Hawa Form 4 & Form 6 wanaopata ajira TRA huwa wanaajiriwa sekta ipi?

Dah kweli man
 
Huwa wanatoa vigezo vyao ila kwa nafasi za kawaida wanaanzia Diploma ,degree na vyeti vinavyolingana na hivyo.Kwa nafasi za chini kama karani au wahudumu nadhani form 4 ambaye ana alama zinazoridhisha. Ila nikushauri kama ni form 6 jiendeleze au hata form 4 bado unayo nafasi usikate tamaa na ajira siyo mpaka kwa hao tra unaweza jiendeleza vizuri na ukapata hata sekta binafsi na maisha yakasogea au ukawa na kitu chako cha msingi pambania kupata maarifa zaidi ndiyo msingi.
 
Haya bwana mkuu
 
Truck driver form four haitoshi ana cheti cha udereva ambayo ni taaluma kama ni hivyo mbona kuna masecretary nao utawaita form four? Mafundi umeme,bomba,AC nao wameajiriwa TRA nao utawaita form four? Kiufupi tra haina ajira ya form four hata wapishi na wahudumu wana vyeti vya taaluma za fani zao.

Namshauri kijana atafute taaluma yeyote inayoweza kumsaidia kuajirika tra atapata kazi.
 
Nadhani kwa form four ni udereva ingawa lazima awe na cheti Cha udereva. Kuna secretary, at least uwe na cheti Cha secretarial.
 
Udereva ni taaluma kama taaluma nyingine na sio kuishia form four tu haitoshi kuwa dereva
Nadhani kwa form four ni udereva ingawa lazima awe na cheti Cha udereva. Kuna secretary, at least uwe na cheti Cha secretarial.
 
Umejibu vyema mkuu japo wanakaza fuvu,kwa Sasa hivii ni ngumu saana kuajiriwa ukiwa na cheti Cha form four au form six peke yake bila kuwa na cheti Cha fani?? Nashangaa mtu kabisa na akilii zake anasema dereva mbona ni form four 😂😂bila kusahau kuwa udereva ni fanii kama fanii zinginee na unasomewaa,au ni kwa vile waafrika tumekalili kuwa ukiendaa kusomea udereva ni umefelii form four
 
Hawajui haya mambo yalivyo mtu akikuta mtu kashika spana anarekebisha ac na kaajiriwa anamwita form four na wakati ana taaluma yake majeshi pekee ndo kuna form four ila kwingine lazima uwe na cheti cha taaluma
 
Hawajui haya mambo yalivyo mtu akikuta mtu kashika spana anarekebisha ac na kaajiriwa anamwita form four na wakati ana taaluma yake majeshi pekee ndo kuna form four ila kwingine lazima uwe na cheti cha taaluma
Hata jeshini lazima upewe taaluma ndio ajira kamili ikufikie,usipo pata taaaluma ya kijeshi huwezi kuwa askari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…