Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
SERIKALI IJIANDAE KUWATETEA DP WORLD KWA SABABU AJIRA NA MAPATO YA BANDARI YATAKASHUKA MNO!
Hawa DP WORLD siyo wawekezaji bali ni mchwa. Tuna mapigo matatu yanahusiana na huu uwekezaji wa kifisadi yanakuja bila kuchelea.
Pigo la kwanza mapato yatashuka kinyume na matarajio yao. Mapato ya wateja wa bandari ya Dar-es-Salaam yatashuka kutokana na kudorora kwa uchumi wa dunia na hawatasafirisha mizigo mingi.
Pigo la pili baada ya TPA kuporwa ugali itabidi wapunguze ajira kutoka wafanyakazi 3, 450 hadi 600 tu. Serikali iliahidi ajira kutoathirika lakini ukweli zitapungua mno.
Pigo la tatu, mizigo haitaongezeka bali itapungua. Wao wanadai ufanisi utaongeza tashwishwi ya kutumia bandari ya Dar lakini uhalisia sababu kuu ya kupanda matumizi ya bandari ni kasi ya kukua GDP. Na kila kipimo kinaonyesha mapato ndani ya SADCC yatashuka.
Wajiandae kumtetea mwekezaji kwa kushindwa kuongeza mapato na kukaza buti kutukamua kwa kodi kufidia pengo la mwekezaji hewa.
Sisi wengine ni mbavu zetu tu zitakazo kuwa hoi pale matutusa watakapobainika walidhani wanajua kumbe hawajui kitu.
Mfupa ulilolishinda jimbo la Delaware Marekani sisi ndiyo kabisa tusubirie porojo za kwanini mapato na ajira zimetoweka.
Jimbo la Delaware lina mkataba bora kuliko huu wetu wa kitumwa lakini hadi sasa miaka 6 imepita hawajalipwa hata senti moja na DubaiTainer pamoja na mizigo yao kuwa karibu mara tatu ya bandari ya Dar-es-Salaam. Mara wamesingizia kovid na sasa wanajitetea uchumi wa dunia umeyumbishwa na vita vya Ukraine, vikwazo vya uchumi dhidi ya Urusi na Uchina n.k