Hawa mabinti wawili watanitoa roho

Hawa mabinti wawili watanitoa roho

Ubungo Mataa

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2018
Posts
411
Reaction score
725
Wana bodi, heshima kwenu.

Kadri muda unavyozidi kwendaa ndio nazidi kuchanganyikiwa, sielewi.. moja haikai, mbili haikai.

Niko kwenye mahusiano na mabinti wawili kwa muda miaka 3+ sasa.. Mmoja ni mzuri sana, mrembo, presentable na udambwiudabwi wa kila aina kwenye masula ya mapenzi na mambo ya show off. Kwenye suala la maisha huyu binti ni chenga, sio mpambanaji kivile.. Ila moyo wangu umelala kwake, kidume sipui kabisa pale.

Huyu mwingi ni binti wa kawaida sana, ana heshima zake tuu.. Kwenye uzur ni kawaida sana, sio mtundu sana.. Kwenye show off yeye hayupo kabisa, akisuka yebo fasta mwendo mdundo.. akibana yeye poa tuu, akibana kwa nyuma na raba bendi kama Jumong fresh tuu hana shida. Ila huyu binti ni mpambanaji bana, ni shujaa.. Linapokuwa swala la maisha huyu binti nampa GPA ya 5.0 ila moyo haupo kwake.

Wote wawili wapo tayar kuolewa muda wowote, hata kesho asubuh.

Nashindwa kabisa kuamua hii issue, nani nimchukue kama mke, nani nimpige chinini maana ni zaidi ya mwaka sasa na nikitazama muda unazidi kukimbia. Kwa upande wangu mm nataman vyote kwa pamoja tena kwa 100%.

Msaada wa mawazo yenye fact tafadhali.
 
Kutokana na maelezo yako ni wazi imani yako haikuruhusu kuwa na mke zaidi ya mmoja; ndio maana unaomba ushauri wa nani umuache kati ya hao wawili! Kama unawapenda sana wote wawili badirisha dini ,uende kule unakoweza kuoa mpaka vipusa wanne!!!
 
Oa huyo wa kwanza ndiyoe anakufaa na mnaendana, huyu mwengine utamtesa bure mwache apate atakayempenda na kumfaa zaidi
 
Oa ambae roho yako inamtaka na mapungufu yake..
Huyu mwingine atampata wa kwake
 
Hii hali inanikumba pia mm. Nina mahusiano na mabinti wawili (wote nna mwaka nao wa mahusiano) na wote nawapenda ktk kiwango ambacho nashindwa kumpiga chini mmoja. Hisingekua dini ningeoa wote wawili, bahati mbaya au nzuri wote wawili ni waiislamu na wapo tayari kubadili dini kunifuata,ila mm kubadili kuwafuata wao na kuoa wote wawili naona ni udhaifu mkubwa mnoo.

Eehh Mola nisaidie mja wako kuamua hili swala[emoji120]
 
Bro jitahid umchukue mpambanaji...

Mim pia bro ilo jambo linanitesa sana, kuna binti nimezaa nae mtoto anamiaka mi4 saiz na kuna binti nipo nae kimahusiano saiz, wote nawapenda 100%, nimefeli swala la maamuzi yupi ni yupi maana nilishaapa sitozaa na wanawake tofauttofaut. Nahis kama nataka kuvunja ahad ya moyo[emoji24]
 
Hili swala kumbe linatutesa wengi[emoji28][emoji28]
 
Kukolea kwa wadada wawili hadi kufikia hatua ya wote kuwa tayari kuolewa nawewe ni kujiendekeza vibaya kunakokuja(ga) kuwatesa kwenye maamuzi ya kuoa yupi na maumivu kwa utakayemwacha!

Kwann usikomae na mtu mmoja toka mwanzo..?
 
Wana bodi, heshima kwenu.

Kadri muda unavyozidi kwendaa ndio nazidi kuchanganyikiwa, sielewi.. moja haikai, mbili haikai.

Niko kwenye mahusiano na mabinti wawili kwa muda miaka 3+ sasa.. Mmoja ni mzuri sana, mrembo, presentable na udambwiudabwi wa kila aina kwenye masula ya mapenzi na mambo ya show off. Kwenye suala la maisha huyu binti ni chenga, sio mpambanaji kivile.. Ila moyo wangu umelala kwake, kidume sipui kabisa pale.

Huyu mwingi ni binti wa kawaida sana, ana heshima zake tuu.. Kwenye uzur ni kawaida sana, sio mtundu sana.. Kwenye show off yeye hayupo kabisa, akisuka yebo fasta mwendo mdundo.. akibana yeye poa tuu, akibana kwa nyuma na raba bendi kama Jumong fresh tuu hana shida. Ila huyu binti ni mpambanaji bana, ni shujaa.. Linapokuwa swala la maisha huyu binti nampa GPA ya 5.0 ila moyo haupo kwake.

Wote wawili wapo tayar kuolewa muda wowote, hata kesho asubuh.

Nashindwa kabisa kuamua hii issue, nani nimchukue kama mke, nani nimpige chinini maana ni zaidi ya mwaka sasa na nikitazama muda unazidi kukimbia. Kwa upande wangu mm nataman vyote kwa pamoja tena kwa 100%.

Msaada wa mawazo yenye fact tafadhali.
Nipe namba zao,harafu subili siku mbili uwapigie,utapata jibu,vijana wasiku hizi mna matatizo gani?!watu wanawaza kwenda kuishi kwenye sayari nyingine,wewe unashindwa kuamua ishu ndogo kama hiyo!?
Ur a stain in menhood.
 
Kukolea kwa wadada wawili hadi kufikia hatua ya wote kuwa tayari kuolewa nawewe ni kujiendekeza vibaya kunakokuja(ga) kuwatesa kwenye maamuzi ya kuoa yupi na maumivu kwa utakayemwacha!

Kwann usikomae na mtu mmoja toka mwanzo..?
Na siku zote utaye mchagua ndiye wrong selection mbeleni.
Sijui kwa nini??!!
 
Back
Top Bottom