Hawa AIRTEL ni matapeli kabisa hasa kwenye kifurushi chao cha MB 850 cha shilingi 1500

Mi kuliko kujiunga huo upuuzi bora hata Mb 800 za vodq kwa 1500 zinakaa japo kdg

Nilijiunga huo uzuzu sikutumia sana hata siku haijaisha Mb 850 zikaishq
Nilishangaa sana
 
Kwangu Mimi naona siku hizi voda bando linaenda vzr Sana(kwa experience yangu) lkn nao zamani walikua Kama Airtel.
Mimi nina 18+ yrs na voda, angalau sasa hivi kidogo naona wameshaanza kujishtukia na kubadilika kwenye data, kuna muda niliwaza niitupe line yao kabisa ingawa maumivu bado yapo. Kuna siku data inaisha haraka na hujafanyia kitu cha maana, na kuna siku linakaa mpaka unawaza wamesahau kuzima au kuna ofa.

Wanachonikera tu ni kuunganisha wateja kwenye huduma bila ridhaa yao.
 
Mbona Tigo ni 750 MB kwa Tshs 1500
 
Mimi mwenyewe huwa nashangaa sana Airtel kuna kifurushi cha Shilingi Elfu 10,000/= cha Mwezi mitandao yote, sms na 4 GB lakini ukishajiunga hizo GB zinabadilika zinakuwa MB ukiwasha Data kidogo tu zinayeyuka tu, Airtel mnatuumiza wateja wenu fanyieni kazi hili tatizo.
 
Mkuu sasahivi tunaipata pata hakuna mtandao wenye afadhali wizi mtupu ila siku yao ipo.
 
Hahahah mkuu airtel sio watu wazuri kabisa leo ndio nimerud online daahh
 
Mkuu nirudi mtandao gani sasa VODA ama TIGO?
 
Unaweza kuwa umezima data lakini bado wanakuletea sms kwamba umemaliza bando..sasa limetumikaje wakati nilikuwa nimezima matumizi ya data?!
Hahahaha nashukuru kwa kulitambua hilo mkuu wengi hawajui khaaaaaa!
 
Reactions: BRN
Mkuu nirudi mtandao gani sasa VODA ama TIGO?
Nipo Voda ,Tigo na Halotel

Voda hawa Mb zao zipo vizuri vifurushi vinaisha kihalali bila longolongo ila bei zao za juu mfano mimi najiunga cha buku 1.7Gb wiki 2 naperuzi bila wasi .


Halotel Mb zao za uongo mara nyingi uongo ukiweka hata Gb2 chap hamna salio na nimewahi kuchunguza kwenye data usage details nakuta nainibiwa kama Mb 150 mpk 160 kwenye GB 2 ,wao wanasema zimeisha ila ukikagua kwenye mahesabu hola.

Tigo sijaona shida yeyote wapo kawaida tu.
 
Nashukuru mkuu bora nilejee vodacom tu maana hali mbaya kwa kweli nimechoka kuperuzi kwa mashaka hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…