Hawa 'Be Forward' wapo serious kweli?

Rene jr ya kweli haya

sijui BIGURUBE anatumia vigezo gani kusema hivyo. muhimu angalia miliage ya gari isiwe kubwa saana. hebu jaribu kusort low tu high kisha angalia milage, ukipenda gari fungua picha kagua kwa uangalifu kuona kama lina mikwaruzo, angalia kwenye dash kama kuna taa yoyote ya error inawaka, kagua chini ya gari (beforward ni kati ya kampuni chache wanazoweka picha za kutosha mpaka chini ya gari) kagua tairi kama hazijawa kipara, kagua usafi wa ndani, utajua tu kama gari imefujwa. nijuavyo mimi beforward wana mbinu zao tofauti tu za kufanya biashara, uza bei ndogo, uza nyingi...na ukikuta promo kama hivi ndiyo wanasafisha ghala unauziwa bei cheap. pia ukipenda fanya ulinganifu wa gari uliyoipenda, same mile age, same color uone wauzaji wengine watakupa quotation ya bei gani. usifuate sana maneno ya wakina sisi, fanya utafiti.
 
Last edited by a moderator:

mkuuu umwongea kweli la msingi ni kufanya utafiti lakini pia kutumia wazoefu kama huwezi
 
Last edited by a moderator:
hawa jamaa sio wauongo tatizo ni moja tu
chaj ya kusafirisha ni mara 10 mpaka 20 ya bei ya kulifikisha hapa kwa nyerere
imagne gari ni dola 200 hadi 400 mpaka lifike ni dola 1400 sasa hapo ujalipia ushuru na takataka zingine


mkuu, usafiri ni juu ya wenye meli, inategemea na ukubwa wa gari. ila kwenye ushuru ndiyo yalipo mabalaa, lakini tutafanyaje sas wakati wawakilishi wetu ndiyo wametupangia hivyo, nadhani wao wanaona gari ni anasa.
 
hawa jamaa sio wauongo tatizo ni moja tu
chaj ya kusafirisha ni mara 10 mpaka 20 ya bei ya kulifikisha hapa kwa nyerere
imagne gari ni dola 200 hadi 400 mpaka lifike ni dola 1400 sasa hapo ujalipia ushuru na takataka zingine

Kwenye issue ya kusafirisha hapo sina complains maana sio wao wanaosafirisha.
 
hivi yule dada mwenye kalio la haja pale be forward yupo?
 
:car:hakuna matata.gari zao zipo fiti.ofisi zao ziko maeneo ya ocean road dsm fika utaeleweshwa.
 
mkuuu jeshi la wokovu na beforward kuna uhusiano gani

Jeshi la wokovu ni kanisa ambalo nchi zilizoendelea huwa wanasaidia watu wasio na kipato mfano wakimbizi, au we ukienda kupiga box afu ukashindwa.

So wanakusanya 2nd hand items na kugawa free au very cheap
 
masai dada na Ukwaju nimeiona gari yenu, CIF $2521 (MPAKA DAR), kama mko serious semen mtumiwe invoice mlipie.
Kweli Mkuu hiyo gari naihitaji sana ila kutuma au kujaza invoice nshaona kizunguzungu ni bora nije niichukulie kwako au Be Forward hapo DSM
Je gharama zitavuka 5m maana naona umetaja CIF wakati bado TRA na vingine
nina 5m kwani nataka niachane na Carina
 
Jeshi la wokovu ni kanisa ambalo nchi zilizoendelea huwa wanasaidia watu wasio na kipato mfano wakimbizi, au we ukienda kupiga box afu ukashindwa.

So wanakusanya 2nd hand items na kugawa free au very cheap

hahahh yaani ili neno kupiga box huwa linanichekesha sana
 
  • malizana na bwana Ukwaju alafu mimi nikutafute sasa
  • mkuu usijali namuendesha bosi mmoja hapa siku nikitumwa nitakupa lift
Bahati iliyoje, nikimalizana na Rene jr brake ya kwanza ni hapo Be Forward wananielekeza ipo Ocean Road (Barack Obama)
nikikosa lift yako basi hata nipate ukweli wa bei ya hizi gari kwa hela ya madafu
 

duu, hiyo haitoshi mkuu, ushuru na ghalama za bandarini tu ni zaidi kidogo ya 5m.
mpaka kuitia mkononi itakaribia 10M kaka.
 
duu, hiyo haitoshi mkuu, ushuru na ghalama za bandarini tu ni zaidi kidogo ya 5m.
mpaka kuitia mkononi itakaribia 10M kaka.
Mkuu ni bora unitafutie hapo DSM kwani zoom tanzania wanazitangaza nzuri na zenye mileage ndogo kuliko za Japan na huenda ukaagiza ukatapeliwa, Meli ikapata ajali Bandarini ukaibiwa
Hizi za 5m zina Road licence na Bima ya hapa kwetu
Tembelea hii niliyoikosa juzi trh 4/Feb/2015
Rene Jr. zunguka tena hapo Mjini hutakosa
1998 Toyota Noah For Sale in Dar Es Salaam, Tanzania | Classified
 

noah old model ya 5M ni kubahatisha, au la imetumika sana, au imetumika sana. mara nyingi zinapotokea za kubahatisha walengaji wanazichukua faster kama iko vizuri kisha wanauza kwa bei ya juu, ndiyo maisha yenyewe ya mjini mkuu. zikitokea za hivyo nitakushtua, si una mtu wa kukagua gari hapa mjini?...maana za hivyo huwa ni fast deal, ukichelewa kidogo tu watu washalipa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…