Baadhi ya hizi nyimbo zinanikumbusha Tanzania iliyokuwa na neema. Viongozi waliokuwa na mapenzi ya kweli na nchi yetu na siku zote waliweka maslahi ya nchi mbele kuliko maslahi yao wenyewe. Tanzania ambayo ilikuwa na chakula kingi mno. Kulikuwa hakuna haja ya kuweka magunia ya vyakula ndani ya nyumba. Mchele ulikuwa unanunua kwa kunusa na kuangalia upi ambao una vijiwe na chuya nyingi na ule unaonukia harufu nzuri. Ukienda dukani kuna michele ya aina tano au zaidi pamoja na bei zilikuwa zinatofautiana kidogo lakini zilikuwa ni poa mno, hivyo kuwawezesha Watanzania wengi kumudu milo mitatu kwa siku. Inanikumbusha kima cha chini cha mshahara wa shilingi 240 lakini kulikuwa kinatosha kabisa kulipa pango, usafiri wa kwenda kazini, kwenda kwenye burudani mbali mbali zikiwemo za sinema na mziki na bado ulikuwa unaweza kujiwekea akiba bank. Inanikumbusha shilingi ishirini ya Tanzania sawa na pound moja ya UK na shilingi tano ya Tanzania sawa na dollar moja ya Marekani. Inanikumbusha hospitali zetu kubwa zilizokuwa na vitanda, vifaa vya kisasa na madawa. Kulikuwa hakuna mgonjwa aliyelala chini au kuchangia kitanda na wagonjwa wengine watano au zaidi.
Inanikumbusha Tanzania iliyokuwa haina mafisadi kama akina fisadi Mkapa, Fisadi Lowassa, fisadi Sumaye, Fisadi Kikwete na mafisadi wengine chungu nzima ndani ya chama na serikali ambapo kila kukicha wanahaha jinsi ya kujiongezea utajiri wao kwa kuwadhulumu Watanzania mali zao mchana kweupe. Inanikumbusha shule zilizokuwa na hadhi ya kuitwa shule, wanafunzi wote walikuwa wanakalia madawati na shule zenye vyoo. Inanikumbusha Tanzania yenye amani ambapo ilikuwa ni nadra sana kusikia mambo ya ujambazi kama ilivyokuwa leo. Wengine mtazikumbuka baadhi ya hizi nyimbo na wengine si ajabu mkawa mnazisikia kwa mara ya kwanza.
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=S63AtiBYMiU[/ame]
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=N1skN6m1GHA[/ame]
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=0zCH0UNK4dI[/ame]
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=RV1n6sfjJBE[/ame]
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=nfm8-uSohsQ[/ame]
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=1Zgtx5EWw3I[/ame]
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=cBSP2W2Tf80[/ame]
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=TlmNF5nc54w[/ame]
Anacheza kwa madaha, anacheza kwa kujidai na kiuno alikuwa pia anakiweza
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=JzKR7EJBivY[/ame]
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=LVC_tHEaIyw[/ame]
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=rm9BkZgKkvA[/ame]
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=sP-7QHSNe20[/ame]
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=-J15J-j7grs[/ame]
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=9URwhcS1OxE[/ame]