Hawa maslay queen bwana, soma na wewe

Hawa maslay queen bwana, soma na wewe

Makonde plateu

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2022
Posts
1,443
Reaction score
3,480
⚠️😭 Socialite huyo wa Nigeria kwa jina la Benjamin(Killaboigram) ambaye ana miaka 26 amekiri na kujutia kumuua mpenzi wake huyo kwa jina la Austa ambaye pia ni socialite baada ya kutokea ugomvi baina yao

Alimuua katika nyumba aliyokuwa anaishi, ilijulikana baada ya familia ya mwanamke kumtafuta ndugu yao bila mafanikio na baadaye kukutwa ameuliwa huku ikidaiwa alikatwakatwa mwilini

Benjamin amejitosa mtandaoni kukikiri kufanya uhalifu huo na kusema anajuta sana kwa alichokifanya kwani na yeye ameshayaharibu maisha yake katika umri wa miaka 26 tu alionao

Killaboigram au Benjamin anamedai alikuwa kwenye mahusiano yasiyo sahihi yaliyojaa sumu na anatamani muda ungerudi nyuma akakajiepusha mapema na mahusiano husika japo Austa alikuwa mwanamke aliyempenda na yeye sio mtu mbaya licha ya kuua

Killaboigram amesema ameamua kukiri wazi alichofanya sababu tangu afanye mauaji ya mpenzi wake huyo yeye mwenyewe hana amani kabisa na pia yupo tayari apate hukumu anayostahi, yupo tayari kwa ajili ya kifo pia

Killaboigram amejiomba msamaha mwenyewe kwa kuharibu maisha yake katika umri mdogo, amemuomba msamaha mama yake na ndugu yake wa pekee ambaye ni wa kiume kwa alichofanya

Killaboigram na mpenzi wake wote kwa pamoja mitandaoni waliluwa wakiachia mapichapicha kuonesha wanaishi maisha mazuri ya kifahari

Lakini kabla ya mauaji aliyofanya, miaka miwili iliyopita Killaboi aliwahi kudakwa na na vyombo vya sheria Nigeria kwa kudaiwa kujihusisha na vitendo vya kitapeli

FB_IMG_1689880197656.jpg
 
Hii storyy ni ya kweli.Huyu kaka ana hela na alikuwa akimpatiq mwanadada (marehemu)lifestyle za mbele.Kwa madai yake katika ugomvi alijikutq amemchoma kisu kwa bahati mbaya
 
Back
Top Bottom