Hatuwezi kupeleka Mahakamani zuio la makubaliano ya Bandari kati ya DP World na Serikali?

Hatuwezi kupeleka Mahakamani zuio la makubaliano ya Bandari kati ya DP World na Serikali?

Baba jayaron

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2015
Posts
4,324
Reaction score
5,933
Natumaini mu wazima na wavumilivu wa hali kwa jina la Mwenyezi.

Kabla ya yote nimpongeze kijana Bwana Wangwe kwa ushindi mkubwa alioupata kwa niaba ya watanzania wote. Ushindi wa zuio la wakurugenzi kusimamia uchaguzi mahakamani ni kuchonga barabara ya haki iliyokua iki kanyagwa mara kwa mara na mtawala wa taifa hili CCM.

Ikiwa ni utaratibu ule ule wa serikali yetu kutumia Amani yetu vibaya kwa kuvunja sheria na utu wetu kwa kutuamulia maamuzi yanayotuacha na maumivu makali na hata kutucost uhai wetu.

Ikiwa makubaliano ya awali kati ya DP WORLD na serikali kutiliwa shaka kwa raia wengi kutoka kada mbali mbali na kupitishwa na Bunge lenye mlengo mmoja tena wakiwemo na wabunge waliohusika "kudalalia" mkataba huu kwakupelekwa Dubai na kugharamiwa kila kitu (HONGO) na kampuni hio, na jinsi serikali inavotumia nguvu kuficha madhaifu ya mkataba huo.

Ni muda sasa wanaharakati kutumia njia hii ya kudai haki mahakamani pengine inaweza kuleta mwanga wa mabadiliko nchini.

Kelele hizi zimezoeleka kiasi ya kuwa kama kelele za chura ambazo hazijawahi kumnyima tembo kunywa maji na maamuzi mengi machungu yamepita kwa kudharau sauti za wananchi wachache waliopata uelewa kulinda wengi wenye uelewa mdogo.

Kwenu wataalamu wa sheria nchini na wanaharakati. Je, hatuwezi kufungua kesi ya ZUIO LA KUSAINIWA NA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA MAKUBALIANO KATI YA SERIKALI YETU NA KAMPUNI YA DP World?

Ikiwa ni kwa utaratibu wa ku sign petition au hata kama kutahitajika gharama watanzania tuchange kunusuru taifa letu kwenda kutafuta haki popote duniani kwakua kuhusu kuandama imeshindikana kutokana na uelewa mdogo pamoja na ugumu wa maisha.

Cc
Pascal Mayalla
Yericko Nyerere
Mzee Mwanakijiji
 
Naunga mkono hoja yako, ukiachilia mbali kesi kufunguliwa na individuals, pia nawasubiri Chadema waongee na waandishi wa habari nione kama watakuja na solution juu ya hili, wanao wanasheria wazuri wanaozijua sheria na taratibu za kimataifa, ni vema nasi tuungane na mataifa mengine yaliyowafungulia kesi hao waarabu matapeli.
 
Bora tuwalipe faini ya kuvunja mkataba kuliko kuwauzia bandari zeru
 
Naunga mkono hoja yako, ukiachilia mbali kesi kufunguliwa na individuals, pia nawasubiri Chadema waongee na waandishi wa habari nione kama watakuja na solution juu ya hili, wanao wanasheria wazuri wanaozijua sheria na taratibu za kimataifa, ni vema nasi tuungane na mataifa mengine yaliyowafungulia kesi hao waarabu matapeli.
Nadhani kama kuna id zao zinajulikana humu tuwaite waje tukikaa kimwa hasara itakua kubwa saana
 
Back
Top Bottom