My dia mimi sidhani kama ni punishment, yaani kuna kitu nimejifunza kabisa sasa siwezi mlaumu mtu eti amenitenda tena niliowahi kumlaumu anatosha kabisa.
Kama mtu ananifuata na utu uzima huu (sikilizeni kwa makini wadada mlioko kati ya 18 mpaka 29) mtu amekufuata hajakubaka mmeenda enda baadae akajiondokea zake basi chukulia huyo hakupangwa kuwa wako.
Ndio maana nikasema jiulize wewe hujawahi mkataa mtu? na yeye mpe uhuru wa kukukataa kama na wewe ulivyokataa uko tena kwa uzuri tu. Itakuwa punishment kama uliowakataa uliwakataa kwa kuwakomoa lakini kama hukuwakataa kwa kuwakomoa jua kwamba hata huyo anaekukataa sasa hakukomoi imetokea tu hawezi endelea na wewe (kwani inasemwa kipimo unachopima ndio utachopiwa)/
Mimi sasa hivi naishi kwa amani sana baada ya kuligundua hili, nikiona dalili za kutoswa tu naanza kurefer nyuma mbona na mimi nilifanyaga hivi, poa maisha yaendelee tu, namuachilia aende hata kabla hajaaga jumla.
Naamini kabisa kila jambo unalolitenda katika haya maisha ndivyo linavyorudi liwe zuri au baya kila mtu anavuna alichopanda hapa hapa duniani (jaribuni kujichunguza kwa makini halafu mtanielewa)