Hauhitaji kuwa mkamilifu bali Unahitaji kufanya

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Watu wengi miongoni mwetu tunahitaji kuwa wa baba bora/ wa mama bora lakini hatujaamua kuwa wazazi,,wengine wanahitaji kuwa wanamuziki wazuri lakini hawajaanza kuimba bado, wengine wanahitaji kuwa wafanyabiashara wakubwa lakini hawajaanza biashara bado.

Tunachohitaji ni kufanya kwanza kisha ukamilifu utakuja baadae,ndani ya kufanya jambo ndio humo humo utakuwa yule unayetaka kuwa na si nje ya hapo.

Unataka kuwa mwandishi bora,,basi anza kwanza kuandika halafu kupitia kuandika kwako utajikuta kupitia makosa ya hapa na pale unakuja kujifunza kuwa mwandishi bora,,,mara nyingi tuna wasoma watu katika komenti kwamba wana story ya kuandika lkn wanasema sio waandishi wazuri,,je utakujaje kuwa mwandishi mzuri kama hujaanza kuandika.

Ndugu zangu tusitake ukamilifu/ perfection kama hajuamua kufanya jambo,,siku zote azimia kufanya jambo au kitu kwanza halafu ukamilifu ndio utafuata

Kadri jinsi unavyofanya jambo fulani mara kwa mara ndio kadri utakavyo kuja kuwa bora zaidi,,ndio maana hata waajiri wanapenda kuajiri watu wenye uzoefu kwakuwa kupitia kufanya wamepata uzoefu na kuwa bora zaidi.

Kwahiyo usiogope kufanya jambo katika maisha yako kisa tu haujawa bora katika jambo hilo,just do it no matter what then perfection will come later

Hao ambao tunawaona leo wamekuwa bora hawakuanza katika ubora tu laa! Bali walianza kwa kuchechemea hlf baadae wakaja kuwa wakamilifu hata wewe pia mwisho wa siku utakuja kuwa mkamilifu

Just do it
Just do it
Just do it

Ni hayo tu!
 
Asante
 
Back
Top Bottom