (🤣🤣🤣)
 
Leo tarehe 03/06/2021 wametua matajiri wakubwa wawili kutoka Marekani kuja kuwekeza TZ .
Wamepokelewa na viongozi wetu!

Inaonesha mama yupo serious na falsafa yake ya uwekezaji...?
Source: clouds media
 
Leo tarehe 03/06/2021 wametua matajiri wakubwa wawili kutoka Marekani kuja kuwekeza TZ .
Wamepokelewa na viongozi wetu!

Inaonesha mama yupo serious na falsafa yake ya uwekezaji...?
Source: clouds media
Ndo tunataka mambo kama haya sasa
 
Pamoja sana mkuu... umemwaga point nzito na wewe ngoja nizipitie taratibu
 
..kuna waraka unaitwa " tanzania vision 2025 " ambao uliandaliwa wakati wa Mzee Mkapa.

..sina uhakika kwa kiasi gani Kikwete na Magufuli walisimamia utekelezaji wa waraka huo.
Shida ni kwamba Tanzania hakuna dira ambayo ipo constant kila Rais anakuja na dira yake na mipango yake, ndo makosa huanzia hapo.. but kikubwa zaidi mi nnachoona hizi sheria zetu ndo zinatuponza
 

Andiko lefu sana, lkn vingi hapo ni hisia tu. Kwa hiyo ili uwe askari bongo, lazima utokee chipkiz ya sisiem (mbavu zangu 🤣 🤣 🤣 ). Lkn niongee kwa kifupi tu. wengi wanaochangia uzi huu ni wale exposure yao imefikia,labda sana sana nairobi. lkn kwa mtu ambaye ameenda nchi nyingine za Afrika. Hususan ni za kusini kama Botswana, Namibia na sasa Angola. ukiwahi fika nchi hizi na kujua siasa zake, hutakuja tena kuongea kuhusu nchi ya kenya. a bandit society, unaipa sifa lukuki wakati kuna uozo uliopitiliza. Nchi haina udhibiti, kuna sehemu watu wanajilinda wenyewe na smg. Halafu unakuja na maneno meengi ya kusifia vitu usivyovijua. Kenya is like a jungle, everyone is striving hard to make a living, otherwise you will be eatenby your fellow people. Ndiyo maana kule pokot wana mifugo mingi, na wako katika hatari ya kuvamiwa na kuuawa huku wakiporwa mifugo yao, lkn serikali haifanyi kitu. matokeo yake wananchi wa kule wamejinunulia smg kutoka wanakokujua wao wenyewe, ili wajilinde. serikali ya kenya wala haina habari na hilo. Yaani ni shida. lkn cha kushangaz unasifia mpaka unatia huruma. kwa kifupi, nenda nchi hizo nilizo kutajia halafu ulinganishe na kesha, nadhani utakuwa na mtazamo uliobadirika na bora zaidi.
 
wacha Wivu Mingi WWE😆
 
Ata Nigeria na Liberia Kuna Usalama hatari,heri Kenya Usalama uko shwari😏Na usisahau wame border Nchi amabazo zimejaa Terrorists Lakini Bado Kenya iko Imara bana🔥🇰🇪🔥Wacha kudanganya watu wwe
 
Being a son of a gun doesn't mean you've lost life direction buddy. Pili,laiti ungejua naandika nikiwa wapi,usingetoa mifano ya hizo nchi za ajabu ajabu! Pole sana kaka
 
Being a son of a gun doesn't mean you've lost life direction buddy. Pili,laiti ungejua naandika nikiwa wapi,usingetoa mifano ya hizo nchi za ajabu ajabu! Pole sana kaka

Bado hizo ni hisia tu, jibu hoja. Hatuongelei wapi kila mmoja wetu anakoandikia. Maana hilo halitusaidii.

Kwa taarifa yako nchi unazoziita za ajabu ajabu, ndiyo nchi ambazo zinapigiwa mfano Afrika.
 
Ata Nigeria na Liberia Kuna Usalama hatari,heri Kenya Usalama uko shwari😏Na usisahau wame border Nchi amabazo zimejaa Terrorists Lakini Bado Kenya iko Imara bana🔥🇰🇪🔥Wacha kudanganya watu wwe

Jibuni hoja jamani. Naelezea what is the mood on ground in Kenya. Nyie mnaongea mambo yasiyo eleweka.
Mengi tutaelewana kipindi cha uchaguzi 2022.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…