Ni Magufuri ndio alivuruga
Siku mtakayokubali kuwa Mwamba hayupo tena ulimwenguni, ndio siku mtakayo pumzika kuteseka INGAWA kovu haliponi.
Ni hivi, mimi binafsi, kama nisipoingia Jamii forums, nikaona HEADINGS za chawa, huwa sina taarifa yoyote ile ihusuyo serikali na kizimkazi, sisikii popote pale!
Enzi za mwamba, sihitaji simu wala runinga kujua yanayoendelea serikali na kwa mwamba, nikitoka nje ya nyumba tu, wananchi wanazungumza na wako well informed.
Kwa sasa, sio tu hawana taarifa, ila hawana hata interest na taarifa zenyewe; chawa inabidi wapige kampeni ya kuelezea na kueneza habari ambazo hazina hata uhalisi na hivyo kutokuwa na mvuto!
Inabidi zibandikwe na kusambaza picha ili kulazimisha wananchi kuona na kumfahamu kizimkazi, wampende kwa lazima; bahati mbaya sioni huo muitikio huku kijijini kwetu.
Wale mabingwa wa kutangaza DENI LA TAIFA enzi zile, saa hii nasikia wengine wanatangaza KUSTAAFU, maana lililopo enzi hii, ni KUFURU.
Bajeti halisi ya kisiwa haizidi bilioni 500, ambapo walikuwa hawazipati zote mpaka mwaka unaisha, UNAENDA KUCHUKUA MKOPO, unampa bilioni 400 kwa pamoja KISHA unamsifia anafanya maendeleo? Ulitaka afanyie nini hizo pesa ambazo hawajawahi kuzigumia kwa pamoja?
Maisha yapo huku chini, katika population ya watu 62m, ni watu wasiozidi 10m ndio wenye kufanya kazi, biashara, siasa, ufisadi, wizi n.k ambapo 7m wapo Dar; watumishi wakiwa hawafiki 1m.
Watu takribani 50m hawana access na sh 2000 kwa siku, watu wasiozidi 6m wanagawana trilioni 36 kwa mwaka!
Hakuna kinachoendelea chini ya hii FREE BOAT style of governing.
Itoshe kusema, sisi bodaboda, unafuu wetu ulikuwa enzi za MWAMBA, ninyi WAKWAPUAJI, ugumu wenu ulikuwa enzi MWAMBA.