Hawa hapa member wa JF na sifa zao za kipekee

Ladies and Gentlemen salaam!

JF ni jukwaa linalotuunganisha watu mbali mbali ambao kimsingi kila mmoja ana sifa zake za kipekee katika uchangiaji, mwonekano wa kitaswira na pia katika uwasilishaji wa hoja binafsi. Sasa leo baada ya kufanya utafiti mdogo nimeona nikudondoshee member hawa wa JF na sifa zao za kipekee "peculiar characters"

MSHANA JR
Ni mtaalamu wa masuala ya imani za ulimwengu wa pili na post zote zinazohusiana na imani hizo za uchawi na ushirikina basi ni rahisi sana kuona member huyu akitajwa kwa lengo la kutoa elimu ama ufafanuzi wa jambo hilo. Mbali na ubobezi huo pia ni mchambuzi mzuri wa masuala mbali mbali ya kisiasa na kijamii ya kitaifa na kimataifa.

JOANAH
Huyu anaonekana kuvutiwa na wengi hasa wakiume hali inayopelekea wamwanzishie nyuzi za kueleza hisia zao kwake. Hii inaonyesha huyu ni binti mrembo asiyependa makuu na pia ni mchangiaji mzuri katika jukwaa hili la JF.

GENTAMYCINE
Huyu anaonekana kuwa na karama ya kuja kuwa mchambuzi mzuri kwa siku za usoni japo kwa sasa hoja zake zinakuwa kama hazieleweki na anatumia nguvu kubwa kuaminisha umma kwamba yeye ni genius wakati sifa hiyo hana. Kwa kifupi ni mtu fulani mwenye kupenda kujivuna hata kwenye vitu ambavyo anapungukiwa.

WARUMI
Ni mdadabuzi na mfukunyuzi wa habari na masuala ya udaku yanayohusu watu maarufu "celebrities". Kwa kifupi ni mtaalumu wa masuala ya udaku.

ZERO IQ
Ni mtu asiyependa makuu na mara kadhaa hoja zake zinasadifu jina lake japo ukizisoma utaishia kutabasamu kama siyo kufurahi. Kwa kifupi jamaa ni comedian mzuri kwenye jukwaa.

VIATU VYA SAMAKI
Huyu ni mbishi wa kusimamia anachokiamini akianzisha jambo mpaka alimalize. Kwa kifupi ni mtu mwenye msimamo

FAIZA FOXY
Ana uwezo wa kufikiri na kuandika lakini ni mtu fulani wa kupenda kukosoa sana na kuwakejeli wengine kwa kudai walienda shuleni kusomea ujinga. Kwa kifupi ni mtu wa kupenda kujivuna na kuwachukulia wengine katika nyanja ya ujinga.

MK54
Huyu ni mpambanaji"fighter" ana juhudi ya kutafuta habari kisha kuidadavua kwa kina kwa lengo la kutoa elimu kwa wengine. Mbali na hilo ni mbobezi na mchambuzi mzuri wa masuala mbali mbali katika nyanja zote za kiuchumi, kijamii, kisiasa n.k kitaifa na kimataifa. Kwa kifupi huyu ni mpambanaji
SKY ECLAT
Ni mpole na pia ni mchangiaji mzuri katika jukwaa hili la JF.

Orodha nyingine itafuata siku zijazo. Mwenye pingamizi, maoni tofauti au nyongeza anakaribishwa.
Umejiunga JF juzi tu (04/06/2019) na umeshatutathmini na kufahamu "sifa" zetu "za kipekee"!

Wewe kweli sumu.

Majanga!
 
Aisee ntakuja nikuungishe best angu!
Mbwa dume: huyu alikuwaga mwizi wa mafuta ya transfomer siku hizi alishaacha hiyo mambo amejiajiri kama muuzaji maarufu wa majeneza jijini Dodoma
 
Ladies and Gentlemen salaam!

JF ni jukwaa linalotuunganisha watu mbali mbali ambao kimsingi kila mmoja ana sifa zake za kipekee katika uchangiaji, mwonekano wa kitaswira na pia katika uwasilishaji wa hoja binafsi. Sasa leo baada ya kufanya utafiti mdogo nimeona nikudondoshee member hawa wa JF na sifa zao za kipekee "peculiar characters"

MSHANA JR
Ni mtaalamu wa masuala ya imani za ulimwengu wa pili na post zote zinazohusiana na imani hizo za uchawi na ushirikina basi ni rahisi sana kuona member huyu akitajwa kwa lengo la kutoa elimu ama ufafanuzi wa jambo hilo. Mbali na ubobezi huo pia ni mchambuzi mzuri wa masuala mbali mbali ya kisiasa na kijamii ya kitaifa na kimataifa.

JOANAH
Huyu anaonekana kuvutiwa na wengi hasa wakiume hali inayopelekea wamwanzishie nyuzi za kueleza hisia zao kwake. Hii inaonyesha huyu ni binti mrembo asiyependa makuu na pia ni mchangiaji mzuri katika jukwaa hili la JF.

GENTAMYCINE
Huyu anaonekana kuwa na karama ya kuja kuwa mchambuzi mzuri kwa siku za usoni japo kwa sasa hoja zake zinakuwa kama hazieleweki na anatumia nguvu kubwa kuaminisha umma kwamba yeye ni genius wakati sifa hiyo hana. Kwa kifupi ni mtu fulani mwenye kupenda kujivuna hata kwenye vitu ambavyo anapungukiwa.

WARUMI
Ni mdadabuzi na mfukunyuzi wa habari na masuala ya udaku yanayohusu watu maarufu "celebrities". Kwa kifupi ni mtaalumu wa masuala ya udaku.

ZERO IQ
Ni mtu asiyependa makuu na mara kadhaa hoja zake zinasadifu jina lake japo ukizisoma utaishia kutabasamu kama siyo kufurahi. Kwa kifupi jamaa ni comedian mzuri kwenye jukwaa.

VIATU VYA SAMAKI
Huyu ni mbishi wa kusimamia anachokiamini akianzisha jambo mpaka alimalize. Kwa kifupi ni mtu mwenye msimamo

FAIZA FOXY
Ana uwezo wa kufikiri na kuandika lakini ni mtu fulani wa kupenda kukosoa sana na kuwakejeli wengine kwa kudai walienda shuleni kusomea ujinga. Kwa kifupi ni mtu wa kupenda kujivuna na kuwachukulia wengine katika nyanja ya ujinga.

MK54
Huyu ni mpambanaji"fighter" ana juhudi ya kutafuta habari kisha kuidadavua kwa kina kwa lengo la kutoa elimu kwa wengine. Mbali na hilo ni mbobezi na mchambuzi mzuri wa masuala mbali mbali katika nyanja zote za kiuchumi, kijamii, kisiasa n.k kitaifa na kimataifa. Kwa kifupi huyu ni mpambanaji
SKY ECLAT
Ni mpole na pia ni mchangiaji mzuri katika jukwaa hili la JF.

Orodha nyingine itafuata siku zijazo. Mwenye pingamizi, maoni tofauti au nyongeza anakaribishwa.
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji108][emoji123][emoji106][emoji106][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom