Hawa kweli ni wanangu?

Hawa kweli ni wanangu?

Kaina

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2015
Posts
380
Reaction score
326
Habari wakuu? Moja kwa moja kwenye mada:

Kuna mdada nilikutana nae kimapenzi tarehe 16/04/2023, baadae akadai ana mimba yangu.

Mimi kwa kuwa nilikuwa na mashaka na ile mimba nikajipa muda nione siku atakazokuja kujifungua kama zinaendana na siku nilizokutana nae.

Bahati nzuri akaja kujifungua tar 30/12/2023 watoto mapacha wa kiume.

Basi kwa kiwa nilitaarifiwa mapema nikawa nimeonesha ushirikiano kuanzia gharama za hospital hadi sasa hivi matumizi.

Ila niwe mkweli tangu day one sijawahi kukubali kutoka moyoni kabisa kwamba hawa ni wanangu.

Mashaka ni mengi na sababu za mashaka ni kama zifuatazo:

1. Siku nimekutana nae nilivaa mpira japo ulikuja kuchomoka baadae.

2. Timing yenyewe ya mimba kuingia hadi kujifungua. Mimba iingie tar 16/4 izaliwe tar 30/4?

Kuna mwanamke nilikutana nae tar 1/4/2023 yaani mwezi ule ule tar 1 ila yeye amekuja kujifungua tar 08/01/2024.

Hii inanifanya nazidi kuwa na mashaka na mimba ya huyu wa mapacha.

3. Watoto hawanifanani. Ni weupe sana na mimi ni mweusi na mama yao ni mweusi, chain yetu sote haina watu weupe.

4. Tabia za huyu mwanamke. Alikuwa na wanaume wengi kiasi kwamba kuna watu kadhaa waliikataa hiyo mimba. Hili nilikuja kulijua baadae.

Uzi huu nimeuleta huku kwenye jukwaa la afya nikihitaji hasa msaada wa wataalam mnisaidie kunipigia hesabu ya hiyo mimba.

Inawezekana mimba mimba kuingia na kuzaliwa ndani ya tarehe tajwa hapo juu?

Maana sotw tunajua mimba ni miezi 9 japo inaweza kuwahi au kuchelewa kidogo.

Msaada kwenu wakuu, maana nipo kwenye wakati mgumu sana na nataka kufanya maamuzi maana nadhani nnaelewa hakuna kitu kinauma kama kulea damu isiyo yako.

Natanguliza shukrani.
 
Wa kwako huyo mzee kama ishu ni timing basi yuko sahihi, mimba ya mapacha mara nyingi huwa haifiki miezi 9 anakua keshajifungua. Mi mwenyew nna mapacha ilichukua miezi 8 na wiki mbili

Kuhusu weupe now ni mapema mno, watoto wote hizaliwa weupe, mpaka mjue rangi halisi ya mtoto huchukua miezi kadhaa

Usikimbie majukumu, umeyatimba
 
Msilete huruma kwenye maisha ya watu. Akawapatie baba yao halali na mimi nikalee ambao ni wangu halali. So far sijaacha kuwalea mpaka sasa
Mbona unatufokea Ungekuwa na msimamo dume usingekuja kulalama hapa!
 
NAKUSHAURI LEO HAO WATOTO MAPACHA BILA UBAGUZI, ikiwezekana mwambie mama yao kuwa unatambua siyo wako ila unalea kwasababu hao watoto hawana hatia. Pole na hongera
 
Back
Top Bottom